Kuna sera kadhaa za transactions ambazo ni muhimu katika suala la uwekaji pesa, utoaji pesa, na internal transfers kati ya akaunti za kutrade. Kujua kanuni hizi kutaboresha matumizi yako ya kuongeza pesa kwenye akaunti zako za kutrade. Makala haya yataeleza sera hizi na kutoa viungo muhimu kwa maudhui yanayohusiana.
- Uwekaji fedha
- Utoaji fedha
Uwekaji fedha
Muhtasari
Ili kutrade, unahitaji kufungua akaunti ya kutrade na kuweka funds kwenye akaunti hiyo. Kila akaunti mpya ya kutrade itahitaji kuwekwa pesa kwa mara ya kwanza kabla ya kutumika, na baadhi ya aina za akaunti zina kiwango cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa.
Maudhui yanayohusiana:
Mara tu masharti ya kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza yametimizwa, kiasi kingine cha pesa kinachowekwa kinaweza kuwa cha chini zaidi kinachohitajika na njia ya malipo iliyochaguliwa. Uchaguzi wa njia za uwekaji fedha zinazopatikana hutegemea nchi iliyochaguliwa wakati wa Usajili wa akaunti ya Exness.
Maudhui yanayohusiana:
Kila njia ya uwekaji fedha ina masharti ya kipekee, kama vile vikomo vya chini/juu zaidi vya pesa zinazoweza kuwekwa, muda wa uchakataji, na masharti ya uthibitishaji wa akaunti. Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB) kila wakati ili kuthibitisha taarifa na upatikanaji wa njia za malipo, kwa kuwa zinaweza kuwa nje ya mtandao kwa ajili ya matengenezo. Endelea kusoma kwa sheria za jumla, au ufuate viungo vyovyote hapa chini kwa maelezo zaidi.
Kanuni za kawaida
- Kichupo cha Uwekaji fedha kwenye EB huonyesha njia zinazopatikana kwa matumizi kwanza, kisha zile zenye masharti ya uthibitishaji; thibitisha akaunti yako ya Exness ili kutumia njia yoyote.
- Aina za akaunti za Kitaaluma zina masharti ya kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa, yanayotofautiana na eneo lililosajiliwa. Thibitisha kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa cha aina ya akaunti kwenye makala ya aina za akaunti.
- Aina za akaunti za Standard hazina masharti ya kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa, lakini njia ya malipo itakuwa na kikomo cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa; thibitisha kikomo cha chini zaidi katika EB.
- Akaunti za njia ya malipo sharti zisajiliwe kwa jina lako kamili la kisheria na zilingane na jina lililosajiliwa kwa akaunti yako ya Exness au hatua hiyo ya uwekaji fedha haitafaulu.
- Uwekaji na utoaji fedha hufanywa kwa sarafu sawa kila wakati, kwa hivyo chagua sarafu kwa uangalifu wakati wa uwekaji fedha; sarafu iliyochaguliwa haihitaji kulingana na sarafu ya akaunti ya kutrade. Viwango vya ubadilishanaji hutumika wakati wa transaction.
- Kagua taarifa ulizoweka, ikiwa ni pamoja na nambari za akaunti, ili kuepuka ucheleweshwaji kwa hatua zako za uwekaji fedha.
Exness haitozi ada ya uchakataji wa hatua za uwekaji fedha kamwe, lakini watoa huduma za malipo fulani hutoza; thibitisha ada za njia uliyochagua katika EB lako au kwenye tovuti ya mtoa huduma za malipo huyo.
Ada za usindikaji
Kwa kawaida Exness haitozi ada za uchakataji kwenye pesa zilizowekwa, lakini baadhi ya watoa huduma za malipo huenda wakatoza. Thibitisha ada zinazoweza kutozwa kwa njia uliyochagua ya malipo kwenye Eneo la kibinafsi, au kwenye tovuti ya mtoa huduma huyo wa malipo kila wakati.
Muda wa uchakataji
Muda wa uchakataji hutofautiana kulingana na njia ya malipo, kama inavyoonekana kwenye EB. Muda wa uchakataji huonyesha muda wa wastani hadi wa juu zaidi wa uchakataji na, ingawa muda wa wastani kwa kawaida ndio muda unaotarajia, hatua za uwekaji fedha zinaweza kuchukua hadi muda wa juu zaidi ulioonyeshwa.
