Eneo la Binafsi, ambalo mara nyingi hujulikana kama EB, ndilo kituo kikuu cha usimamizi wa akaunti. EB hufunguliwa akaunti ya Exness inaposajiliwa.
Ili uingie kwenye akaunti ya biashara:
- Tembelea Tovuti ya Exness.
- Bofya Ingia.
- Weka anwani yako ya barua pepe iliyosajiliwa ya Exness, na Nenosiri la akaunti ya Exness.
- Bofya Endelea ili kuingia.
- Eneo la Binafsi: Menyu ya vipengele
- Eneo la Binafsi: Akaunti zangu
- Eneo la Binafsi: Uwekaji pesa
- Eneo la Binafsi: Utoaji pesa
- Eneo la Binafsi: Historia ya transaction
- Eneo la Binafsi: Uchanganuzi
- Eneo la Binafsi: Usimamizi wa Portfolio
- Eneo la Binafsi: Social Trading
- Eneo la Binafsi: Utendaji
- Eneo la Binafsi: Mipangilio
- Eneo la Binafsi: Usaidizi wa Exness
Eneo la Binafsi: Menyu ya vipengele
Menyu ya vipengele inapatikana kwenye sehemu ya juu ya Eneo lako la Binafsi (EB) na inajumuisha vipengele kadhaa muhimu:
- Salio
- Jumla ya free margin ya akaunti zote za kutrade. Bofya ili kuonyesha akaunti zako. Bofya Hamisha au Toa ili kuanzisha transactions hizi kutoka kwa kichupo cha Utoaji fedha.
- Lugha
- Huonyesha lugha iliyochaguliwa ndani ya EB.
- Taarifa
- Viungo vya nyenzo, ikiwa ni pamoja na Zana & Huduma, Biashara na Usaidizi.
- Menyu ya gridi
- Viungo ambavyo vitakuelekeza kwenye vipengele na huduma zinazopatikana za Exness, kama vile Terminali ya Exness.
- Arifa
- Arifa za akaunti zinazoweza kuchaguliwa ambazo zinaweza kukuelekeza upya kwenye sehemu inayohusiana ya EB lako.
- Wasifu
- Jina lako na sehemu ya anwani yako ya barua pepe iliyosajiliwa huonyeshwa hapa. Kubofya Mipangilio kutafungua mipangilio ya wasifu wako, huku kubofya Masharti ya Biashara kukiorodhesha vipengele vinavyotumika vya biashara vya akaunti hii.
Eneo la Binafsi: Akaunti zangu
Kichupo cha Akaunti zangu katika Eneo lako la Binafsi (EB) huwa na akaunti zote za kutrade zilizofunguliwa. Akaunti zako za kutrade huwa zimepangwa katika vichupo vitatu:
- Real
- Akaunti zinazotumika za kutrade zinazotumia funds halisi.
- Demo
- Akaunti za demo zinazotumika zinazotumia funds pepe.
- Imehifadhiwa kwenye kumbukumbu
- Akaunti real za kutrade ambazo zimehifadhiwa kwenye kumbukumbu.
Ili kufungua akaunti mpya ya kutrade, bofya + Fungua Akaunti Mpya. Unaweza kupanga akaunti hizi kulingana na mpya zaidi, ya awali zaidi, free margin au jina la utani kialfabeti na hata kuchagua kuonyesha akaunti zako katika mwonekano wa orodha au wa gridi.
Kadi za akaunti ya kutrade
Kila akaunti ya kutrade huonyeshwa kama kadi yenye maelezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na:
- Akaunti: Real au Demo
- Jukwaa la Akaunti:MT4 au MT5
- Aina ya akaunti: Standard, Standard Cent, Pro, Raw Spread au Zero
- Jina la utani: Jina chaguo-msingi au la utani lilioundwa la akaunti hii.
