Tumekusanya orodha ya mada za kawaida za utatuzi wa hitilafu kwa watumiaji wa VPS ya Exness. Tafadhali fuata kiungo kwa maelezo zaidi kuhusu VPS ya Exness ni nini, au bofya kichupo chochote hapa chini kwa mada hiyo ya utatuzi wa hitilafu:
- Siwezi kuingia
- Kusakinisha VPS upya
- Nimesahau nenosiri
- Kasi ya VPS iko chini
- VPS iliyokwama
- Hitilafu ya jukwaa la biashara
- Lugha ya VPS
- Eneo la seva
- Muda wa kusubiri
- Sasisho la toleo la awali la MT
- Advisors za FXBlue
Siwezi kuingia kwenye VPS yangu
Ikiwa huwezi kuingia kwenye VPS yako ya Exness kwa kutumia maelezo yako ya kuingia, jaribu hatua zifuatazo:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio > Seva Pepe ya Kibinafsi ili kuthibitisha kuwa una VPS ya Exness inayotumika.
- Thibitisha kuwa umeweka maelezo yako ya kuingia kwa usahihi. Usiweke nafasi yoyote, angalia anwani ya IP, na uingie kwenye Eneo lako la Binafsi. Nenosiri hutumwa mara moja pekee, kwa hivyo ukilisahau, sharti liwekwe upya (tazama kichupo cha Nenosiri lililosahaulika).
- Weka nenosiri lako upya kwenye Eneo la Binafsi
a. Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio > Seva Pepe ya Kibinafsi.
b. Bofya aikoni ya nukta 3 (kona ya juu kulia) kando ya Washa upya.
c. Bofya Weka Nenosiri Upya.
d. Tafadhali subiri hali inapoonyesha "Inawasha upya".
e. Bofya Ingia kisha Bofya ili kutazama kando ya sehemu ya Nenosiri ya VPS.
- Ikiwa hauwezi kuweka upya nenosiri, jaribu tena baada ya saa moja; majaribio mengi yasiyo sahihi yanaweza kuzuia majaribio zaidi ya kuingia kwa saa moja.
Ikiwa nenosiri halitabadilika, tafadhali wasiliana na Usaidizi.
Kusakinisha VPS upya
Fuata hatua hizi ikiwa utahitaji kusakinisha VPS ya Exness upya:
Hakikisha kuwa umehifadhi nakala za data, ikiwa ni pamoja na scripts na Expert Advisors, kabla ya kuanza.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Fungua Mipangilio na uchague option ya Seva Pepe ya Kibinafsi.
- Bofya aikoni ya nukta 3 (kona ya juu kulia) kando ya kitufe cha Washa upya.
- Chagua lugha unayopendelea na idadi ya terminali ambazo ungependa kusakinisha.
- Chagua Sakinisha VPS upya (data yote itaondolewa; inapendekezwa uhifadhi nakala yake kwanza).
Hatua ya kusakinisha upya huchukua takriban dakika 15-20 kukamilika; rudi kwenye EB lako baada ya muda huu ili kuthibitisha usakinishaji upya huu na kupata Nenosiri la VPS yako ya Exness. Tafadhali wasiliana na Usaidizi ikiwa usakinishaji upya wa VPS ya Exness hautafanikiwa.
Nilisahau nenosiri langu la VPS
Jaribu mojawapo ya options hizi mbili ikiwa umesahau nenosiri lako la VPS ya Exness:
Option ya kwanza
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio > Seva Pepe ya Kibinafsi.
- Bofya aikoni ya nukta 3 (kona ya juu kulia) kando ya Washa upya.
- Bofya Weka Nenosiri Upya.
- Tafadhali subiri hali inapoonyesha "Inawasha upya".
- Bofya Ingia kisha Bofya ili kutazama kando na sehemu ya Nenosiri ya VPS.
Option ya pili
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio > Seva Pepe ya Kibinafsi.
- Bofya Ingia.
- Bofya Weka Nenosiri Upya.
- Tafadhali subiri hali inapoonyesha "Inawasha upya".
- Bofya Ingia kisha Bofya ili kutazama kando ya sehemu ya Nenosiri ya VPS.
Manenosiri yanaweza kutazamwa mara moja pekee, kwa hivyo tafadhali hifadhi nenosiri lako mahali salama.
Ikiwa nenosiri halitabadilika, tafadhali wasiliana na Usaidizi.
Kasi ya VPS yangu iko chini
Wakati kasi ya VPS iko chini kuna mambo kadhaa unaweza jaribu ili kuionyesha upya:
Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio> Seva Pepe ya Kibinafsi na ubofye Washa upya.
Futa nafasi kwenye VPS kwa kuenda kwenye sehemu ya programu ya MT4/5, fungua Folda ya Data > Tester kisha uondoe/ufute faili zote kwenye folda za Logs na History.
Ikiwa kasi ya VPS yako bado iko chini
Kwanza hifadhi nakala ya data yako, ikiwa ni pamoja na scripts na Expert Advisors kisha:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio > Seva Pepe ya Kibinafsi..
