Unahitajika kufanikiwa kuweka pesa kwa mara ya kwanza kabla ya kuanza kutrade. Katika Exness, tunatoa aina mbalimbali za njia za malipo za kuweka pesa kwa urahisi kutoka sehemu yoyote ya dunia. Malipo yanakubaliwa kutoka kwa akaunti zilizosajiliwa kwa jina la mteja pekee, kwa hivyo akaunti za wahusika wengine hazikubaliwi.
Kumbuka: Wateja kutoka Afrika Kusini, Kenya na Vietnam wanahitajika kuthibitisha wasifu wao kikamilifu kabla ya kuweka pesa.
Jinsi ya kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB) na ubofye kwenye kichupo cha Uwekaji pesa.
- Chagua njia ya malipo, ukizingatia vikomo vya chini na vya juu zaidi, na muda wa uchakataji.
- Weka kiasi ambacho ungependa kuweka na ubofye Endelea.
- Angalia maelezo katika muhtasari uliowasilishwa na Uthibitishe.
- Utaelekezwa kwenye ukurasa wa njia ya malipo ili kukamilisha transaction hiyo.
Ni vyema kujua
Kabla ya kuweka pesa zako, kuna mambo machache ya kukumbuka:
Njia ya malipo
Kwa njia rahisi zaidi ya kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza, angalia njia za malipo zinazopatikana katika eneo lako. Utapata njia, muda wake wa uchakataji na vikomo vya chini/juu zaidi vinavyoonyeshwa kwenye kichupo cha Uwekaji pesa cha EB.
Wakati wa kuchagua njia ya malipo, zingatia:
- Masharti ya uthibitishaji - Hakikisha kuwa umekamilisha wasifu wako wa mteja kiuchumi na uthibitishaji wa akaunti ili kuwezesha njia zote za malipo.
- Sarafu - Weka pesa katika sarafu sawa na ile uliyoweka kwenye akaunti yako ya kutrade ili kuepuka gharama za ubadilishaji. Kumbuka kuwa sarafu ya akaunti ya kutrade haiwezi kubadilishwa baada ya akaunti ya kutrade kufunguliwa.
Kidokezo: Unaweza kufungua akaunti mpya za kutrade ikiwa unahitaji akaunti yenye sarafu maalum.
- Muda wa uchakataji - Muda wa uchakataji hutofautiana, kwa hivyo uthibitishe kabla ya kuchagua njia ya malipo.
- Ada za uwekaji pesa - Njia nyingi za malipo hazitozi ada za uwekaji pesa lakini zinaweza kuwa na kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa.
Tunapendekeza usome zaidi kuhusu njia za malipo zinazopatikana na kuhusu transactions za akaunti ya kutrade.
Kiasi cha pesa
Kiasi unachoweza kuweka kwa mara ya kwanza hutegemea akaunti ya kutrade uliyo nayo na njia ya malipo uliyochagua.
-
Aina ya akaunti
- Akaunti za Kitaaluma huwa na kiasi chao cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza kulingana na eneo lililosajiliwa, lakini sharti hili hutumika kwa kuweka pesa kwa mara ya kwanza pekee.
- Akaunti za standard zinahitaji kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza kinacholingana na njia ya malipo iliyochaguliwa.
-
Njia ya malipo
- Njia za malipo huwa na sharti la kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa linalotumiwa kwa kila hatua ya uwekaji pesa; si tu kwa kuweka pesa kwa mara ya kwanza.
Kiasi cha pesa unachoweza kuweka kwa mara ya kwanza kinapaswa kutoshana na kiasi cha juu zaidi kati ya hivi viwili.
Mfano
Ikiwa akaunti ya Pro inahitaji kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza cha USD 200 ilhali njia ya malipo ina kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa cha USD 10, kiasi cha pesa unachoweka kwa mara ya kwanza kinapaswa kuwa angalau USD 200.
Ujumbe wa hitilafu utaonekana kwenye EB lako ili kukuarifu kama kiasi cha pesa unachoweka ni kidogo kuliko kiasi kinachohitajika kwa njia hiyo ya malipo.
Biashara huwa imezuiwa kwenye akaunti za real zilizofunguliwa hivi majuzi hadi masharti ya kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza yatimizwe. Utaona ujumbe wa hitilafu ya ‘trading disabled’ au kitufe cha Order Mpya hakitafanya kazi ukijaribu kufungua order kwenye jukwaa la biashara kabla ya kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza.