VPS service ya Exness huwezesha watumiaji kuendesha mikakati ya biashara ya kiotomatiki bila kuathiriwa na vikwazo vya kompyuta ya mezani ya kibinafsi au vya muunganisho wa intaneti.
Watumiaji wapya wanahimizwa kufuata mwongozo wetu wa mtumiaji wa mara ya kwanza wa VPS ya Exness.
Je, VPS ni nini?
+Seva ya kibinafsi ya mtandaoni (VPS) ni mfumo wa kompyuta unaodhibitiwa kwa mbali kutoka mahali popote duniani. Seva za VPS hukuruhusu kuendesha mikakati ya biashara ya kiotomatiki bila kuathiriwa na vikwazo vya muunganisho wa kompyuta ya mezani au mtandao.
VPS ni zana muhimu kwa traders wenye uzoefu ambao wangependa kufanya biashara yao iwe ya kiotomatiki na kuboresha muda wao wa kujibu.
Faida za VPS ya Exness
+- Kasi: Seva za VPS ziko karibu na seva za biashara za Exness zilizoko Amsterdam, Hong Kong, Singapore, Miami na Johannesburg; hii huhakikisha execution ya haraka na ya kutegemewa.
- Uthabiti: VPS haitegemei ubora wa muunganisho wako wa intaneti kwa sababu ni kompyuta pepe; kwa hivyo, muunganisho wako wa kibinafsi wa mtandao hautaathiri execution ya orders.
- Biashara ya saa 24: fanya trade kwa kutumia Expert Advisors (EA) hata wakati kompyuta yako imezimwa.
- Uwezo wa kubebeka: inaweza kufikiwa kwenye mfumo wowote wa uendeshaji (Windows, Mac OS, Linux) au kifaa chochote (kompyuta ya mezani, kompyuta kibao, simu, vipakatalishi).
- Uhamaji: fanya trade popote ulipo ulimwenguni ukitumia akaunti yako ya Exness.
Unaweza kutumia VPS yako mwenyewe kutrade kwenye seva zetu. Hata hivyo hatuwezi kuhakikisha ubora wa muunganisho wako wa VPS, ndiyo maana tunapendekeza VPS ya Exness.
Vigezo vya VPS ya Exness
+VPS ya Exness inahitaji kufikia vigezo vya salio la jumla la akaunti na/au jumla ya kiwango cha biashara. Vigezo mahususi vya kufikiwa na masharti yanayotumika yanaweza kupatikana kwenye Eneo lako la Binafsi; ingia kwenye EB lako (Mipangilio kisha Seva Pepe ya Kibinafsi) ili kuthibitisha vigezo hivi.
Vigezo vya kiwango cha biashara
Kiwango cha biashara hakizingatii akaunti za kutrade za Social Trading/Usimamizi wa Portfolio zilizofunguliwa na wawekezaji, lakini akaunti za kutrade zinazotumiwa na Watoa Mkakati na Wasimamizi wa Portfolio kutrade hazijumuishwi.
Je, ninawezaje kukokotoa kiwango kilichofanyiwa trade katika lots?
Inasaidia kuelewa jinsi ya kukokotoa mchango wa lot kwa instrument ya biashara kwa vigezo vya jumla vya kiwango cha biashara:
- Lot yoyote inayofanyiwa trade kikamilifu inajumuisha hali ya iliyofunguliwa na iliyofungwa, ambayo pamoja inafafanuliwa kama lot moja ya ununuzi na uuzaji.
- Orders zilizofunguliwa hufafanuliwa kama lot moja; order hiyo inapofungwa inakuwa lot ya ununuzi na uuzaji.
- Contract size ya instrument hukokotolewa kama kiwango cha biashara order inapofunguliwa (lot ya kawaida) na tena wakati order imefungwa (lot ya ununuzi na uuzaji).
Order iliyofanyiwa trade kikamilifu (kufunguliwa na kufungwa) huchangia katika contract size ya instrument ya biashara mara dufu ya kiwango chako cha biashara.
Mifano ya ukokotoaji:
- Lot 1 iliyofunguliwa ya USDJPY huchanga USD 100,000 kwa kiwango chako cha biashara.
- Baada ya kufunga lot 1 ya ununuzi ya USDJPY, hii hukuwa lot moja ya ununuzi na uuzaji na huchangia USD 200,000 kwa kiwango chako cha biashara.
- Kwa hivyo ili kufikia kigezo cha kiwango cha biashara cha USD milioni 1.5 (kwa mfano), ni lots 7.5 za USDJPY pekee zilizofanyiwa trade kikamilifu zinazohitajika.
