Baada ya kujisajili na kuthibitisha kikamilifu akaunti yako ya Exness, uko tayari kuanza kutrade kwa hatua chache rahisi:
Weka pesa kwa mara yako ya kwanza
Kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza hutegemea aina ya akaunti uliyochagua: Standard au ya Kitaaluma.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
- Nenda kwenye kichupo cha Uwekaji fedha.
- Chagua njia ya malipo unayopendelea.
- Fuata vidokezo ili kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza.
Ujumbe wa hitilafu ya “Trade is Disabled" utaonekana kwenye jukwaa la biashara wakati wa kufungua order kabla ya masharti ya kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa kufikiwa.
Chagua jukwaa la biashara
Haya ni majukwaa ya biashara yanayopatikana tunayotoa na jinsi ya kuingia:
- Programu ya Exness Trade: Pakua programu ya Exness Trade na uingie ukitumia maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako ya Exness.
- Terminali ya Exness: Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB) bofya Trade kwenye akaunti yoyote inayotumika ya kutrade na uchague Terminali ya Exness.
- Majukwaa ya kompyuta ya mezani ya MetaTrader: Pakua na usakinishe MetaTrader 4 au MetaTrader 5 kwenye kifaa chako cha mezani na uingie ukitumia maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako ya kutrade.
- Majukwaa ya kifaa cha mkononi ya MetaTrader: pakua na usakinishe MetaTrader 4 au MetaTrader 5 kwenye kifaa chako cha mkononi, kisha ingia ukitumia maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako ya kutrade.
- WebTerminal: Ingia kwenye WebTerminal kwenye tovuti yetu kwa kutumia maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako ya kutrade.
- MultiTerminal ya MT4: Pakua na usakinishe MultiTerminal ya MT4 kwenye kompyuta yako ya mezani ya Windows na uingie ukitumia akaunti yako ya kutrade.
Huwezi kutumia akaunti ya kutrade ya MT4 kwenye jukwaa la biashara la MT5 na kinyume chake. Huwezi kubadilisha uoanifu wa akaunti ya kutrade baada ya kufunguliwa.
Ongeza instruments zako za biashara unazopendelea
Ongeza instrument yoyote ambayo ungependa kutrade, ikiwa ni pamoja na forex , bidhaa , stocks na indices, kwa vipendwa vya jukwaa lako la biashara ulilochagua kwa urahisi.
Kwenye Terminali ya Exness, ongeza instruments kwenye upau wa kutafutia kisha uchague instrument ili kuonyesha chati yake.
Kwenye Programu ya Exness Trade, nenda kwenye kichupo cha Trade na uchague instrument yako kutoka kwa orodha inayoonyeshwa ya instruments au uweke instrument hiyo kwenye upau wa kutafutia.
Ongeza instruments za biashara kwenye dirisha lako la Taarifa za Soko katika majukwaa ya kifaa cha mkononi na ya kompyuta ya mezani ya MetaTrader.
Kokotoa margin
Margin ni kiasi kilichohifadhiwa kinachohitajika ili kufungua na kudumisha position ya biashara yenye leverage. Hakikisha kuwa una funds za kutosha kwenye akaunti yako ili kufungua na kudumisha trade.
Jaribu kikokotoo chetu cha biashara ili kukokotoa margin inayohitajika.
Angalia saa za biashara
Ilhali biashara inapatikana 24/5*, kujua saa za biashara za soko, saa za biashara za instrument, saa za biashara za majira ya joto/baridi na mapumziko ya kila siku kunaweza kurahisisha biashara.
Jua saa za soko kwa kila instrument ya biashara katika makala yafuatayo:
- Saa za biashara za jozi za sarafu za forex
- Saa za biashara za bidhaa
- Saa za biashara za cryptocurrencies
- Saa za biashara za indices
- Saa za biashara za stocks
*Biashara kwenye baadhi ya instruments kama vile cryptocurrencies hupatikana kwa wiki nzima, hata katika wikendi.
Anza kutrade
Sasa uko tayari kuanza kutrade.
Angalia miongozo yetu ya kina: