- Kuwasilisha hati za uthibitishaji
- Kuangalia akaunti imethibitishwa kikamilifu
- Kikomo cha muda wa uthibitishaji wa akaunti
- Kuhusu akaunti za Exness ambazo hazijathibitishwa
- Kuthibitisha akaunti ya pili ya Exness
Wakati unaposajili akaunti yako ya Exness, unapaswa kujaza Wasifu wa Kiuchumi na uwasilishe Uthibitisho wa Utambulisho (POI) na Uthibitisho wa Makazi (POR). Tunahitaji kuthibitisha hati hizi ili kuhakikisha kwamba shughuli zote kwenye akaunti yako ya Exness zinatekelezwa na wewe, mwenye akaunti halisi.
Tazama video iliyo hapa chini ili kujifunza jinsi ya kupakia hati zako ili kuthibitisha akaunti yako ya Exness kwa hatua chache rahisi:
Kuwasilisha hati za uthibitishaji
Baada ya kukamilisha hatua ya Wasifu wa Kiuchumi ya usajili wa akaunti, utafikia hatua ya uthibitishaji wa hati. Hati hizi ni muhimu sana na kuhakikisha kuwa zinakubalika kutaharakisha sana mchakato wa uthibitishaji.
Utahitaji kuandaa hati mbili (2) tofauti za uthibitishaji wa POI na POR. Kwa mfano, unaweza kutumia pasipoti yako kwa POI na bili yako ya matumizi ya makazi kwa POR.
Hati za POI lazima zitolewe na mamlaka zinazoongoza na lazima ziwe halali wakati wa kuwasilisha. Hati ya POR lazima iwe na umri wa miezi 6 au chini ili iwe halali kwa kuwasilishwa.
Hapa kuna mifano ya hati unazoweza kuwasilisha:
Uthibitisho wa Utambulisho (POI):
- Pasipoti ya kimataifa
- Kadi ya kitambulisho
- Leseni ya udereva
Uthibitisho wa Makazi (POR):
- Bili ya matumizi (umeme, gesi, maji, Intaneti)
- Cheti ya makazi
- Bili ya ushuru
- Taarifa ya akaunti ya benki
Fuata maagizo yaliyoonyeshwa katika hatua hii kama ifuatavyo:
- Ingiza jina lako kamili jinsi linavyoonekana kwenye hati zako zote za uthibitishaji, kisha ubofye Pakia Hati.
- Chagua nchi iliyotoa hati yako ya utambulisho kutoka kwenye menyu kunjuzi, na uchague aina ya hati ya utambulisho. Unaweza kuonyeshwa baadhi ya mifano ya hati zinazokubalika mara tu chaguo hizi zitakapochaguliwa.
- Bofya Pakia hati ili kupakia nakala dijitali ya hati yako ya utambulisho. Unaweza pia kubofya chaguo hapa chini ili kupiga na kupakia picha ya hati yako ya utambulisho. Hakikisha pembe zote za hati zimejumuishwa kwenye picha na maelezo ya kibinafsi yanaweza kuonekana wazi. Baada ya kuambatishwa, bofya Wasilisha hati.
- Zingatia mahitaji ya hati ya uthibitisho wa makazi, kisha ubofye Pakia hati ili kuipakia, au chaguo lililo hapa chini ili kupiga picha hati. Hakikisha pembe zote za hati zimejumuishwa kwenye picha na maelezo ya kibinafsi yanaweza kuonekana wazi. Baada ya kuambatishwa, bofya Wasilisha hati.
Tunapendekeza sana ufuate kiungo kwa uangalizi wa kina katika Hati za uthibitishaji wa akaunti ya Exness.
Kuangalia akaunti imethibitishwa kikamilifu
Unapoingia katika Eneo lako la Kibinafsi, hali yako ya uthibitishaji itaonyeshwa juu ya Eneo la Kibinafsi.
Hali yako ya uthibitishaji inaonyeshwa hapa.
Kikomo cha muda wa uthibitishaji wa akaunti
Kuanzia wakati wa amana yako ya kwanza, unapewa siku 30 za kukamilisha uthibitishaji wa akaunti unaojumuisha uthibitishaji wa utambulisho, makazi na wasifu wa kiuchumi.
Idadi ya siku zilizosalia kwa uthibitishaji inaonyeshwa kama arifa katika Eneo lako la Kibinafsi, ili iwe rahisi kwako kufuatilia kila wakati unapoingia.
Jinsi kikomo chako cha muda wa uthibitishaji kinaonyeshwa.
Kuhusu akaunti za Exness ambazo hazijathibitishwa
Kuna vikwazo vinavyowekwa kwa akaunti yoyote ya Exness ambayo bado haijakamilisha mchakato wa uthibitishaji wa akaunti.
Vizuizi hivi ni pamoja na:
- Kiasi cha juu zaidi cha amana ya hadi USD 2 000 (kwa kila Eneo la Kibinafsi) baada ya kukamilisha Wasifu wa Kiuchumi, na kuthibitisha anwani ya barua pepe na/au nambari ya simu.
- Kikomo cha siku 30 cha kukamilisha uthibitishaji wa akaunti kutoka wakati wa kuweka amana yako ya kwanza.
- Ikiwa uthibitisho wa utambulisho umethibitishwa, kikomo chako cha juu zaidi cha kuweka amana ni USD 50 000 (kwa kila Eneo la Kibinafsi), ukiwa na uwezo wa kufanya biashara.
- Vikwazo hivi huondolewa baada ya uthibitishaji kamili wa akaunti.
- Ikiwa uthibitishaji wa akaunti yako hautakamilika ndani ya siku 30, amana, uhamishaji na utendakazi wa biashara hazitapatikana hadi akaunti ya Exness itakapothibitishwa kikamilifu.
Kikomo cha muda cha siku 30 kinatumika kwa washirika kuanzia wakati wa usajili wao wa kwanza wa mteja, huku hatua za uondoaji kwa mshirika na mteja zikizimwa pamoja na amana na biashara baada ya kikomo cha muda.
Amana zilizo na sarafu digitali na/au zilizo na kadi za benki zinahitaji akaunti ya Exness iliyothibitishwa kikamilifu, kwa hivyo haiwezi kutumika hata kidogo katika kipindi cha utendakazi wenye kikomo cha siku 30, au hadi akaunti yako itakapothibitishwa kikamilifu.
Kuthibitisha akaunti ya pili ya Exness
Ukiamua kusajili akaunti ya pili ya Exness, unaweza kutumia hati sawa na ambazo zilitumika kuthibitisha akaunti yako ya msingi ya Exness. Sheria zote za utumiaji za akaunti hii ya pili bado zinatumika, kwa hivyo ni lazima mmiliki wa akaunti awe mtumiaji aliyeidhinishwa.