Ili kukokotoa unahitaji lots ngapi zilizofanyiwa trade kikamilifu kwa instrument ya biashara, tumia ukokotoaji ufuatao:
Lot iliyofanyiwa trade kikamilifu = ((kiwango kilichofanyiwa trade katika USD / sarafu ya msingi hadi kiwango cha USD) / contract size) / 2
Ukokotoaji huu unaweza kutumika kwa instrument yoyote ya biashara; kama inavyoonyeshwa hapa chini kwa mfano wa kiwango cha biashara cha USD milioni 1.5:
- Cryptocurrencies: ikiwa bei ya BTCUSD = 30,000, basi ((1,500,000 / 30,000) / 1) / 2 = lots 25 za ununuzi na uuzaji.
- Forex: ikiwa bei ya EURUSD = 1.07, basi ((1,500,000 / 1.07) / 100,000) / 2 = lots 7 za ununuzi na uuzaji.
- Indices: ikiwa JPY225 ni 0.0078 dhidi ya USD kwa contract size ya 26,000, basi ((1,500,000 / 0.0078) / 26,000) / 2 = lots 3,700 za ununuzi na uuzaji.
- Hisa: ikiwa hisa ya TSLA ni USD 116, basi ((1,500,000 / 116) / 100) / 2 = lots 64.5 za ununuzi na uuzaji.
- Nishati: ikiwa bei ya UKOIL ni USD 84, basi ((1,500,000 / 84) / 1,000) / 2 = Lots 9 za ununuzi na uuzaji.
Katika mifano hii, ni kiasi cha lot ya ununuzi na uuzaji pekee kinachohitaji kufanyiwa trade ndani ya siku 30 za kalenda ili kutimiza masharti kwa VPS ya Exness (pamoja na salio la jumla la akaunti kati ya USD 500 na 1,999). Zingatia bei ya kati ya sarafu ya msingi kila wakati (kati ya bid na ask) wakati wa order ili kuongoza ubadilishaji wa lots hadi USD.
Jinsi ya kutuma maombi
+- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Bofya Mipangilio (menyu ya upande wa kushoto).
- Fungua kichupo cha Seve Pepe ya Kibinafsi.
- Ikiwa umetimiza masharti ya vigezo, utaona uthibitisho.
- Bofya Tuma ombi la VPS hosting.
- Chagua idadi ya terminali za biashara zinazopatikana na lugha ya mfumo wa uendeshaji na eneo la seva ya VPS, kisha ubofye Tuma Ombi la VPS hosting ili uthibitishe.
- Kumbuka: Kiasi na lugha za terminali ya biashara haziwezi kubadilishwa bila kusakinisha upya VPS. Ili kubadilisha eneo, tumia options za Futa Seva na Tuma ombi la VPS hosting (hatua ya 5) tena.
- Kubali Makubaliano ya Mtumiaji ya VPS kwa kubofya Kubali na uendelee .
- Ombi lako la VPS ya Exness sasa limewasilishwa. Rudi hapa ili kuangalia hali ya ombi lako; inapoonyesha “Mtandaoni ”, iko tayari kutumika.
Jinsi ya kuunganisha
+Mara tu ombi lako la VPS ya Exness litakapokamilika, EB lako litaionyesha kama Mtandaoni na VPS ya Exness sasa inapatikana ili uweze kuunganisha.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Bofya Mipangilio kwenye menyu ya upande wa kushoto.
- Fungua kichupo cha Seve Pepe ya Kibinafsi.
- Kando na kichwa cha Seva Pepe ya Kibinafsi, thibitisha kuwa VPS ya Exness iko Mtandaoni.
- Bofya Ingia.
- Arifa ibukizi itaonyesha maelezo yako ya VPS ya Exness ( Anwani ya VPS, Maelezo ya kuingia kwenye VPS na Nenosiri la VPS).
- Bofya Fuata maagizo ya muunganisho wa VPS na ufuate maagizo kwenye skrini ambayo yanajitokeza.
- Ukishakamilisha maagizo, utaunganishwa kwa Exness VPS.
Kabla ya kutumia VPS ya Exness kufanya biashara, tunapendekeza sana uweke nenosiri la kipekee kwanza.
Kwa Exness Trade
Ili kuunganisha na Exness Trade:
- Fungua programu ya Exness Trade.
- Bofya kichupo cha Wasifu.
- Chagua option ya VPS.
- Fuata hatua sawa zilizoelezewa hapo juu ili toleo la tovuti lipate maelezo yako ya kuingia kwenye VPS ya Exness.
