Exness hutoa aina mbalimbali za njia za malipo za kuweka pesa kwa urahisi kutoka sahemu yoyote ya ulimwengu. Malipo hukubaliwa kutoka kwa akaunti zilizosajiliwa kwa jina la mteja pekee, kwa hivyo akaunti za wahusika wengine hazikubaliwi.
Akaunti za kutrade huonyesha hitilafu ya "trading disabled" kwenye terminali ya biashara ikiwa biashara inajaribiwa kabla ya kuweka kiasi cha pesa kinachotimiza masharti kwa mara ya kwanza; kamilisha hatua ya kuweka pesa ili kutatua hitilafu hii.
Mambo mawili muhimu ya kuzingatia wakati wa kuweka amana:
Njia rahisi zaidi ya kuweka pesa kwa mara ya kwanza itategemea ni njia gani za malipo zinapatikana katika eneo lako. Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi ili uende kwenye sehemu ya Kuweka pesa na uangalie maelezo kama vile kiasi cha chini zaidi/juu zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa na muda wa uchakataji.
Njia ya malipo
Hatua yako ya kwanza ni kuchagua njia ya malipo kwa hivyo zingatia yafuatayo:
- Kamilisha wasifu wako wa kiuchumi na uthibitishaji wa utambulisho: baadhi ya njia za malipo zina masharti ya uthibitishaji, kwa hivyo tunakuhimiza uthibitishe akaunti yako kikamilifu ili kuwezesha njia zote za malipo.
- Chagua sarafu inayofaa: kuweka pesa kwa sarafu sawa na ile iliyowekwa kwenye mipangilio ya akaunti yako ya kutrade hukusaidia kuepuka gharama za ubadilishaji. Hata hivyo, sarafu ya akaunti haiwezi kubadilishwa akaunti ya kutrade inapofunguliwa.
Kidokezo: Unaweza kufungua akaunti mpya za kutrade ikiwa unahitaji moja kuwekwa kwa sarafu maalum.
- Kasi ya uchakataji wa hatua za kuweka pesa: muda wa uchakataji wa njia ya malipo hutofautiana, kwa hivyo uthibitishe katika Eneo lako la Binafsi.
- Ada za uwekaji wa pesa: njia nyingi za malipo hazitozi ada za kuweka pesa kwenye akaunti zako za kutrade, lakini zinaweza kuhitaji kiasi cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa ili kuepuka ada za uwekaji wa pesa kutoka kwa washirika wengine. Thibitisha ada zozote za uwekaji wa pesa kutoka kwa mhusika mwingine kabla ya kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza.
Kiasi cha pesa kinachoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza
Ukishachagua njia unayopendelea ya kuweka pesa, zingatia ni kiasi gani cha pesa utakachoweka.
Masharti ya kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza yatategemea aina ya akaunti ya kutrade na njia ya malipo iliyochaguliwa.
- Aina ya akaunti: aina za akaunti za kitaaluma zina kiasi chao cha kipekee cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza, lakini masharti haya ya kiasi cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa yanatumika tu kwa kuweka pesa kwa mara ya kwanza. Aina za akaunti za Standard huhitaji tu kiasi cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza kinacholingana na njia ya malipo iliyochaguliwa.
- Njia ya malipo: njia za malipo zina masharti ya kiasi cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa ambacho kinatumika kwa kila hatua ya kuweka pesa; sio tu kwa kuweka pesa kwa mara ya kwanza.
Kiasi cha pesa unachoweka kwa mara ya kwanza kinapaswa kuendana na kipengele cha juu zaidi kati ya hivi viwili.
Kwa mfano, ikiwa akaunti ya Pro inahitaji kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza cha USD 200 nayo njia ya malipo ina kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa cha USD 10, pesa utakazoweka kwa mara ya kwanza zinapaswa kuwa angalau USD 200.
Ujumbe wa hitilafu utaonekana kwenye Eneo lako la Binafsi ili kukuarifu ikiwa pesa ulizoweka ziko chini ya kiasi kinachohitajika kwa njia hiyo ya malipo.
Biashara imezuiwa kwenye akaunti za real zilizofunguliwa hivi majuzi hadi masharti ya kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza yatimizwe. Utaona ujumbe wa hitilafu ya ‘trading disabled’ au kitufe cha Order mpya hakitafanya kazi ukijaribu kufungua order kwenye jukwaa la biashara kabla ya kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu njia za malipo zinazopatikana na kutazama maktaba yetu ya video zenye maelezo, tembelea sehemu ya mifumo ya malipo.
Kwa taarifa zaidi kuhusu uwekaji wa pesa kwa ujumla, fuata kiungo cha makala yetu kuhusu uwekaji wa pesa.
Comments
0 comments
Article is closed for comments.