Uwekaji na utoaji wa pesa unaofanya kutumia kadi yako ya malipo au ya mkopo ni njia rahisi ya kuweka funds katika akaunti yako ya kutrade, lakini kuna baadhi ya mambo muhimu ya kukumbuka unapofanya miamala ukitumia kadi ya benki.
Tafadhali kumbuka kuwa kadi zifuatazo za benki zinakubaliwa na zitatumika kwa miamala ya USD, EUR, na JPY (kwa JCB pekee):
- VISA na VISA Electron
- Mastercard
- Maestro Master
- JCB (Japan Credit Bureau)*
*Kadi ya JCB ndiyo kadi pekee ya benki inayokubaliwa nchini Japani; kadi zingine za benki haziwezi kutumika. Zingatia masharti maalum ya utoaji wa faida katika kiungo hiki.
Muhimu: Kadi za benki hazipatikani kwa akaunti zilizosajiliwa nchini Kongo, Liberia, Myanmar, Serbia, Sierra Leone, Somalia na Thailandi.
Kuweka pesa
Sehemu hii inaangazia taarifa zaidi kuhusu mada hizi:
- Jinsi ya kuweka pesa kwa kutumia kadi ya benki
- Ukaguzi wa jina la mwenye kadi
- Muda na ada za uchakataji wa uwekaji wa pesa
Kusimamia kadi za benki
Kadi yoyote ya benki inayotumiwa kuweka pesa huhifadhiwa kiotomatiki kama option ya uwekaji na utoaji wa pesa zaidi.
Jinsi ya kuweka pesa kwa kutumia kadi ya benki
Kabla ya kuweka pesa zako kwa mara ya kwanza ukitumia kadi ya benki, unahitaji kuthibitisha wasifu wako kikamilifu
Kiasi cha chini zaidi cha pesa unachoweza kuweka ukitumia kadi ya benki ni USD 10 na kiasi cha juu zaidi ni USD 10 000 kwa kila transaction, au kiasi sawa kwenye sarafu ya akaunti yako.
Kwa kadi mpya za benki
- Kwenye Eneo lako la Binafsi la Exness, bofya kichupo cha Deposit.
- Chagua Bank Card.
- Kisha, chagua akaunti ya kutrade ya kuweka pesa, sarafu na kiasi cha pesa unachoweka. Bofya Continue.
- Jaza fomu kwa taarifa za kadi ya benki kama vile nambari ya kadi yako ya benki, jina la mwenye kadi, tarehe ya mwisho ya matumizi na msimbo wa CVV. Bofya Continue.
- Kisha, muhtasari wa transaction utaonyeshwa. Bofya Confirm.
- Ujumbe utaonekana ili kuthibitisha kuwa transaction ya kuweka pesa imekamilika.
Katika hali nyingine, kutakuwa na hatua ya ziada ya kuweka OTP inayohitajika na benki yako kabla ya kukamilisha transaction ya kuweka pesa.
Ukaguaji wa jina la mwenye kadi
Unapoongeza kadi ya benki kwa transactions zako, kuna kanuni chache za kuzingatia wakati wa kuweka jina la mwenye kadi. Hii ni kuhakikisha kuwa transactions zinachakatwa vizuri.
- Jina la mwenye kadi linapaswa kuandikwa kwa herufi za Kiingereza pekee.
- Maneno ambayo hayaruhusiwi ni BANK, VISA, MASTER, MAESTRO, CARD, MOMENT, TEST, PAYMENT, GOLD, NAME, MC, INSTANT, EXPRESS, HOLDER, DEPOSIT, DEBIT, CREDIT, na UNIVERSAL.
- Maneno matatu yanaruhusiwa na yanaweza kujumuisha alama moja
- Sharti kuwe na angalau nafasi moja kati ya maneno ambayo yanapaswa kuwepo.
- Alama moja maalum inaruhusiwa:
- ‘ (alama moja ya kundondoa)
- ` (alama ya nyuma ya kundondoa)
- ~ (tilde)
- . (nukta)
- - (kistariungio)
- Idadi ya juu zaidi ya herufi, ikiwa ni pamoja na alama na nafasi, ni herufi 27.
- Alama ya dashi “-” inatambuliwa kama kitoa kikomo kati ya maneno.
Ikiwa mojawapo ya kanuni haijatimizwa, ujumbe wa hitilafu utaonyeshwa chini ya sehemu ya jina la mmiliki wa kadi.
Kwa kadi za benki zilizopo
- Bofya kichupo cha Deposit kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Chagua Bank Card..
- Chagua kadi ya benki iliyopo kutoka kwenye menyu kunjuzi na uweke msimbo husika wa CVV.
- Chagua akaunti ya kutrade ya kuweka pesa, sarafu na kiasi cha pesa unachoweka. Bofya Continue.