- Nambari ya akaunti: Nambari zinazowakilisha akaunti ya kutrade (zinazotumika kama maelezo ya kuingia kwenye majukwaa ya biashara)
Bofya aikoni ya nukta tatu ili kuonyesha options za akaunti ya kutrade, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuhamisha funds, kubadilisha leverage ya juu zaidi, kubadilisha jina la akaunti, kutazama taarifa zako za akaunti, kuweka ufikiaji wa kusoma pekee kwa akaunti yako ya kutrade, kudhibiti taarifa zako, kubadilisha nenosiri la biashara na kuhifadhi akaunti kwenye kumbukumbu.
Eneo la Binafsi: Uwekaji pesa
Kichupo cha Uwekaji pesa huonyesha njia za malipo zinazopatikana kwa akaunti zako za kutrade na pochi ya uwekezaji kulingana na eneo lililosajiliwa. Kila njia ya malipo huonyesha muda wake wa uchakataji uliokadiriwa, ada na kiasi cha juu/chini zaidi cha pesa unachoweza kuweka.
Lebo ya Inapendekezwa inamaanisha kuwa njia hii ina kiwango cha juu ya mafanikio katika eneo lako lililosajiliwa. Baadhi ya njia za malipo zinaweza kuwa nje ya mtandao kwa ajili ya matengenezo ya kawaida, kwa hivyo thibitisha upatikanaji wa sasa katika EB. Njia za uwekaji fedha zilizofanikiwa huonyeshwa chini ya Njia zangu zilizohifadhiwa.
Njia zangu zilizohifadhiwa
Njia za uwekaji pesa zilizohifadhiwa huwa na nambari ya akaunti ya kutrade, jina kamili na sarafu ya akaunti. Ili kuondoa njia iliyohifadhiwa, bofya menyu ya nukta 3 na uchague Futa.
Sio njia zote zilizohifadhiwa zitakuwa na option ya kufutwa na njia zilizofutwa haziwezi kurejeshwa isipokuwa ikiwa zimetumika tena.
Eneo la Binafsi: Utoaji pesa
Kichupo cha Utoaji pesa huonyesha njia za utoaji pesa za akaunti zako za kutrade na pochi ya uwekezaji kulingana na eneo lililosajiliwa. Kila njia ya utoaji fedha huonyesha muda uliokadiriwa wa uchakataji, ada, na kiwango cha chini/juu zaidi cha pesa zinazoweza kutolewa.
Lebo ya Inapendekezwa inamaanisha kuwa njia hii ina kiwango cha juu ya mafanikio katika eneo lako lililosajiliwa.
Ikiwa refunds zozote za kadi ya benki zinazosubiri zitafanywa, zitaonyeshwa kwenye sehemu ya juu ya eneo hili. Njia zilizotumika za utoaji fedha zitaonyeshwa chini ya Njia zangu zilizohifadhiwa.
Njia zangu zilizohifadhiwa
Njia za utoaji pesa zilizohifadhiwa tayari zina nambari ya akaunti ya kutrade, jina kamili na sarafu ya akaunti zilizowekwa. Ili kuondoa njia iliyohifadhiwa, bofya menyu ya nukta 3 na uchague Futa.
Sio njia zote zilizohifadhiwa zitakuwa na option ya kufutwa na njia zilizofutwa haziwezi kurejeshwa isipokuwa ikiwa zimetumika tena.
Uhamisho wa ndani
Ili kuhamisha funds kati ya akaunti za kutrade au kutoka kwa akaunti ya kutrade katika Eneo lako la Binafsi hadi kwa akaunti ya kutrade katika Eneo tofauti la Binafsi, chagua kutoka kwa options zifuatazo chini ya kichupo cha Utoaji pesa:
- Kati ya akaunti zako: Kati ya akaunti za kutrade katika EB sawa.
- Kwa mtumiaji mwingine: Hadi kwa akaunti ya kutrade katika EB tofauti.
Ili kuhamisha funds hadi kwa akaunti ya kutrade katika EB tofauti, utahitaji nambari ya akaunti ya kutrade na anwani ya barua pepe iliyosajiliwa ya mtumiaji huyo au uhamishaji huo hautakamilika.
