Hongera kwa kuanza safari yako ya biashara na Exness. Baada ya kusajili na kuthibitisha akaunti yako kikamilifu, ni wakati wa kuanza kutrade. Makala haya yatakuongoza katika hatua za kuanza kufanya biashara na Exness.
- Weka pesa
- Chagua jukwaa la biashara
- Ongeza instruments za kutrade
- Kokotoa margin
- Angalia saa za biashara
- Anza kutrade
1. Weka pesa kwa mara yako ya kwanza
Pesa unazoweka kwa mara yako ya kwanza hutegemea aina ya akaunti uliyochagua, ikiwa ni akaunti ya Standard au Kitaaluma. Pata maelezo zaidi kuhusu kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza kabla ya kuchagua njia ya malipo inayofaa zaidi.
Jinsi ya kuweka pesa:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
- Nenda kwenye kichupo cha Uwekaji fedha.
- Chagua njia yako ya malipo unayopendelea.
- Fuata vidokezo vifuatavyo ili kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza.
Kumbuka: Biashara imezimwa kwa chaguomsingi hadi masharti ya kiasi cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa yatimizwe. Ujumbe wa hitilafu unaoonyesha “Trade Imezimwa”, ikiwa unajaribu kufungua trade bila kuweka pesa.
2. Chagua jukwaa la biashara
Tunatoa majukwaa mbalimbali ya biashara kwa urahisi wako. Pata maelezo ya majukwaa ya biashara na jinsi yanavyolingana kabla ya kuchagua jukwaa linalokufaa zaidi.
Hizi ndizo terminali za biashara tunazotoa na jinsi ya kuingia:
-
Programu ya Exness Trade
- Pakua Programu ya Exness Trade na uingie kwa kutumia akaunti yako ya Exness.
-
Terminali ya Exness
- Ingia kwenye Eneo la Binafsi (EB), bofya kwenye aikoni ya menyu kwenye sehemu ya mada ya juu, na ubofye kwenye Terminali ya Exness.
-
Terminali za Kompyuta ya mezani za MetaTrader 4 au MetaTrader 5
- Pakua na usakinishe jukwaa ulilochagua la MetaTrader 4 au MetaTrader 5 kwenye kompyuta yako ya mezani, na uingie ukitumia maelezo yako ya kuingia katika Exness.
-
WebTerminal ya MT4/MT5
- Ingia kwenye WebTerminal kwenye tovuti yetu kwa kutumia nambari yako ya akaunti, nenosiri na seva.
-
Terminali za Vifaa vya Mkononi za MetaTrader
- Pakua na usakinishe programu ya MetaTrader 4 au programu ya MetaTrader 5 kwenye simu yako na uingie kwa kutumia maelezo yako ya kuingia katika Exness.
-
Multiterminal ya MT4
- Pakua na usakinishe Multiterminal ya MT4 kwenye kompyuta yako ya mezani ya Windows na uingie kwa kutumia akaunti yako ya kutrade.
Kumbuka: Ukifungua akaunti ya MetaTrader 4, hutaweza kuingia kwenye MetaTrader 5 kwa kutumia maelezo yako ya kuingia kwenye MT4 yako na kinyume chake. Ikiwa ungependa akaunti za MT4 na MT5, itabidi uzifungulie akaunti tofauti za kutrade.
3. Ongeza instruments zako za biashara unazopendelea
Tunatoa instrument mbalimbali za biashara ikiwa ni pamoja na Forex, Bidhaa, Stocks, na Indices. Kwenye jukwaa lako la biashara ulilochagua, unaweza kuongeza instruments ambazo ungependa kutrade.
Ukiwa na Terminali ya Exness, ongeza instruments kwa kutafuta instrument kwenye upau wa kutafutia, na kisha kuchagua instrument hiyo ili kuonyesha chati yake na kuanza kuifuatilia.
Kwenye Programu ya Exness Trade, nenda tu kwenye kichupo cha Trade na uchague instrument yako kwenye orodha iliyoonyeshwa ya instruments, au utafute kwa haraka kwa kuandika jina la instrument hiyo kwenye upau wa kutafutia.