- Kisha, muhtasari wa transaction utaonyeshwa. Bofya Confirm.
- Ujumbe utaonekana kuthibitisha kwamba shughuli ya kuweka pesa imekamilika.
Wakati na ada za uchakataji wa kuweka pesa
Ada za uchakataji wa kuweka pesa | Bila malipo |
Wakati wa uchakataji wa kuweka pesa |
Wastani: Papo hapo** Muda wa juu zaidi: hadi siku 5 |
**Neno “instant” linaonyesha kuwa transaction inafanywa ndani ya sekunde chache bila kuchakatwa na wataalamu wetu wa idara ya fedha. Hata hivyo, hii sio hakikisho kuwa transaction itakamilika mara moja, lakini kwamba mchakato huanzishwa papo hapo.
Kumbuka: Vikomo vilivyobainishwa hapo juu ni kwa kila transaction isipokuwa inapobainishwa vinginevyo. Tafadhali rejelea Eneo lako la Binafsi kwa taarifa mpya zaidi.
Kutoa pesa
Sehemu hii ina taarifa zaidi kuhusu mada zifuatazo:
- Kanuni za utoaji wa pesa za Exness
- Utoaji wa pesa sawia na njia ya malipo
- Jinsi ya kutuma ombi la refund
- Kadi za benki ambazo muda wake umepita
- Kadi za benki zilizopotea au zilizoibwa
- Muda na ada za uchakataji wa utoaji wa pesa
Sheria za kutoa pesa za Exness
Kulingana na kanuni za utoaji wa pesa ya Exness, funds na faida zilizowekwa sharti zitolewe kupitia njia tofauti.
Utoaji wa pesa sharti ufuate kipaumbele cha mfumo wa malipo ili kuboresha muda wa transaction; toa funds kwa kutumia utaratibu huu:
- Refund kwenye kadi ya benki
- Refund ya Bitcoin
- Utoaji wa faida, kwa kuzingatia uwiano wa kuweka na kutoa pesa.
Utoaji wa pesa zilizowekwa unajulikana kama ombi la refund, ilhali utoaji wa faida kutoka kwa akaunti yako ya kutrade ni operesheni yake yenyewe.
Ni mara tu ombi la refund litakapochakatwa na kukamilika ndipo utaweza kutoa faida kwenye kadi yako ya benki, isipokuwa ukisubiri siku 90 za kazi kuanzia tarehe uliyoweka pesa. Pia, refunds zinaweza kufanywa kwa sehemu hadi masharti ya refund yatimizwe, hii inajulikana kama ombi la refund ya sehemu.
Utoaji wa uwiano wa njia ya malipo
Utoaji wa pesa sharti ufanywe kwa kutumia mfumo sawa wa malipo, akaunti sawa na sarafu ile ile iliyotumika kwa transaction ya uwekaji wa pesa.
Iwapo umetumia idadi ya kadi tofauti za benki na/au njia za malipo kuweka funds kwenye akaunti yako ya kutrade, basi utoaji wa pesa sharti ufanywe kwenye akaunti hizo za benki na/au njia za malipo kwa uwiano sawa na pesa zilivyowekwa.
Huu hapa ni mfano wa kukusaidia kuelewa hili vyema:
Umeweka jumla ya USD 1,000 kwenye akaunti yako ya kutrade.
- USD 500 ukitumia Kadi ya A
- USD 300 ukitumia Kadi ya B
- USD 200 ukitumia Neteller
Kulingana na hali hili, utaruhusiwa tu kutoa jumla ya kiasi kulingana na uwiano huu:
- 50% ya utoaji wa pesa ukitumia Kadi ya A
- 30% ya utoaji wa pesa ukitumia Kadi ya B
- 20% ya utoaji wa pesa ukitumia Neteller
Sasa, hebu tuchukulie kuwa umepata faida ya USD 500 na ungependa kutoa pesa zote, ikiwa ni pamoja na faida.
Kwa mujibu wa kanuni ya uwiano, hapa kuna vikomo vya juu zaidi kwa kila njia ya utoaji:
- Kadi A - USD 750
- USD 500 zitafanyiwa refund kwanza, kisha USD 250 kama utoaji wa faida
- Kadi ya B - USD 450
- USD 300 zitafanyiwa refund kwanza, kisha USD 150 kama utoaji wa faida
- Neteller - USD 300
Kumbuka kuwa utoaji wa faida unapatikana tu mara tu masharti ya refund yanapofikiwa. Hii itaonyeshwa katika Eneo lako la Binafsi unapotoa pesa. Unaweza kupata maelezo kwa kina kuhusu hili katika makala yetu kwenye kila kitu unachohitaji kujua kuhusu utoaji wa pesa.
