Ikiwa ungependa kutumia huduma ya VPS ya Exness bila malipo ili kuboresha uzoefu wako wa biashara, lakini hujui ni wapi pa kuanzia? Makala haya yatakuongoza katika hatua zote muhimu kuanzia mwanzo hadi mwisho:
- Je, ninapaswa kujua nini kabla ya kuanza?
- Je, ninawezaje kutimiza masharti?
- Je, ninaweza kutuma ombi wapi?
- Je, ninawezaje kuendelea kufikia VPS ya Exness?
- Je, ninawezaje kuunganishwa kwenye VPS ya Exness?
- Je, ninaweza kuweka nenosiri jipya?
- Je, ninawezaje kuweka mipangilio ya Expert Advisors (EA) katika VPS ya Exness?
- Je, ninawezaje kutatua hitilafu za VPS ya Exness?
Je, ninapaswa kujua nini kabla ya kuanza?
VPS ya Exness inatolewa bila malipo, lakini watumiaji wanatakiwa kufikia kiasi fulani cha salio la akaunti na/au kiwango cha biashara kabla ya huduma hii iweze kutumika. Pia kuna masharti yanayoendelea ili kudumisha huduma hii unapotimiza masharti; unaweza kupoteza uwezo wa kufikia VPS ya Exness ikiwa masharti haya hayajafikiwa. Kuelewa Masharti ya matumizi ya VPS ya Exness kunapendekezwa wakati wa kutumia huduma hii.
Je, ninawezaje kutimiza masharti?
Tembelea Eneo lako la Binafsi (EB) ili uone salio la akaunti yako mahususi au salio la akaunti au vigezo vya kiwango cha biashara.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Fungua menyu ya Mipangilio.
- Chagua Seva Pepe ya Binafsi.
Kiasi halisi kinachohitajika kinaweza kutofautiana, kwa hivyo ni bora kuthibitisha kiasi hiki kwenye EB lako kila wakati.
- Salio la akaunti: kiasi cha funds kinachopatikana kilichowekwa kwenye akaunti yako ya kutrade.
- Kiwango cha biashara: kiasi cha funds kinachotumika kufungua na kufunga orders katika terminali ya biashara kwa kutumia akaunti ya kutrade, kinachofuatiliwa katika lots lakini hukokotolewa katika USD. Hii haijumuishi akaunti za kutrade za Usimamizi wa PortfolioauSocial Trading.
Tunapendekeza usome zaidi kuhusu kutuma ombi la VPS ya Exness ili upate maelezo ya kina.
Ili utimize masharti kwa kutumia salio la akaunti:
Weka funds kwenye akaunti ya kutrade kwa kiasi kilichoonyeshwa katika vigezo ikiwa inahitajika. Salio lililopo la akaunti ya kutrade linakubaliwa, kwa hivyo unaweza kupata kuwa tayari unatimiza masharti ya kupata VPS ya Exness bila kuhitaji kuweka pesa. Vigezo hivi vinapofikiwa, unaweza kutuma ombi la VPS ya Exness.
Ili utimize masharti kwa kutumia salio la akaunti na kiwango cha biashara:
Weka funds kwenye akaunti ya kutrade kwa kiasi kinachoonyeshwa katika vigezo, kisha trade (orders zilizofunguliwa na zilizofungwa) kwa thamani ya kiwango kinachohitajika cha biashara. Tembelea EB baada ya kutimiza vigezo hivi ili utume ombi la VPS ya Exness.
Fuata kiungo hiki ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi kiwango cha biashara kinavyokokotolewa kwenye VPS ya Exness.
Je, ninaweza kutuma ombi wapi?
Sehemu hiyo hiyo ya EB lako pia itakupa fursa ya kutuma ombi la VPS ya Exness:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Fungua menyu ya Mipangilio.
- Chagua Seva Pepe ya Binafsi.
Hapa utaona masharti ya vigezo kabla ya kuweza kutuma ombi.
- Bofya Tuma Ombi la VPS hosting ikiwa unatimiza masharti.
Sehemu hii ya Eneo lako la Binafsi sasa itabadilika, ikionyesha uteuzi mpya wa options za VPS ya Exness.
Je, ninawezaje kuendelea kufikia VPS ya Exness?
Ili kuhifadhi VPS, sharti ukamilishe vigezo hivi:
- Sharti ufikie kiwango cha biashara kilichobainishwa (au kiasi sawa katika sarafu au mali yoyote) kwa kipindi cha siku 30, kipindi cha siku 90 au kipindi cha siku 180. Ni kigezo kimoja pekee cha muda kinachohitajika kufikiwa ili kundelea kufikia VPS ya Exness. Vipindi vya muda hufunguka unapovifikia, yaani, kipindi cha siku 90 huanza kutumika baada ya siku 90.