Kwa Windows
Hivi ndivyo unavyoweza kuunganisha kwenye kifaa cha Windows:
- Andika Remote Desktop Connection kwenye menyu ya Mwanzo kisha uanzishe programu hii.
- Weka Anwani ya VPS (iliyoonyeshwa kwenye hatua ya 6 hapo juu) panapohitajika.
- Ikiwa unapanga kutumia Expert Advisors (EA), fuata hatua hizi za ziada kabla ya kuendelea:
- Bofya Show Options kwenye dirisha la Remote Desktop Connection.
- Nenda kwenye kichupo cha Local Resources. Chini ya Local devices and resources, chagua More. Kumbuka: Hatutawahi kufikia faili zako za kibinafsi zilizohifadhiwa kwenye VPS.
- Weka alama kwenye kisanduku kilicho karibu zaidi na maelezo ya faili ambapo EA zako zinapatikana, kisha ubofye OK.
- Sasa bofya Connect.
- Weka Maelezo ya kuingia kwenye VPS na Nenosiri la VPS (ilivyoonyeshwa kwenye hatua ya 6 hapo juu) na uthibitishe maelezo haya kwa kubofya OK .
Kwa Mac
Hapa unavyoweza kuunganisha kwa kutumia kifaa cha Mac.
- Pakua programu ya Microsoft Remote Desktop kutoka kwa duka la programu.
- Anzisha programu na ubofye Add PC.
- Weka Anwani ya VPS (ilivyoonyeshwa kwenye hatua ya 6 hapo juu) kwenye sehemu ya PC Name.
- Chagua menyu kunjuzi ya User Account na uchague Add User Account.
- Weka Maelezo ya kuingia kwenye VPS na Nenosiri la VPS (ilivyoonyeshwa kwenye hatua ya 6 hapo juu) na uthibitishe maelezo haya kwa kubofya Add.
- Bofya Add ili ukamilishe mipangilio hii.
- Chagua na uanzishe Kompyuta hii ya mbali katika programu ya Microsoft Remote Deposit. Bofya Continue ikiwa ujumbe wa uthibitishaji utawasilishwa.
Ukiweka maelezo ya VPS ya Exness yasiyo sahihi mara kadhaa, anwani yako ya IP itazuiliwa kufikia huduma ya VPS kwa muda; subiri kama saa moja kabla ya kujaribu tena.
Ingawa inawezekana kuingia kwenye VPS kwa kutumia akaunti yoyote ya kutrade ya MT, inapendekezwa kuwa matumizi yako ya Exness VPS yawe ni ya akaunti zako za kibinafsi za kutrade. Tafadhali rejelea Masharti ya Matumizi ya VPS ya Exness kwa maelezo zaidi.
Anzisha upya/Washa upya VPS
+Kuanzisha upya VPS yako kunaweza kusaidia kutatua utendaji wa VPS; fuata kiungo kwa Mada zetu za utatuzi wa VPS.
Ili kuzuia kupotea kwa taarifa za biashara wakati wa kuanzisha upya VPS, zima mipangilio yoyote ya biashara ya kiotomatiki na uiwezeshe baada ya kuwasha upya VPS, au ufuatilie hali ya uendeshaji ya Expert Advisors.
Ili kuanzisha upya kwenye EB lako:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Bofya Mipangilio kwenye menyu ya upande wa kushoto.
- Fungua kichupo cha Seve Pepe ya Kibinafsi.
- Bofya Washa upya kisha uthibitishe hatua ya kuwasha upya.
- Seva ya VPS sasa itaanza upya.
Ili kuanzisha upya ukiwa umeingia:
- Bofya kwenye Start (aikoni ya Windows).
- Bofya kitufe cha kuwasha/kuzima na uchague Restart.
Maombi ya order mpya, marekebisho ya order na kughairiwa kwa order hakuwezekani kwenye majukwaa ya biashara yaliyosakinishwa kwa VPS baada ya kuanzishwa upya. Hata hivyo, orders zilizofunguliwa zitabaki zikiwa zimefunguliwa na Expert Advisors zozote zikiendelea kufanya kazi.
Kufuta VPS
+Unapofuta VPS yako data yote ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na Expert Advisors, hutolewa kwa mfumo. Mchakato huu hauwezi kubatilishwa, lakini unaweza kuwa muhimu kama kuanzisha upya.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Bofya Mipangilio kwenye menyu ya upande wa kushoto.
- Fungua kichupo cha Seve Pepe ya Kibinafsi.
- Bofya aikoni ya nukta 3 (karibu na kitufe cha Washa upya) kisha uchague Futa Seva.
