Hatua ya 1: Jisajili na ufungue akaunti
Hatua ya 2: Kamilisha uthibitishaji wa akaunti
Hatua ya 3: Weka amana yako ya kwanza
Hatua ya 4: Chagua kituo cha biashara
Hatua ya 5: Anza kufanya biashara
Huu ni mwongozo wa jinsi unaweza kuwa na akaunti yako ya Exness na kuiendeleza katika hatua 5 rahisi:
-
Jisajili na ufungue akaunti yako
Ili kusajili akaunti yako ya Exness, tembelea Exness.com na ubofye kitufe cha Fungua akaunti kilicho juu ya skrini. Fuata kiungo upate mwongozo wa kina kuhusu jinsi ya kusajili akaunti yako ya Exness, au utazame video ya mafunzo ifuatayo:
-
Kamilisha uthibitishaji wa akaunti
Pili, utahitaji kuthibitisha kwa ukamilifu akaunti yako ya Exnesskwa kukamilisha vitendo vifuatavyo:
- Thibitisha anwani ya barua pepe na nambari yako ya simu.
- Jaza fomu ya Wasifu wa Kiuchumi.
- Wasilisha Ushahidi wa Utambulisho (POI).
- Wasilisha Ushahidi wa Makazi (POR).
Tunahitaji kuthibitisha maelezo haya ili kuhakikisha kwamba shughuli zote kwenye akaunti zinatekelezwa na wewe, na si mtu mwingine.
Tazama video hii kuhusu jinsi ya kuthibitisha kikamilifu akaunti yako ya Exness:
-
Weka amana yako ya kwanza
Mara tu akaunti yako itakaposanidiwa, unaweza kuweka amana katika akaunti ya biashara ili uanze kufanya biashara. Kichupo cha Amana cha Eneo la Kibinafsi kitaonyesha njia zote za malipo zinazopatikana katika eneo lako. Bofya kwenye njia ya malipo ya chaguo lako ili kuonyesha mahitaji yake ya uthibitishaji. Tunapendekeza usome zaidi kuhusu kuweka amana yako ya kwanza ili uweze kuchagua njia ya malipo inayokufaa.
Kumbuka: Ufanyaji biashara umezimwa kwenye akaunti halisi zilizoundwa upya hadi mahitaji ya chini zaidi ya amana yatimizwe. Utaona ujumbe wa hitilafu wa 'Biashara Imezimwa' ikiwa unajaribu kufungua biashara bila kuweka amana.
-
Chagua kituo cha biashara
Tunatoa anuwai ya vituo vya biashara ikiwa ni pamoja na vituo vya kompyuta ya mezani, vituo vya vifaa vya mkononi na vituo vya wavuti.
Soma kuhusu kufahamu vituo vya biashara kwa maelezo zaidi.
-
Anza biashara
Kwa kuwa sasa umefungua akaunti yako ya biashara na umechagua kituo cha biashara, unaweza kuanza kufanya biashara. Fuata kiungo ili upate mwongozo muhimu kuhusu jinsi ya kuanza kufanya biashara na mengine mengi.
Rasilimali zinazosaidia
Kituo cha Usaidizi
Kituo chetu cha Usaidizi ni sehemu moja inayoshughulikia hoja zote zinazohusiana na Exness. Kinajumuisha:
- Miongozo ya Eneo la Kibinafsi na matumizi ya mifumo mbalimbali ya malipo.
- Maelezo ya kina juu ya uanzishaji wa majukwaa mbalimbali ya biashara.
- Masuluhisho ya Utatuzi wa shida kwa matatizo ya kawaida ambayo unaweza kukutana nayo.
Tovuti ya Elimu
Tovuti yetu ya Elimu ina taarifa nyingi muhimu kuhusu biashara na sekta ya CFD kwa ujumla. Unaweza kupata:
- Miongozo ya video kuhusu ubadilishanaji wa sarafu.
- Uchambuzi na semina za wavuti
- Faharasa ya maneno yanayohusiana na ubadilishanaji wa sarafu.