Kuhusu maombi ya refund
Ombi la refund ni utoaji wa funds zilizowekwa na sharti likamilishwe kabla ya kutolewa kwa faida kutoka kwa akaunti ya kutrade. Kiasi cha refunds kupitia kadi za benki hakiwezi kuwa kikubwa kuliko kilichowekwa na sharti kitimize masharti ya refund yaliyoonyeshwa katika Eneo lako la Binafsi unapotuma ombi la refund.
Maombi mengine ya refunds kwa sehemu ni wakati maombi ya refunds yanafanywa kwa kiasi kidogo badala ya jumla ya kiasi cha funds kilichowekwa.
Kumbuka: Ikiwa maombi ya refund kwa sehemu hayapatikani katika eneo lako, itabidi utume ombi la refund kamili kulingana na kanuni za kipaumbele za mfumo wa malipo kabla ya kutoa faida.
Jinsi ya kutuma ombi la refund
- Chagua Bank Card kutoka sehemu ya Withdrawal ya EB yako.
- Bofya Show my refunds kutoka ukurasa unaofuata.
- Chagua kadi ya benki ili ukamilishe refund.
- Katika ukurasa unaofuata, jaza fomu, ikijumuisha:
-
- Kuchagua kadi ya benki kama mbinu ya malipo.
- Chagua akaunti ya kutrade kurefund kutoka.
- Weka kiasi refund.
Bofya Continue.
- Muhtasari wa muamala utawasilishwa; bofya Confirm ili kuendelea.
- Weka nambari ya kuthibitisha iliyotumwa kwako kwa barua pepe au SMS (kulingana na aina ya usalama) ya Eneo lako la Binafsi, kisha ubofye Confirm.
- Ujumbe utathibitisha kuwa ombi la refund limekamilika.
Kadi za benki zilizoisha muda wake
Ikiwa muda wa kadi yako ya benki umeisha lakini umepewa kadi mpya ya benki kwa ajili ya akaunti hiyo hiyo ya benki, mchakato wa refund ni wa moja kwa moja; unahitaji tu kufuata hatua za kuomba refund kama kawaida.
Ikiwa kadi yako iliyoisha muda wake haijaunganishwa tena kwa akaunti ya benki kwa vile imefungwa kabisa, ni lazima uwasiliane na Timu ya Usaidizi na uthibitisho wa akaunti iliyofungwa ya benki. Timu ya Usaidizi inaweza kukuongoza kupitia ombi la refund, kwa kutumia njia zingine za malipo zinazopatikana au Mifumo ya Malipo ya Kielektroniki (EPS).
Kadi za benki zilizopotea au zilizoibiwa
Iwapo kadi ya benki imepotea au kuibiwa, tafadhali wasiliana na Timu ya Usaidizi ili upate uthibitisho na wanaweza kukusaidia kwa ombi lako la refund punde tu uthibitishaji wa akaunti utakapokamilika.
Jinsi ya kutoa faida
Kiasi cha chini zaidi unaweza kutoa kwenye kadi yako ya benki ni USD 0 kwa EB za wavuti na za kompyuta ya mezani na kwa programu ya Social Trading***, wakati utoaji wa faida ya juu zaidi ni USD 10 000 kwa kila transaction.
- Chagua Bank Card kwenye eneo la Withdrawal katika Eneo lako la Binafsi.
- Jaza fomu na taarifa zifuatazo:
a. Chagua kadi ya benki unayopendelea kutoka kwenye menyu kunjuzi.
b. Chagua akaunti ya kutrade utakatoa kutoka.
c. Weka kiasi cha pesa unachotoa katika sarafu ya akaunti yako.
- Bofya Continue.
- Muhtasari wa transaction utawasilishwa; bofya Confirm ili kuendelea.
- Weka nambari ya uthibitishaji uliyotumiwa kupitia barua pepe au SMS (kulingana na aina yako ya usalama), kisha ubofye Confirm.
- Ujumbe utathibitisha kuwa ombi la refund limekamilika.
Tafadhali kumbuka kuwa utoaji wa faida ukitumia kadi za benki nchini Japani na Korea Kusini haukubaliki. Tafadhali kumbuka kutoa faida kupitia njia tofauti ya malipo.
Utoaji wa faida haupatikani nchini Pakistan, India na Botswana. Wateja kutoka nchi hizi wanaweza kufanya refund kwa kadi zao za benki, lakini utoaji wa faida sharti ufanywe kupitia njia yoyote ya malipo inayopatikana katika EB.
Muda na ada za uchakataji wa kutoa pesa
Transaction | Muda wa Uchakataji | Ada za uchakataji |
---|---|---|
Maombi ya refund na utoaji wa faida | Hadi siku 10 za kazi | Bila malipo |
***Social trading haipatikani kwa wateja waliosajiliwa na huluki yetu ya Kenya.