- Thibitisha kuwa ungependa kufuta seva.
Kusakinisha upya VPS
+Kusakinisha upya VPS huruhusu watumiaji kusanidi upya kiasi cha majukwaa ya biashara yaliyojumuishwa katika VPS, lugha chaguo-msingi ya VPS, pia husaidia katika maswala kadhaa ya utatuzi wa masuala ya VPS.
Kwanza hifadhi nakala ya data yako, ikiwa ni pamoja na scripts na Expert Advisors kisha:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
- Fungua Mipangilio na uchague option ya Seva Pepe ya Kibinafsi.
- Bofya aikoni ya nukta 3 (kona ya juu kulia) kando ya kitufe cha Washa upya.
- Chagua lugha unayopendelea na idadi ya terminali ambazo ungependa kusakinisha.
- Ukimaliza, chagua Sakinisha upya VPS (data yote itaondolewa; ndio maana inapendekezwa uhifadhi nakala ya data).
Ikiwa hatua hizi hazikusaidia, tafadhali fungua tikiti kwenye kituo cha usaidizi kwa usaidizi zaidi.
Kupoteza ufikiaji
+Utapoteza uwezo wa kufikia VPS ya Exness ikiwa utashindwa kufikia kiwango mahususi cha biashara (au kiasi sawa kwa sarafu/mali yoyote) kwa kipindi cha siku 30, kipindi cha siku 90, au kipindi cha siku 180. Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi ili kuthibitisha kiwango cha biashara kinachohitajika kwa akaunti yako.
Ni orders kutoka Akaunti za real pekee zinazozingatiwa kwa vigezo vya kiwango cha biashara na sio akaunti za demo.
Ni kigezo kimoja pekee cha muda kinachohitajika ili kudumisha ufikiaji wa VPS ya Exness.
- Usipofikia vigezo vyovyote vya kiwango cha biashara vinavyohitajika kwa siku 30 mfululizo za kalenda, VPS yako itasitishwa na data yako yote ya mtumiaji ya VPS itafutwa na haiwezi kurejeshwa.
- Kukiuka masharti ya matumizi ya VPS ya Exness kunaweza kusababisha kupoteza ufikiaji wa VPS ya Exness.
Maonyo ya kutotumika kwa VPS hutumwa mara kwa mara kwa siku 30 zinazofuatana za kalenda (siku ya 20, 28, 29, na haswa 30). Ikiwa vigezo vinavyohitajika bado havijafikiwa, VPS itasitishwa. Pending orders hazichangii kwa jumla ya kiwango cha biashara.
VPS isiyotumika
Unaweza kupoteza ufikiaji ikiwa vigezo vifuatavyo havitatimizwa:
- Sharti uingie na ufanye trade kwenye VPS ukitumia akaunti ya kutrade iliyounganishwa ya VPS ndani ya siku 5 baada ya VPS kutolewa. Utapokea maonyo siku ya 3 na siku ya 5 kabla ya VPS kusitishwa (pending orders hazijumuishwi).
- Sharti uingie na ufanye trade kwenye VPS angalau mara moja kila baada ya siku 30 au VPS hiyo itasitishwa, bila kujali kama unatimiza vigezo vya siku 90 au 180. Utapokea maonyo siku ya 27 na siku ya 30 kabla ya VPS kusitishwa (pending orders hazijumuishwi).
Kwa mfano:
VPS hutolewa tarehe 1 Juni:
- Mteja huingia na kufanya trade kwa kutumia VPS tarehe 4 Juni (ndani ya Siku 5 kutoka tarehe ya utoaji wa VPS).
- Sharti mteja aingie na afanye trade tena kwa kutumia VPS kati ya tarehe 5 Juni hadi 4 Julai (siku 30 tangu trade ya mwisho kwenye VPS) na vipindi vinavyofuata.
Kurejesha VPS ya Exness
+Unaweza kutuma tena ombi la VPS ya Exness wakati wowote inapokufaa zaidi lakini sharti utimize vigezo vya masharti na ufuate hatua sawa na kutuma maombi ya VPS ya Exness.
Kiwango cha biashara pekee ndicho kinachozingatiwa kwa vigezo vya kutimiza masharti unapotuma maombi tena ya VPS ya Exness.
VPS ya Exness inapositishwa, data yote ya mtumiaji iliyo ndani ya kompyuta pepe hufutwa, ikiwa ni pamoja na Expert Advisors zilizopakiwa, mapendeleo ya saa za kimaeneo na manenosiri maalum. Data ya mtumiaji haiwezi kurejeshwa na hupotea kabisa.