- Bofya aikoni ya nukta 3 (kona ya juu kulia) kando ya Washa upya.
- Chagua Sakinisha upya VPS ambayo itarejesha VPS yako ya Exness kwa mipangilio ya chaguo-msingi (data yote itaondolewa; ndiyo sababu inapendekezwa uihifadhi nakala).
- Weka maelezo ya VPS yako kabla ya kubofya Sakinisha upya VPS.
Ikiwa hatua hizi hazijatatua hitilafu hiyo, tafadhali wasiliana na Usaidizi.
VPS yangu inakwama
VPS yako ikiacha kufanya kazi au ikikwama, jaribu:
Toka kwenye VPS, kisha uingie tena.
Ingia kwenye Eneo la Binafsi na ufungue Mipangilio > Seva Pepe ya Kibinafsi, kisha uchague Washa upya.
Ikiwa VPS bado inakwama
Kwanza hifadhi nakala ya data yako, ikiwa ni pamoja na scripts na Expert Advisors kisha:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio > Seva Pepe ya Kibinafsi..
- Bofya aikoni ya nukta 3 (kona ya juu kulia) kando ya Washa upya.
- Chagua Sakinisha upya VPS ambayo itarejesha VPS yako ya Exness kwa mipangilio ya chaguo-msingi (data yote itaondolewa; ndiyo sababu inapendekezwa uihifadhi nakala).
- Weka maelezo ya VPS yako kabla ya kubofya Sakinisha upya VPS.
Ikiwa hatua hizi hazijatatua hitilafu hiyo, tafadhali wasiliana na Usaidizi.
Sina idadi sahihi ya majukwaa ya biashara yaliyosakinishwa
Ikiwa huoni kiasi sahihi cha programu za MT4/MT5 kwenye VPS yako, fuata hatua hizi:
Kwanza hifadhi nakala ya data yako, ikiwa ni pamoja na scripts na Expert Advisors kisha:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio > Seva Pepe ya Kibinafsi..
- Bofya aikoni ya nukta 3 (kona ya juu kulia) kando ya Washa upya.
- Chagua Sakinisha upya VPS ambayo itarejesha VPS yako ya Exness kwa mipangilio ya chaguo-msingi (data yote itaondolewa; ndiyo sababu inapendekezwa uihifadhi nakala).
- Weka kiasi ambacho ungependa cha majukwaa ya biashara ya MetaTrader, kisha ubofye Sakinisha upya VPS.
Ikiwa hatua hizi hazijatatua hitilafu hiyo, tafadhali wasiliana na Usaidizi.
Ningependa kubadilisha lugha ya VPS yangu
Ili kubadilisha lugha inayotumiwa na VPS yako, fuata hatua hizi:
Kwanza hifadhi nakala ya data yako, ikiwa ni pamoja na scripts na Expert Advisors kisha:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio > Seva Pepe ya Kibinafsi..
- Bofya aikoni ya nukta 3 (kona ya juu kulia) kando ya Washa upya.
- Chagua Sakinisha upya VPS ambayo itarejesha VPS yako ya Exness kwa mipangilio ya chaguo-msingi (data yote itaondolewa; ndiyo sababu inapendekezwa uihifadhi nakala).
- Chagua lugha yako mpya kutoka kwa menyu kunjuzi; utahitaji pia kuweka idadi ya majukwaa ya MetaTrader. Bofya Sakinisha upya VPS ukishamaliza.
Ikiwa hatua hizi hazijatatua hitilafu hiyo, tafadhali wasiliana na Usaidizi.
Ningependa kubadilisha eneo la seva yangu ya VPS
Njia pekee ya kubadilisha eneo la seva ya VPS ni kufuta huduma ya VPS ya Exness na kuisakinisha tena, ukibainisha eneo la seva wakati wa usakinishaji. Data zote, ikiwa ni pamoja na EA na scripts, zitapotea wakati wa kufutwa na sharti utimize masharti ya VPS ya Exness ili kuisakinisha tena.
Ili kufuta VPS ya Exness:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi na ufungue Mipangilio kisha Seva Pepe ya Kibinafsi.
- Bofya aikoni ya nukta 3 (kona ya juu kulia) kando ya Washa Upya.
- Chagua Futa kisha Ndiyo, futa seva.
- Fungua kichupo cha Seva Pepe ya Kibinafsi kwenye Mipangilio na utume ombi la VPS ya Exness upya.
- Chagua akaunti yako ya msingi ya kutrade ya VPS kwanza, kisha Exness itapendekeza eneo la karibu la seva ya VPS kwa akaunti yako ya MT iliyochaguliwa. Sasa unaweza kubadilisha eneo la VPS katika point hii.
Sasa eneo la seva yako ya VPS ya Exness litakuwa limebadilika. Ikiwa hatua hizi hazikusaidia, tafadhali wasiliana na Usaidizi.
Je, ninawezaje kuangalia viwango vyangu vya muda wa kusubiri?