Njia nyingi za malipo zinazotolewa huonyesha uchakataji wa papo hapo, kumaanisha kuwa transaction hiyo hufanywa ndani ya sekunde chache bila uchakataji wa wataalamu wetu wa idara ya kifedha (sio kwamba uchakataji wa transation hiyo hukamilika papo hapo).
Ikiwa unahitaji usaidizi katika transaction yako, nenda kwenye Historia yako ya transaction, chagua transaction ambayo unahitaji usaidizi, na ubofye Pata usaidizi ili kutuma ombi la usaidizi.
Utoaji fedha
Muhtasari
Kuna sera ambazo ni muhimu kukumbuka wakati unatoa pesa kwenye akaunti za kutrade. Baadhi ya njia za utoaji fedha hazipatikani kwa akaunti za Exness ambazo hazijathibitishwa, kwa hivyo inashauriwa kuwa uthibitishe akaunti yako ya Exness haraka iwezekanavyo.
Maudhui yanayohusiana:
- Je, ninawezaje kufanya transaction kwa kutumia akaunti yangu ya kutrade?
- Je, ninawezaje kuthibitisha akaunti yangu ya Exness?
Njia iliyotumiwa kuweka funds inajitajika kwa kuzitoa, kwani sharti njia sawa itumike kwa hatua zote mbili katika hali nyingi. Ikiwa njia iliyotumiwa kwa uwekaji fedha haipatikani kwa utoaji fedha, njia mbadala zinaweza kutumiwa ikiwa zinaweza kutumika (zinapatikana katika EB na eneo lako). Njia iliyotumiwa sharti iwe imesajiliwa chini ya jina sawa la kisheria na lililosajiliwa kwenye akaunti ya Exness, na inaweza kuhitaji uthibitishaji wa akaunti ya malipo inapotumika kwa mara ya kwanza.
Wasiliana na Usaidizi ukiwa na Kitambulisho chako cha transaction katika hali kama hizo.
Kipaumbele cha njia ya malipo ndiyo sera muhimu zaidi ya utoaji fedha ya kukumbuka, na inategemea njia za uwekaji fedha zilizotumiwa. Kadi za benki zinaweza kutumika kwa aina mbili za utoaji fedha: maombi ya refund na utoaji wa faida. Maombi ya refund ni utoaji wa pesa zilizowekwa, kwa uwiano na njia zilizotumiwa kuziweka (mifano imeonyeshwa hapa chini), na sharti yakamilishwe kwanza; maombi ya refund kwa sehemu fulani yanapatikana. Masharti ya ombi la refund yanaonyeshwa juu ya Kichupo cha utoaji fedha cha EB lako, ikiwa inatumika. Utoaji wa faida hufanywa baada ya maombi yote yanayohitajika ya refund, na ni uwiano wa utoaji wa faida iliyopatikana kutokana na biashara (mifano imeonyeshwa hapa chini). Tunapendekeza sana kusoma kuhusu kipaumbele cha njia ya malipo kilichoelezwa hapa chini.
Maudhui yanayohusiana:
- Je, ninawezaje kuweka na kutoa pesa kwa kutumia kadi za benki?
- Je, maombi ya refund ya sehemu fulani hufanya kazi vipi?
Kila njia ya utoaji fedha ina masharti ya kipekee, kama vile vikomo vya chini/juu zaidi, muda wa uchakataji, na masharti ya uthibitishaji wa akaunti. Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB) kila wakati ili kuthibitisha taarifa na upatikanaji wa njia za malipo, kwa kuwa zinaweza kuwa nje ya mtandao kwa ajili ya matengenezo. Endelea kusoma kwa sheria za jumla, au ufuate viungo vyovyote hapa chini kwa maelezo zaidi.
Kanuni za kawaida
- Kipaumbele cha njia ya malipo (maelezo ya kina yako hapa chini) sharti kifuatwe ili kuhakikisha transactions za haraka.
- Kabla faida iweze kutolewa kutoka kwa akaunti ya kutrade, ombi la refund kwa kiasi kamili cha pesa kilichowekwa kwa kutumia kadi ya benki sharti likamilishwe. Maombi ya refund kwa sehemu fulani yanapatikana kwa baadhi ya akaunti za Exness.
- Kiasi cha juu zaidi cha pesa kinachoweza kutolewa kwa wakati wowote ni sawa na free margin ya akaunti yako ya kutrade.