- Sharti uingie na ufanye trade kwenye VPS kwa kutumia akaunti uliyofungua ndani ya siku 5 baada ya kufikia VPS. Ikiwa vigezo hivi havijafikiwa, utapokea maonyo kwenye siku ya 3 na siku ya 5 kabla ya VPS kusitishwa (Pending orders hazijumuishwi).
- Sharti uingie na ufanye trade kwenye VPS angalau mara moja kila baada ya siku 30 au VPS hiyo itasitishwa, bila kujali kama mteja huyo anatimiza vigezo vya siku 90 au 180. Ikiwa vigezo hivi havijafikiwa, utapokea maonyo siku ya 27 na siku ya 30 kabla ya VPS kusitishwa (Pending orders hazijumuishwi).
Ingia kwenye EB ili uthibitishe vigezo kamili vya kudumisha ufikiaji wa VPS ya Exness.
Je, ninawezaje kuunganishwa kwenye VPS ya Exness?
Hatua inayofuata ni kuunganisha kwenye huduma ya VPS ya Exness kupitia programu ya uunganisho wa mbali kwenye kifaa chako cha kielektroniki. Hii inawezekana kwenye Windows au Mac.
1. Pata maelezo yako ya kuingia kwenye VPS ya Exness
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Fungua menyu ya Mipangilio.
- Chagua Seva Pepe ya Binafsi.
- Thibitisha kuwa VPS ipo Mtandaoni (upande wa juu kushoto wa skrini), kisha ubofye Ingia kwenye akaunti.
- Dirisha ibukizi itaonekana:
-
- Anwani ya VPS
- Kuingia kwenye VPS
- Nenosiri la VPS
-
Nenosiri la VPS huonyeshwa mara moja; hakikisha kuwa unaliandika katika hatua hii au utahitaji kuweka upya nenosiri.
- Hatimaye, fuata hatua zilizo hapa chini kulingana na aina ya kifaa unachotumia.
2. Kuingia kwenye akaunti ukitumia maelezo yako ya kuingia
Kwa Windows
- Andika Remote Desktop Connection kwenye menyu ya Start kisha uanzishe programu hii.
- Weka Anwani ya VPS.
- Ikiwa unapanga kutumia Expert Advisors (EA), fuata hatua hizi za ziada kabla ya kuendelea:
-
- Bofya Onyesha Options kwenye dirisha la Remote Desktop Connection.
- Nenda kwenye kichupo cha Local Resources. Kwenye Local devices and resources, chagua More.
- Weka alama kwenye kisanduku kilicho karibu zaidi na maelezo ya faili ambapo EAs zako zinapatikana, kisha ubofye OK.
-
Kumbuka: Exness haiwezi kufikia faili zako za binafsi zinazotumiwa kwenye VPS kamwe.
- Sasa bofya Connect.
- Weka Maelezo ya Kuingia kwenye VPS na Nenosiri la VPS kisha uthibitishe maelezo hayo kwa kubofya OK.
Kwa Mac
- Pakua programu ya Microsoft Remote Desktop kwenye duka la programu.
- Anzisha programu hiyo na ubofye Add PC.
- Weka Anwani ya VPS kwenye sehemu ya PC Name.
- Chagua menyu kunjuzi ya User Account kisha uchague Add User Account.
- Weka Maelezo ya Kuingia kwenye VPS na Nenosiri la VPS kisha uthibitishe maelezo hayo kwa kubofya Add.
- Bofya Add ili ukamilishe mipangilio hii.
- Chagua na uanzishe Kompyuta hii ya mbali katika programu ya Microsoft Remote Deposit. Bofya Continue ikiwa ujumbe wa uthibitishaji utaonyeshwa.
Kumbuka: kuweka kitambulisho cha VPS ya Exness kimakosa mara kadhaa kutasitisha kwa muda anwani yako ya IP; subiri takriban saa moja kabla ya kujaribu tena.
Je, ninaweza kuweka nenosiri jipya?
Ndiyo, sharti ubadilishe nenosiri lako la chaguomsingi la VPS ya Exness na unaweza kuombwa ulibadilishe.
Ili ubadilishe nenosiri lako la VPS ya Exness:
- Ingia kwenye akaunti ukitumia maelezo yako ya kuingia kwenye VPS (kama inavyoonyeshwa hapo juu)
- Bofya menyu ya Start (aikoni ya Windows) na ubofye avata ya mtumiaji kisha uchague mipangilio ya Change account.