Eneo la Binafsi: Historia ya transaction
Kichupo cha Historia ya transaction kitaorodhesha kila transaction ambayo inafanywa katika Eneo lako la Binafsi, ikiwa ni pamoja na:
- Uwekaji fedha
- Kutoa pesa
- Uhamishaji
- Refunds: Refunds za kadi ya benki zinapatikana hapa.
- Zawadi: Ada inayotozwa kwa baadhi ya aina za akaunti (Raw Spread, Zero).
- Rebates: Malipo yanayochakatwa kupitia mfumo wa rebates.
Kubofya kipengele chochote katika historia ya transaction huonyesha muhtasari wa transaction, ikiwa ni pamoja na kitambulisho cha ankara na muda wa transaction kwa kina. Bofya Pata usaidizi ili kuongeza maombi ya usaidizi kwa transactions zako zinazohusiana na malipo.
Hali ya aina ya transaction inaweza kuonyeshwa kama:
- Imekamilika: transaction hiyo imekamilika.
- Inachakatwa: transaction hiyo bado haijakamilika.
- Imekataliwa: transaction hiyo imeghairiwa (sababu inaweza kutofautiana).
Eneo la Binafsi: Uchanganuzi
Kichupo cha Uchanganuzi kwenye Eneo lako la Binafsi(EB) huwa na habari na uchanganuzi wa soko na uliotolewa na Trading Central katika Analyst News na FXStreet News katika Habari za Soko mtawalia. Hapa, kiungo cha Kalenda ya Kiuchumi inapatikana, ambapo matukio ambayo yanaweza kusababisha vipindi vya masharti ya juu ya margin (HMR) yanakusanywa ili uweze kuyafikia kwa urahisi.
Habari za Mchanganuzi
Habari zinazopatikana hapa hutolewa na Trading Central na kutofautishwa na vikundi vya instruments za biashara. Kubofya hadithi yoyote kutafungua maudhui yake upande wa kulia wa kipengele hiki.
Unaweza kupanga habari hizi kwa kuchuja zana kama vile mawazo, timeframe na trends. Upau wa kutafutia unaweza pia kutumika kupata habari.
Taarifa za Soko
FXStreet News huratibu makala ya habari za sasa na zinazovuma zinazohusiana na biashara. Lebo zinaweza kutumika kuchuja makala yanayoonyeshwa na kubofya makala kutayafungua.
Eneo la Binafsi: Usimamizi wa Portfolio
Kichupo cha Usimamizi wa Portfolio katika Eneo lako la Binafsi (PA) huruhusu traders kujisajili ili kuwa Wasimamizi wa Portfolio ambao wanaweza kuunda mtandao na Wawekezaji wao, kudhibiti funds zao, kuweka ada maalum za utendaji na kufurahia kutotozwa ada za jukwaa. Kichupo huonyeshwa tu ikiwa Usimamizi wa Portfolio unapatikana katika eneo lako.
Eneo la Binafsi: Social Trading
Kichupo cha Social Trading katika Eneo lako la Binafsi (EB) ni jukwaa la usimamizi kwa watoa mkakati na wawekezaji. Mikakati inaweza kuundwa na kudhibitiwa na wawekezaji wanaweza pia kufuatilia uwekezaji wao katika mkakati.
Kichupo hiki huonyeshwa tu ikiwa Social Trading inatolewa katika eneo lako.
Eneo la Binafsi: Utendaji
Kichupo cha Utendaji katika Eneo lako la Binafsi (EB) hutoa muhtasari wa data iliyokusanywa kuhusu utendaji wako wa biashara. Unaweza kuona utendaji wa jumla wa Eneo lako la Binafsi (akaunti zote za kutrade) au uchague kutoka kwa akaunti zako zinazotumika za kutrade. Huwa kimegawanywa katika:
- Muhtasari
- Unaweza kuona utendaji wako wa jumla wa biashara kwa akaunti zote au uchague akaunti mahususi ya kutrade na timeframe kwenye menyu kunjuzi. Pointi kadhaa za data na chati zitatolewa, zikiwemo:
- Faida halisi
- Orders zilizofungwa
- Kiasi cha biashara
- Equity
Kumbuka: Takwimu za wakati halisi zinapatikana katika jukwaa lako la biashara; ni orders zilizofungwa pekee ndizo zitaonyeshwa kwenye chati.
