Akaunti za Exness zina vipengele vya usalama vinavyosaidia kuthibitisha mmiliki wa akaunti na kupunguza hatari ya matumizi yasiyoidhinishwa ya akaunti. Inapendekezwa pia usome kuhusu kujikinga kutokana na shughuli za ulaghai. Zaidi ya hayo, tunatoa Vipengele kadhaa vya usalama vya Exness. Hapa kuna baadhi ya hatua zinazohitaji uthibitishaji wa akaunti:
-
-
-
- Kubadilisha nenosiri lako la Eneo la Binafsi
- Kurejesha nenosiri la Eneo lako la Binafsi
- Kubadilisha aina yako ya usalama
- Kubadilisha mshirika
- Kutoa pesa
- Kubadilisha nenosiri la biashara
- Kuweka na kubadilisha nenosiri la ufikiaji wa kusoma pekee
-
-
Aina ya usalama
Aina ya usalama ya akaunti inarejelea njia iliyochaguliwa ya kuthibitisha mmiliki wa akaunti kwa kuthibitisha umiliki wa akaunti uliotumwa kwake na aina yake ya usalama iliyochaguliwa ya Eneo la Binafsi (EB). Aina ya usalama inaweza kubadilishwa katika hali fulani.
Anwani ya barua pepe | Misimbo ya uthibitishaji hutumwa kwenye anwani yako ya barua pepe iliyosajiliwa. Weka msimbo huo unapoombwa ili kuthibitisha ombi lako. Kubadilisha aina ya usalama kutoka kwa simu hadi barua pepe kunawezekana tu ndani ya siku 30 za usajili. |
Nambari ya simu | Misimbo ya uthibitishaji hutumwa kwenye namba yako ya simu iliyosajiliwa. Weka msimbo au OTP* ya sauti ili kuthibitisha ombi lako. Ni nambari moja ya simu pekee inayoweza kutumika kwa wakati mmoja; nambari iliyotumiwa kusajili huwekwa kwa chaguomsingi lakini inaweza kubadilishwa katika mipangilio ya aina yako ya usalama. |
Programu ya uthibitishaji | Programu ya Uthibitishaji ni hatua muhimu katika uthibitishaji wa mteja. Tofauti na aina zingine za usalama, msimbo unaotolewa na programu ya uthibitishaji hutumiwa kwa uthibitishaji badala ya OTP inayotumwa kwa barua pepe au simu. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia programu ya uthibitishaji kwa akaunti yako ya Exness. |
Arifa za programu | Arifa za programu hukuruhusu kufanya hatua zinazohitaji kiwango cha juu cha usalama kwa haraka. Hatua inapofanywa, kwa mfano, ombi la utoaji pesa, arifa ya programu hutumwa kupitia programu ya Exness Trade. Bofya Thibitisha/Kataa ili kuthibitisha ombi hilo. |
Tumejumuisha orodha ya programu na maduka ambapo programu ya uthibitishaji inaweza kupakuliwa (inaweza kutofautiana kulingana na eneo):
Kwenye iOS | Kwenye Android |
Kumbuka: Kuweka msimbo usio sahihi wa uthibitishaji mara nyingi kutasababisha akaunti hiyo kuzuiwa. Unahitaji kusubiri saa 24 ili ujaribu hatua hiyo tena. Kufuta faili zako za akiba na vidakuzi kunaweza kukuruhusu kujaribu tena mapema, lakini hakuna uhakikisho kuwa hii itafanya kazi.
Jinsi ya kubadilisha aina yako ya usalama
Ili kubadilisha aina yako ya usalama, ingia kwenye Eneo la Binafsi (EB) na ufuate hatua zilizo hapa chini kulingana na mabadiliko ambayo ungependa ya aina ya usalama. Wasiliana na Usaidizi ikiwa unahitaji usaidizi.
Ili kubadilisha aina ya usalama kuwa programu ya Uthibitishaji:
- Chagua Mipangilio kwenye menyu kuu, ubofye Mipangilio ya Usalama, sogeza chini hadi uthibitishaji wa Hatua Mbili, kisha bofya Badilisha.
