Wakati wa kusajili akaunti mpya ya Exness, unapaswa kukamilisha Wasifu wa Kiuchumi na uwasilishe hati za uthibitisho wa utambulisho (POI) na za uthibitisho wa makazi (POR) kwa uthibitishaji kamili wa akaunti.
Uthibitishaji wa akaunti ni muhimu ili kuhakikisha kuwa ni mmiliki wa akaunti pekee anayeweza kufikia akaunti yake ya Exness. Kwa sababu za usalama, vikomo vya pesa huwekwa kwenye akaunti ambazo hazijathibitishwa na baadhi ya njia za malipo hazipatikani.
Video iliyo hapa chini itakuongoza jinsi ya kuthibitisha akaunti yako ya Exness kikamilifu; huku makala yakielezea uthibitishaji kwa kina zaidi.
- Jinsi ya kuthibitisha kikamilifu akaunti yako ya Exness
- Kuhusu hati za uthibitishaji
- Jinsi ya kuangalia ikiwa akaunti imethibitishwa kikamilifu
- Vikwazo vya akaunti ya Exness ambayo haijathibitishwa
- Kikomo cha muda wa uthibitishaji wa akaunti
- Kuthibitisha akaunti ya pili ya Exness
Jinsi ya kuthibitisha kikamilifu akaunti yako ya Exness
Baada ya kusajili akaunti mpya ya Exness, thibitisha akaunti yako kikamilifu kwa kufuata hatua hizi:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
- Bofya Kuwa Trader wa Real juu ya eneo hili ili kuanza. Kitufe hiki kinaweza kuonekana kwa njia tofauti ikiwa ulikuwa umeanza mchakato wa uthibitishaji hapo awali lakini hukukamilisha.
- Thibitisha anwani yako ya barua pepe, ikiwa bado hujathibitisha.
- Thibitisha nambari yako ya simu, ikiwa bado hujathibitisha.
- Weka taarifa zako za kibinafsi; hakikisha kuwa jina lako kamili ambalo umeweka linalingana kabisa na lililoonyeshwa kwenye hati zako za uthibitishaji.
Katika hatua hii, pesa zinazoweza kuwekwa ni hadi USD 2 000, lakini akaunti ya Exness ambayo haijathibitishwa kikamilifu na pesa zilizowekwa kwa mara ya kwanza zitaanzisha muda wa uthibitishaji wa siku 30.
- Kisha kamilisha Wasifu wa Mteja Kiuchumi, unaohitajika kabla ya hati za uthibitishaji ziweze kuwasilishwa.
- Unaanza hatua ya Kuthibitisha hati kwa kuweka jina lako la kisheria, kisha kubofya Pakia hati ili kuendelea. Kumbuka, jina lako la kisheria sharti lilingane kabisa na hati zote za uthibitishaji, pamoja na jina lililosajiliwa linalotumika kwa njia zozote za malipo zitakazotumika na Akaunti yako ya Exness.
- Kisha utawasilisha hati yako ya uthibitisho wa utambulisho (POI):
- Chagua nchi ambayo ulipata kitambulisho chako kwenye menyu kunjuzi.
- Chagua aina ya kitambulisho.
- Chagua mojawapo ya options ili kuambatisha hati yako ya POI; mifano ya hati za POI zinazoweza kukubalika itaonyeshwa. Bofya Inayofuata ili kuwasilisha hati.
Katika hatua hii, unaweza kuweka pesa za hadi USD 50 000, lakini akaunti ya Exness bado haitakuwa imethibitishwa kikamilifu na bado itakuwa chini ya kikomo cha muda cha siku 30 za uthibitishaji.
- Taarifa kuhusu hati zinazokubalika za uthibitisho wa makazi (POR) zitaonyeshwa; chagua mojawapo ya options za kuambatisha hati yako ya POR, kisha ubofye Inayofuata.