- Bofya Sign-in options kwenye menyu ya upande wa kushoto, kisha Change chini ya kichwa chaPassword.
- Weka nenosiri la sasa, kisha ubofye Next.
- Sasa weka nenosiri lako jipya mara mbili, na uweke kidokezo cha hiari ili kikusaidie kulikumbuka. Bofya Nextili uthibitishe nenosiri jipya.
- Nenosiri lako la VPS sasa limesanidiwa.
Je, ninawezaje kuweka mipangilio ya Expert Advisors (EA) katika VPS ya Exness?
VPS ya Exness huja ikiwa imesakinishwa awali pamoja na seti ya FX Blue Expert Advisors, ingawa unaweza kusakinisha EA yako binafsi kama inavyohitajika.
Kwenye EA yako mwenyewe
Kwanza unganisha kwenye VPS ya Exness kisha ufuate hatua hizi.
Kwenye MT4
- Fungua MetaTrader 4 kwenye VPS ya Exness.
- Bofya Faili kisha Fungua Folda ya Data.
- Fungua folda ya MQL4 na ubandike faili za wataalamu, scripts, na indicators kwenye folda zinazolingana (Expert Advisors, Script, Indicators).
- Anzisha upya MetaTrader 4.
- Katika dirisha la Usogezaji , panua folda inayofaa: Indicators, Expert Advisors au Scripts.
- Bofya na uburute EA kwenye chati ambayo ungependa ili uanze kuweka mipangilio ya EA (fuata maagizo ya skrini ili ukamilishe).
Kwenye MT5
- Fungua MetaTrader 5 kwenye VPS ya Exness.
- Bofya Faili kisha Fungua Folda ya Data.
- Fungua folda ya MQL5 na ubandike faili za experts, scripts na indicators kwenye folda zinazolingana (Expert Advisors, Scripts, Indicators)
- Anzisha upya MetaTrader 5.
- Katika dirisha la Usogezaji , panua folda inayofaa: Indicators, Expert Advisors au Scripts.
- Bofya na uburute EA kwenye chati ambayo ungependa ili uanze kuweka mipangilio ya EA (fuata maagizo ya skrini ili ukamilishe).
Ikiwa EA yako ni faili ya .exe, ihifadhi kwenye eneo-kazi lako la mbali na uwasiliane na Usaidizi ili upate usaidizi zaidi.
Kwenye EA ya FX Blue
Unganisha kwenye VPS ya Exness, kisha:
- Tafuta na utekeleze kisakinishi cha FX Blue kwenye eneo-kazi la VPS kwa jukwaa la biashara (MT4 au MT5) ukiwa umeingia kwenye VPS ya Exness.
Fungua jukwaa la biashara (MT4/MT5) angalau mara moja kabla ya kujaribu kutekeleza kisakinishaji sahihi cha EA ya FX Blue.
- Bofya Sawa ili uanze usakinishaji.
- Andika Y kwenye kisanduku na ubofye Sawa ili uendelee.
- Baada ya usakinishaji kukamilika, utaona ujumbe wa uthibitisho kwenye skrini. Bofya OK.
- EA iliyosakinishwa inaweza kupatikana kwenye dirisha la Usogezaji la MT4 au MT5.
Tafadhali kumbuka Exness haiwezi kuwajibikia makosa yoyote katika na yanayotokana na matumizi ya EA ya FX Blue. Ili upate sheria na masharti ya EA ya FX Blue, tembelea fxblue.com/about/terms.
Je, ninawezaje kutatua hitilafu za VPS ya Exness?
Ukikumbana na matatizo katika VPS ya Exness, huenda suluhu limechapishwa kwenye Kituo cha Usaidizi kwa ajili yako. Ikiwa tatizo lako halijaorodheshwa hapa chini, tafadhali wasiliana na Usaidizi ili upate usaidizi zaidi.
- Siwezi kuingia kwenye VPS ya Exness.
- Nimesahau nenosiri langu la VPS ya Exness.
- Utendaji wa VPS ya Exness una kasi ya chini.
- VPS yangu ya Exness imesitishwa na haiwezi kutumika.
- Sina idadi ya majukwaa ya biashara niliyoomba kusakinishwa.
- Ningependa kubadilisha lugha yangu ya VPS ya Exness.
- Ningependa kubadilisha eneo la VPS yangu ya Exness.
Tunapendekeza ufuate kiungo ili upate maelezo ya kina kuhusu VPS ya Exness kwa ujumla.