Hongera, umefikia Hatua ya 5! Umeweka amana yako ya kwanza na umeweka vituo vyako vya biashara pia. Kinachobaki kufanya ni kuweka biashara yako ya kwanza. Tuanze:
- Ingia kwenye kituo
- Ongeza zana za biashara
- Kokotoa kiasi halisi
- Angalia saa za soko
- Fungua biashara
- Funga biashara
Ingia kwenye kituo
Ongeza zana za biashara
Je! una alama unazopendelea ambazo ungependa kufanya biashara, kama vile EURUSD? Fuata hatua hizi ili kubinafsisha orodha ya alama katika dirisha lako la Taarifa za Soko katika Kituo cha Wavuti au Kituo cha Kompyuta ya Mezani:
- Bofya kulia popote kwenye dirisha la Taarifa za Soko.
- Bofya Alama, kisha uchague kundi la zana za biashara ambazo ungependa kutazama.
- Chagua zana ya kufanya biashara na ubofye Onyesha (au Onyesha zote ikiwa ungependa kuongeza zana zote zinazopatikana), kisha ufunge dirisha.
Zana ya biashara uliyochagua sasa itaonyeshwa kwenye dirisha la Taarifa za Soko. Ikiwa ungependa kutazama chati ya ishara uliyoongeza, iburute kwenye dirisha la chati.
Jifunze jinsi ya kuongeza zana kwenye iOS na Android.
Kokotoa kiasi halisi
Kiasi halisi ni kiasi cha pesa kilichohifadhiwa ili kufungua na kudumisha nafasi ya biashara ya mkopo. Daima hakikisha una pesa za kutosha kwenye akaunti yako ili kufungua biashara.
Ili kuhesabu kiasi halisi kinachohitajika ili kufungua nafasi, tumia Kikokotoo cha Uwekezaji.
Angalia saa za soko
Kabla ya kufanya biashara yako ya kwanza, hakikisha kuwa unaelewa ni lini masoko ya kifedha duniani yanafunguliwa na kufungwa, na lini unaweza kufanya biashara.
Fungua biashara
Ili kufanya biashara kwenye Kituo cha Kompyuta ya Mezani au Kituo cha Wavuti:
- Bofya kulia popote kwenye Kichupo cha Biashara na uchague Agizo Jipya.
- Jaza sehemu zinazohitajika:
- Alama: Chagua alama ya biashara kutoka kwenye orodha kunjuzi, ambayo inaonyesha alama ambazo umeongeza kwenye dirisha lako la Taarifa za Soko.
- Aina ya agizo: Chagua Utekelezaji wa Soko au Agizo Linalosubiri. Akaunti za Kitaalamu zinaweza kufikia Utekelezaji wa Papo hapo pia.
- Kiasi: Andika ukubwa wa idadi (kiasi unachotaka kufanya biashara) kwa agizo lako. Ukubwa wa chini na juu zaidi wa idadi unategemea aina ya akaunti yako. Bofya hapa kusoma zaidi.
- Aina ya Biashara: Chagua Nunua au Uza unavyotaka.
Utaweza kufuatilia maendeleo ya biashara yako katika dirisha la Kituo.
Funga Biashara
Kuna njia mbili za kufunga biashara wazi kwenye Kituo cha Kompyuta ya Mezani au Kituo cha Wavuti:
- Bofya X kwenye biashara wazi iliyoko upande wa kulia wa Kichupo cha Biashara
- Bofya kulia kwenye biashara wazi katika Kichupo cha Biashara, na ubofye Funga Agizo.
Kipengele cha kufunga nafasi zote ni kipengele kinachopatikana kwa watumiaji wetu wa Kituo cha Exness pekee. Kipengele hiki hukuruhusu kufunga maagizo yote yaliyo wazi kwa mbofyo mmoja tu kwa kubofya kitufe cha Close all positions kilicho katika kona ya juu kulia mwa kituo cha biashara.
Unaweza pia kufunga sehemu fulani ya biashara - kufunga sehemu fulani ya kiasi cha biashara na kuacha nyingine wazi. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufunga sehemu fulani ya agizo kwenye vituo mbalimbali vya biashara vinavyopatikana, kwa kurejelea makala yetu ya kina.
Tafadhali kumbuka: kufunga biashara hakutafanyika kiotomatiki, isipokuwa ikiwa ni agizo ambalo linasubiri au komesha.
Ikiwa huwezi kufunga biashara kama ilivyoelezwa hapo juu, tafadhali fuata kiungo hiki ili kujua zaidi kuhusu kwa nini huwezi kufunga biashara.
Ni hayo tu! Sasa unajua jinsi ya kufanya biashara ya ubadilishanaji wa sarafu kwenye MetaTrader 4 au MetaTrader 5. Rejelea sehemu ya Vituo kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia vituo vya biashara.