Ikiwa unahisi kuwa huenda una matatizo ya muunganisho, inaweza kuwa muhimu kuangalia kasi ya muunganisho (muda wa kusubiri) ya VPS ya Exness kwa seva za biashara.
Ili uone viwango vyako vya sasa vya muda wa kusubiri:
- Fuata hatua ili ujiunganishe kwenye VPS ya Exness.
- Kwenye kompyuta pepe ya mezani ya VPS ya Exness, fungua jukwaa ulilochagua la MetaTrader.
- Ingia kwenye akaunti ukitumia akaunti yako ya kutrade kwa kubofya kulia kwenye Akaunti katika dirisha la Kivinjari na uchague Ingia kwenye Akaunti ya Kutrade.
- Bofya upau wa hali ya muunganisho (upande wa chini kulia mwa dirisha la Terminali kwenye MT4 au dirisha la Kisanduku cha zana kwenye MT5) ili uonyeshe orodha ya seva za biashara zinazoweza kuunganishwa na muda wao wa kusubiri (katika ms).
- Seva unayochaguliwa huchaguliwa kiotomatiki kulingana na ms za chini zaidi zinazopatikana, lakini unaweza kuchagua seva tofauti ili uangalie ikiwa seva hiyo inaboresha muunganisho wako kwa ujumla.
- Bofya Changanua seva upya ili uonyeshe upya data hii na labda utambue muda wa juu wa kusubiri usio wa kawaida (katika ms).
- Kubofya Ingia kwenye akaunti kutakuruhusu kuingia ukitumia akaunti ya kutrade (njia mbadala ya hatua ya 3).
Je, muda wa kusubiri ni nini?
Muda wa kusubiri ni kasi ambayo taarifa husafiri kutoka kwenye kifaa chako hadi seva ya biashara. Hupimwa kwa ms (milisekunde), kiasi halisi cha muda kati ya wakati amri imewekwa na wakati seva inapokea amri hiyo. Kadri muda wa kusubiri ulivyo chini, ndivo munganisho ulivyo bora zaidi. Kadri muda wa kusubiri ulivyo juu, ndivyo inavyochukua muda mrefu kuwasiliana kati ya kifaa na seva.
Ikiwa VPS ya Exness bado ina kasi ya chini kwenye kifaa chako, jaribu kufuata hatua zetu za kutatua hitilafu ya VPS ya Exness yenye kasi ya chini au wasiliana na Usaidizi ili upate usaidizi zaidi.
Sasisho la toleo la awali la MT
Baadhi ya hitilafu zisizotarajiwa zinaweza kutatuliwa kwa kuhakikisha kuwa matoleo ya MetaTrader katika VPS yako ya Exness yako yamesasishwa hadi toleo jipya zaidi.
Kumbuka: Expert Advisors (EA) haziondolewi kwenye mchakato wa usasishaji lakini zingine zinaweza hitaji kusakinishwa upya ili kuendana na toleo hilo jipya. Orders zilizofunguliwa husalia zikiwa zimefunguliwa wakati wa usasishaji.
Je, ninawezaje kuangalia toleo langu la sasa la MetaTrader?
- Fungua MetaTrader 4 au 5 kwenye VPS ya Exness.
- Fungua Usaidizi katika upau wa menyu kuu.
- Chagua Kuhusu.
- Dirisha ibukizi litaonyesha toleo/muundo wa sasa wa MetaTrader chini ya "MetaTrader 4 EXNESS" au "MetaTrader 5 EXNESS" mtawalia.
Je, ninawezaje kusasisha MetaTrader?
- Funga kila onyesho lililofunguliwa la MetaTrader 4 na 5.
- Tafuta programu ya MT Updater kwenye eneo-kazi la VPS ya Exness.
- Fungua MT Updater.
- Subiri programu hiyo ipakue na kusakinisha kiotomatiki toleo la hivi karibuni la MetaTrader. Mchakato huu unaweza kuchukua dakika chache.
- Uthibitishaji utatokea mara tu sasisho litakapokamilika; bofya Sawa ili kukamilisha sasisho.
Je, nenosiri langu la msimamizi ni lipi?
Unaweza ombwa uweke nenosiri la msimamizi baada ya kutumia Programu ya MetaTrader iliyosasishwa. Tafadhali chagua HAPANA kwenye dirisha ibukizi, kwa kuwa hii sio muhimu na MetaTrader itafanya kazi kawaida baada ya kufunga dirisha hili.
Hitilafu za usasishaji?
Ikiwa utakumbana na hitilafu yoyote wakati wa mchakato wa usasishaji, funga dirisha la uthibitishaji dirisha ibukizi na uanzisha upya VPS ya Exness na uendeshe programu hiyo ua usasishaji tena. Ikiwa sasisho bado halifaulu tafadhali wasiliana na Usaidizi ili waweze kusaidia.
Je, ninawezaje kusakinisha Expert Advisors za FX Blue?
Tafadhali fuata kiungo cha makala yetu yanayotoa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwezesha Expert Advisors za FX Blue katika VPS ya Exness.