- Ingia kwenye EB lako tena baada ya saa 24 ili kuthibitisha kuwa akaunti yako sasa imethibitishwa kikamilifu. Ikiwa hati zako za uthibitishaji zimekataliwa, unaweza kuanza mchakato tena kuanzia hatua ya 7.
Baada ya kuthibitishwa, vikomo vya pesa zinazoweza kuwekwa vitaondolewa, huku kadi ya benki na njia za malipo zinazotumia cryptocurrencies zikipatikana.
Kuhusu hati za uthibitishaji
Hati za uthibitishaji ambazo ni sahihi na zinazoweza kusomeka ni muhimu, lakini zinaweza kutofautiana kwa kiasi kikubwa kulingana na nchi ambayo akaunti yako ya Exness imesajiliwa.
Tunapendekeza ufuate kiungo kwa maelezo ya kina kuhusu Hati za uthibitishaji wa akaunti ya Exness.
Jinsi ya kuangalia ikiwa akaunti imethibitishwa kikamilifu
Unapoingia kwenye Eneo lako la Binafsi, hali yako ya uthibitishaji huonyeshwa juu ya Eneo la Binafsi.
Hali yako ya uthibitishaji inaonyeshwa hapa.
Vikwazo vya akaunti ya Exness ambayo haijathibitishwa
Vizuizi vimewekwa kwa akaunti za Exness ambazo hazijathibitishwa, ambavyo ni pamoja na:
- kiasi cha juu zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa cha hadi USD 2 000 (kwa kila Eneo la Binafsi) baada ya kukamilisha Wasifu wa Mteja Kiuchumi, ambao huwasilishwa barua pepe yako na nambari yako ya simu zinapothibitishwa.
- Kikomo cha siku 30 cha kukamilisha uthibitishaji wa akaunti kuanzia siku uliyoweka pesa kwa mara yako ya kwanza.
- Uthibitisho wa utambulisho ukishathibitishwa, kiasi cha juu zaidi cha pesa unazoweza kuweka ni USD 50 000 (kwa kila Eneo la Binafsi), pamoja na uwezo wa kutrade.
- Vikomo huondolewa tu baada ya uthibitishaji kamili wa akaunti.
- Siku 30 baada ya kuweka pesa kwa mara ya kwanza, kuweka pesa, kuzihamisha na biashara zitazimwa hadi akaunti yako ya Exness ithibitishwe kikamilifu.
Kikomo cha muda wa uthibitishaji wa akaunti
Akaunti ya Exness ina siku 30 baada ya kuweka pesa kwa mara ya kwanza ili kukamilisha uthibitishaji wa akaunti kikamilifu kabla ya kuweka pesa, kuzihamisha na biashara zaidi kuzimwa. Muda uliosalia wa uthibitishaji unaonyeshwa kwenye Eneo lako la Binafsi.
Jinsi kikomo chako cha muda wa uthibitishaji kinaonyeshwa.
Kikomo cha muda cha siku 30 kinatumika kwa washirika kutoka usajili wao wa mteja wa kwanza. Huduma ya kutoa pesa kwenye akaunti za washirika huzimwa ikiwa hawajathibitishwa ndani ya siku 30.
Kwa kuwa kuweka pesa kutumia cryptocurrency na/au kadi za benki kunahitaji Akaunti ya Exness iliyothibitishwa kikamilifu, njia hizi haziwezi kutumika kamwe hadi akaunti yako ya Exness iwe imethibitishwa kikamilifu.
Kuthibitisha akaunti ya pili ya Exness
Ukiamua kusajili akaunti ya pili ya Exness, unaweza kutumia hati sawa za uthibitishaji zilizotumiwa kuthibitisha akaunti yako ya Exness ya kwanza. Kanuni zote za matumizi hutumika kwa akaunti hii ya pili (mwenye akaunti sharti pia awe mtumiaji aliyethibitishwa).
Comments
0 comments
Article is closed for comments.