- Bofya kwenye Programu ya uthibitishaji na ubofye Inayofuata.
- Changanua msimbo wa QR ukitumia programu yako ya uthibitishaji.
- Weka msimbo wa herufi 6 unaotolewa na programu ya uthibitishaji, kisha ubofye Thibitisha.
- Mchakato wako wa uthibitishaji wa hatua 2 sasa umekamilika.
Utatumia msimbo wenye herufi 6 kwenye programu yako ya uthibitishaji wakati wowote uthibitishaji wa akaunti unahitajika badala ya kutumiwa na Exness.
Ili ubadilishe kutoka barua pepe hadi simu:
- Chagua Mipangilio kwenye menyu kuu, bofya Mipangilio ya Usalama na usogeze chini hadi uthibitishaji wa Hatua Mbili kisha ubofye Badilisha.
- Bofya Badilisha kwenye option ya Aina ya usalama.
- Chagua nambari ya simu iliyosajiliwa kutoka kwenye orodha, au ubofye +Nambari mpya ya simu.
- Thibitisha hatua hii kwa msimbo wa uthibitishaji uliotumwa kwa nambari yako ya simu.
Ili kubadilisha kutoka simu hadi barua pepe:
- Bofya kwenye Mipangilio ya Usalama na usogeze chini hadi Uthibitishaji wa Hatua Mbili kisha ubofye Badilisha.
- Bofya Badilisha kwenye option ya Aina ya usalama na uiweke kama Barua pepe.
Kumbuka: Hii inawezekana tu ndani ya siku 30 za usajili.
Ili kubadilisha kutoka nambari moja ya simu hadi nyingine:
- Bofya kwenye Mipangilio ya Usalama na usogeze chini hadi Uthibitishaji wa Hatua Mbili kisha ubofye Badilisha.
- Chagua nambari ya simu iliyosajiliwa kutoka kwenye orodha, au ubofye +Nambari mpya ya simu.
- Thibitisha hatua hii kwa msimbo wa uthibitishaji uliotumwa kwa nambari hii ya simu.
Ili kubadilisha kutoka nambari ya simu au barua pepe hadi Arifa ya programu:
- Bofya kwenye Mipangilio ya Usalama na usogeze chini hadi Uthibitishaji wa Hatua Mbili kisha ubofye Badilisha.
- Bofya Badilisha kwenye option ya Aina ya usalama.
- Chagua Arifa za programu.
- Ukibadilisha aina yako ya usalama, utapokea arifa kwenye EB lako inayoonyesha misimbo ya QR.
- Ikiwa huna programu ya Exness Trade iliyosakinishwa au inahitaji kusasishwa, changanua msimbo wa kwanza wa QR ukitumia kifaa chako cha mkononi ili usasishe au uipakue kutoka PlayStore au AppleStore.
- Baada ya programu hiyo kusakinishwa au kusasishwa, ingia kwa kutumia programu na uchanganue msimbo wa pili wa QR ili kuwasha arifa za programu. Bofya Ruhusu arifa.
- Weka msimbo wa uthibitishaji wenye herufi 6 uliotumwa kwa aina yako ya sasa ya usalama ili kuthibitisha kubadili kwako hadi Arifa za programu.
- Ukurasa huo utaonyesha kuwa umebadilisha hadi Arifa za programu. Bofya Nimeelewa ili kukamilisha mchakato huo.
Kwa transactions zinazohitaji msimbo wa uthibitishaji, Arifa ya programu itatumwa kwa programu yako ya Exness Trade ili kuthibitisha transaction hiyo.
Hakikisha kuwa programu yako ya Exness Trade imesasishwa hadi toleo jipya zaidi ili kuwezesha arifa za programu ndani ya programu. Sharti pia uruhusu arifa za programu kwa programu hiyo kwenye mipangilio ya kifaa chako cha mkononi.
Ukipoteza ufikiaji wa nambari yako ya simu, tunapendekeza ufuate hatua kwenye makala yetu kuhusu kudhibiti taarifa za akaunti au kuwasiliana na Usaidizi kwa usaidizi.
Kuangalia aina yako ya usalama
- Ingia kwenye Eneo la Binafsi.