- Historia ya maagizo
- Unaweza kutazama historia ya kina ya order ya akaunti ya kutrade kwa Orders zilizofungwa na Orders zilizofunguliwa, pamoja na kipindi cha muda na kupakua faili ya maandishi ya historia ya order ya uteuzi wa sasa kwa kubofya Pakua CSV.
- Bofya order mahususi iliyofungwa ili kutazama maelezo yake. Jinsi order inavyofungwa huonyeshwa chini ya Imefungwa kwa na hujumuisha muhtasari wa stop-out ikiwa order hiyo ilifungwa kutokana na stop-out.
- Faida za Exness
- Ikiwa inapatikana katika eneo lako, kichupo hiki huorodhesha mafao ya Exness pekee ambayo yamelinda funds za akaunti yako ya kutrade, kama vile:
- Ulinzi dhidi ya Stop out
- Ulinzi wa salio hasi
- Swap-free
Eneo la Binafsi: Mipangilio
Katika Eneo lako la Binafsi (EB), vipengele muhimu vya udhibiti wa akaunti chini ya Mipangilio vinajumuisha:
- Wasifu
- Taarifa zako za kibinafsi zilizosajiliwa, hali ya uthibitishaji na kikomo cha kiasi cha pesa kinachoweza kuwekwa huonyeshwa hapa.
- Mshirika Wangu
- Kwa traders walioalikwa na Mshirika, unaweza kudhibiti maelezo yako ya mawasiliano yaliyoshirikiwa na Mshirika wako katika sehemu hii. Ikiwa umekubali ombi la mshirika wako la kushiriki maelezo ya mawasiliano, unaweza kuona barua pepe yake na kubadilisha anwani ya barua pepe uliyoshiriki.
Kidokezo: Ili kuwa Mshirika, unaweza kuanza safari yako ya Programu ya Ushirikiano ya Exness kwa kubofya Alika Rafiki na upate pesa kwenye menyu ya vichupo.
- Mipangilio ya usalama
- Uidhinishaji unajumuisha maelezo yako ya kuingia katika akaunti ya Exness na option ya kubadilisha nenosiri lako. Uthibitishaji wa hatua 2 ni aina yako ya usalama na unaweza pia kuondoka kwenye vifaa vingine ili kulinda akaunti yako.
- Terminali za biashara
- Jukwaa chaguomsingi ambalo akaunti zako za kutrade za MT4 na MT5 zinatumia linaweza kuwekwa hapa. Options ni pamoja na:
- Kituo cha Exness
- Metatrader 4 au 5
- MT4 au MT5 WebTerminal
- Masharti ya biashara
- Hapa, hali ya masharti ya biashara yanayopatikana yanatumika kwa akaunti ya Exness, kama vile Ulinzi dhidi ya Salio Hasi, Ulinzi dhidi ya Stop Out, Viwango vya Zero Stop na Hali ya Swap-Free, huonyeshwa.
- Seva ya Kibinafsi ya Mtandaoni
- Unaweza kudhibiti au kutuma maombi ya huduma VPS ya Exness bila malipoikiwa unatimiza masharti fulani.
- Exness Premier
- Hali ya daraja na taarifa za wanachama wa Programu ya Exness Premier huonyeshwa katika sehemu hii.
Eneo la Binafsi: Usaidizi wa Exness
Kwenye Eneo lako la Binafsi (EB), sehemu ya chini kulia itaonyesha wijeti ya Mratibu wa Exness kila wakati.
Bofya aikoni ya usemi ili kupata usaidizi kutoka kwa chatiboti yetu ambayo hukuwa tayari kila wakati. Chatiboti inaweza kukusaidia kwa kazi nyingi muhimu zinazohusiana na akaunti yako ya Exness, kama vile biashara, transactions, n.k. Unaweza pia kutumia Mratibu wa Exness kuwasiliana na Usaidizi.