- Utoaji fedha kwa kawaida huhitaji njia, akaunti ya malipo na sarafu sawa na iliyotumika kwa uwekaji fedha. Ikiwa njia nyingi za malipo zinatumiwa kwa uwekaji fedha, kunapaswa kuwa na uwiano kwa utoaji fedha katika njia hizi.
- Njia mbadala zinaweza kupatikana kwa traders waliotimiza masharti; katika hali za kipekee, tunaweza kuondoa kanuni ya kawaida ya uwiano wa utoaji fedha kulingana na kufanikiwa kwa uthibitishaji wa akaunti na kuidhinishwa na wataalamu wetu wa malipo.
- Uthibitishaji wa akaunti ya malipo unahitajika unapotumia mfumo wa malipo kwa utoaji fedha ambao haujatumiwa hapo awali; unatarajiwa kuwasiliana na Usaidizi ukiwa na uthibitisho wa umiliki wa akaunti katika hali kama hizo.
- Ikiwa hauwezi kutumia option rahisi ya malipo, basi inaweza kumaanisha kuwa akaunti yako bado haijatimiza masharti ya kutumia njia hiyo. Options rahisi hutegemea mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na historia ya akaunti na udhibiti wa hatari.
- Gundua options zako za utoaji fedha katika EB lako; options hizi zinatokana na eneo lako lililosajiliwa na hali ya uthibitishaji wa akaunti.
Exness haitozi ada ya uchakataji wa hatua za utoaji fedha kamwe, lakini watoa huduma za malipo fulani hutoza; thibitisha ada za njia uliyochagua katika EB lako au kwenye tovuti ya mtoa huduma za malipo huyo.
Kipaumbele cha njia ya malipo
Kipaumbele cha mfumo wa malipo huhakikisha kuwa hatua za utoaji fedha ni za haraka na kwa wakati huo huo zinazingatia kanuni za kifedha za kieneo. Utoaji fedha kwa kutumia njia za malipo zilizoorodheshwa sharti ufanyike kwa utaratibu, kulingana na kipaumbele hiki:
- Maombi ya refunds ya kadi ya benki
- Utoaji wa faida (hutolewa kwa uwiano kwa njia zote za uwekaji fedha zilizotumika).
Kipaumbele cha mfumo wa malipo hutumika kwenye akaunti yako ya Exness, sio kwa akaunti binafsi za kutrade.
Mfano wa kipaumbele cha njia ya malipo
Umeweka jumla ya USD 1 000 kwenye akaunti yako ya kutrade: USD 700 kwa kutumia kadi ya benki na USD 300 kwa kutumia Neteller.
Umepata USD 500, na ungependa kuzitoa zote, ikiwa ni pamoja na faida:
- Akaunti yako ya kutrade ina free margin ya USD 1 500 (jumla ya pesa ulizoweka awali na faida).
- Maombi ya refund sharti yafanywe kwanza, kwa kufuata kipaumbele cha mfumo wa malipo, yaani kufanya refund ya USD 700 kwa kadi yako ya benki kwanza.
- Baada ya maombi yote ya refund kwa kutumia kadi ya benki kuchakatwa, toa faida kwa uwiano na ulivyoweka pesa, yaani, toaUSD 250kwa kutumia kadi yako ya benki kwanza, kisha USD 150 kwa kutumia akaunti yako ya Neteller.
Mfumo wa kipaumbele cha malipo huhakikisha kuwa Exness inafuata kanuni za kifedha na kuzuia utakatishaji wa fedha haramu na ulaghai unaoweza kutokea, na kuifanya kuwa kanuni muhimu bila ubaguzi.
Muda wa uchakataji
Muda wa uchakataji hutofautiana kulingana na njia ya malipo, kama inavyoonekana kwenye EB. Muda wa uchakataji huonyesha muda wa wastani hadi wa juu zaidi wa uchakataji na, ingawa muda wa wastani kwa kawaida ndio muda unaotarajia, hatua za utoaji fedha zinaweza kuchukua hadi muda wa juu zaidi ulioonyeshwa.
Njia nyingi za malipo zinazotolewa huonyesha uchakataji wa papo hapo, kumaanisha kuwa transaction hiyo hufanywa ndani ya sekunde chache bila uchakataji wa wataalamu wetu wa idara ya kifedha (sio kwamba uchakataji wa transation hiyo hukamilika papo hapo).
Ikiwa unahitaji usaidizi katika transaction yako, nenda kwenye Historia yako ya transaction, chagua transaction ambayo unahitaji usaidizi, na ubofye Pata usaidizi ili kutuma ombi la usaidizi.