Kusajili akaunti ya Exness kutafungua Eneo la Binafsi (EB), kituo kikuu ambapo unaweza kudhibiti hatua kama vile kufungua akaunti mpya za kutrade na kubadilisha mipangilio ya akaunti yako.
Hivi ndivyo unavyoweza kusajili akaunti ya Exness:
- Tembelea Tovuti ya Exness na ubofye Jisajili.
- Weka nchi yako ya makazi na anwani ya barua pepe. Vinginevyo, unaweza pia chagua kujisajili kwa kutumia akaunti yako ya Google kwa kubofya Google.
Nchi ya makazi haiwezi kubadilishwa baadaye, huku njia mahususi za malipo za kila nchi zikitolewa katika EB lako; hivyo tafadhali chagua kwa uangalifu.
- Kisha, unda nenosiri. Nenosiri lako linapaswa kufuata masharti yaliyoonyeshwa.
- Bofya Msimbo wa mshirika (kwa hiari) ikiwa ungependa kujisajili chini ya mshirika.
Ukiweka msimbo batili wa mshirika, sehemu hii itafutwa ili ujaribu tena.
- Kisha, weka tiki kwenye kisanduku ili kuthibitisha kuwa wewe si raia au mkazi wa Marekani.
- Bofya Endelea.
Sasa umesajili akaunti ya Exness na utaona Eneo lako la Binafsi (EB). Kwa chaguomsingi, akaunti moja real na moja ya demo ya MT5 hufunguliwa na hupatikana kwenye sehemu ya Akaunti Zangu.
Kumbuka: Ukipokea ujumbe wa hitilafu unaoonyesha kuwa anwani yako ya barua pepe tayari imeunganishwa kwa akaunti, tunapendekeza utafute jinsi ya kurejesha nenosiri lililopotea.
Ili kufungua akaunti mpya ya kutrade:
- Bofya Fungua Akaunti Mpya kwenye sehemu ya Akaunti Zangu.
- Kwa chaguomsingi, akaunti ya kutrade ya MT5 huwa imechaguliwa kwa ajili yako. Unaweza kuibadilisha kwa kubofya MT5 kwenye upande wa juu kulia.
- Kisha, chagua aina ya akaunti yako: Standard, Pro, Raw Spread, au Zero, Standard Cent. Bofya Endelea. Kwa akaunti za demo, chaguo la Standard Cent halipatikani.
- Weka maelezo yafuatayo:
- Leverage ya juu zaidi
- Salio la kuanzia (kwa akaunti za demo pekee)
- Sarafu
- Jina wakilishi la akaunti
- Nenosiri la biashara
- Ukimaliza, bofya Fungua Akaunti.
Ili kuweka pesa, unashauriwa kuwa uthibitishe akaunti yako ya Exness kikamilifu kwanza, kwa kuwa kuna vikomo vinavyowekwa kwenye akaunti za Exness hadi zitakapothibitishwa kikamilifu. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu vipengele vya EB lako, soma Eneo la Binafsi ni nini.