- Chagua Mipangiliokwenye menyu kuu.
- Fungua kichupo cha mipangilio ya Usalama.
- Aina ya usalama huonyeshwa hapa.
PIN ya usaidizi
PIN ya usaidizi ni muunganisho wa kipekee wa herufi na nambari unaotumiwa kuthibitisha mmiliki wa akaunti anayewasiliana na Usaidizi. Ni kiwango cha juu zaidi cha usalama kwa akaunti ya Exness, kwa kuwa ni mmiliki wa akaunti pekee anayeweza kuifikia. Usaidizi unahitajika kutuma na kupokea taarifa nyeti na kufanya PIN ya usaidizi kuwa muhimu ili kupata data ya faragha ya mmiliki wa akaunti.
Muhimu: PIN ya usaidizi haipaswi kukanganywa na msimbo wa uthibitishaji wa aina ya usalama ya akaunti na/au nenosiri la akaunti ya kutrade.
PIN ya usaidizi ya akaunti hutolewa baada ya ombi kutumwa. Hutumika kama njia ya kukuthibitisha kama mmiliki aliyeidhinishwa wa akaunti. PIN ya usaidizi, ikishatolewa, ni halali kwa saa 24 pekee.
Ikiwa aina yako ya usalama imewekwa kuwa Barua pepe au programu ya uthibitishaji, PIN ya usaidizi itatumwa kwa nambari ya simu inayotumika iliyosajiliwa kwenye akaunti; ikiwa aina ya usalama ni Simu - PIN itatumwa kwa nambari ya simu ya sasa ambayo inatumika kama aina ya usalama.
Manenosiri
Aina kadhaa tofauti za manenosiri hulinda akaunti ya Exness. Kuelewa manenosiri haya mbalimbali kunaweza kusaidia kuepuka mkanganyiko wakati nenosiri linahitajika.
Aina za manenosiri
Manenosiri yanayohitajika ili kulinda akaunti yako ya Exness ni pamoja na:
Nenosiri la Eneo la Binafsi (EB) | Linalotumika kuingia kwenye EB lako; nenosiri kuu la akaunti yako ya Exness. |
Nenosiri la biashara | Kila akaunti ya kutrade ina nenosiri lake, linalotumiwa unapoingia kwenye jukwaa la biashara kwa kutumia akaunti hiyo ya kutrade. |
Nenosiri la ufikiaji wa kusoma pekee (hapo awali ulijulikana kama nenosiri la mwekezaji) |
Sawa na nenosiri la biashara, nenosiri hili pia huwekwa kwa kila akaunti ya kutrade. Trade zote huzuiwa wakati umeingia kwenye akaunti ya kutrade kwa kutumia nenosiri la ufikiaji wa kusoma pekee. Nenosiri la ufikiaji wa kusoma pekee na nenosiri la biashara haziwezi kufanana. |
PIN ya usaidizi | Hili sio nenosiri, lakini ni muhimu kukumbuka matumizi yake. PIN ya Usaidizi hutumika kuthibitisha akaunti unapowasiliana na Usaidizi. |
Ili kurejesha nenosiri, soma maagizo kwenye jinsi ya kurejesha nenosiri lililopotea.
Mahitaji ya nenosiri
Kila nenosiri sharti lijumuishe:
- Herufi 8 hadi 15
- Herufi kubwa na ndogo
- Mchanganyiko wa nambari, herufi za Kiingereza na herufi maalum
Kwa mfano:
eH#z4@H9!
Nenosiri thabiti linapendekezwa sana ili kulinda akaunti yako ya Exness; usishiriki nenosiri hili na mtu yeyote kamwe. Usaidizi hautakuomba kamwe uwasilishe nenosiri lolote isipokuwa PIN ya Usaidizi inayotumiwa kuthibitisha umiliki wa akaunti pekee.
Kumbuka: Manenosiri yaliyowekwa hayatumwi kwa barua pepe yako kwa sababu za usalama. Ikiwa umesahau au umepoteza nenosiri, fuata hatua zilizoonyeshwa za kurejesha nenosiri hapo juu.