Ikiwa unafanya trade kwa kutumia majukwaa ya simu ya mkononi na ya kompyuta ya mezani, unaweza kuongeza instruments za biashara kwenye kwenye Taarifa zako za Soko. Pata maelezo ya jinsi ya kufanya hivyo katika makala yafuatayo:
- Jinsi ya kutumia MetaTrader 4
- Jinsi ya kutumia MetaTrader 5
- Jinsi ya kutumia WebTerminal ya MetaTrader
- Jinsi ya kutumia Multiterminal ya MT4
4. Kokotoa margin
Margin ni kiasi kilichobakizwa kinachohitajika ili kufungua na kudumisha position ya biashara yenye leverage. Ili kukokotoa margin inayohitajika kwa instrument yoyote kwa leverage yoyote, tumia Kikokotoo cha Uwekezaji. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Kikokotoo cha Uwekezaji.
Inapendekezwa uhakikishe kuwa una funds za kutosha kwenye akaunti yako ili kufungua na kudumisha trade.
5. Angalia saa za soko
Ingawa kutrade katika Exness kunapatikana 24/5*, Ni muhimu kufahamu saa za biashara za soko, saa za biashara ya instrument, saa za biashara za majira ya joto/baridi, na mapumziko ya kila siku kabla ya kutrade.
Jua saa za soko kwa kila instrument ya biashara katika makala yafuatayo:
- Saa za biashara za jozi za sarafu za forex
- Saa za biashara za Bidhaa
- Saa za biashara za Cryptocurrencies
- Saa za biashara za Indices
- Saa za biashara za Stocks
*Kufanya biashara kwenye baadhi ya instruments kama vile cryptocurrencies kunapatikana kila siku ya wiki, hata wikendi.
6. Anza kutrade
Sasa uko tayari kuanza kutrade. Hapa kuna hatua fupi za kufungua na kufunga trade kwa kutumia Terminal ya Exness na programu ya Exness Trade.
Ingia kwenye Terminali ya Exness sasa
Fungua na ufunge trade kwenye Terminali ya Exness
Ili kufungua:
- Kwenye chati ya instrument uliyochagua, bofya Sell au Buy.
- Weka kiwango cha order katika lots, sarafu au vitengo.
- Unaweza pia kuweka pending order, take profit, na stop loss.
- Baada ya kumaliza, bofya Thibitisha.
Ili kufunga:
- Bofya tu aikoni ya x kwenye order kwenye kichupo cha Portfolio.
Fungua na ufunge trade katika Exness Trade
Ili kufungua:
- Kwenye kichupo cha Trade, chagua instrument ambayo ungependa.
- Bofya Sell au Buy kwenye skrini inayofuata.
- Chagua idadi ya lots, sarafu au vitengo na ubofye Thibitisha.
Ili kufunga:
- Kwenye kichupo cha Akaunti, tafuta order ambayo ungependa kufunga chini ya kichupo cha Zilizofunguliwa.
- Bofya order ambayo ungependa kufunga, kisha ubofye Funga order.
- Dirisha ibukizi la uthibitisho litaonyesha maelezo ya order; bofya Thibitisha ili kufunga order.
Hapa kuna makala ambayo yanaweza kukufaa wakati wa safari yako ya biashara:
- Je, ninaweza kutrade instruments gani?
- Je, huduma ya VPS ya Exness ni nini?
- Je, ni vipengele gani vya usalama vinavyotolewa kwa akaunti yangu ya Exness?
- Je, ninawezaje kudhibiti mipangilio ya akaunti yangu ya kutrade?
- Je, ninapaswa kujua nini kuhusu akaunti za swap-free?
Ukikumbana na matatizo yoyote, rejelea miongozo yetu ya utatuzi ili kuyasuluhisha. Vinginevyo, unaweza kuwasiliana na Usaidizi kila wakati.
Comments
0 comments
Article is closed for comments.