Eneo Binafsi lako ni sehemu moja ya shughuli zote zinazohusiana na Exness, ikijumuisha:
- Kuweka amana kwenye akaunti zako za biashara
- Kuunda akaunti mpya za biashara
- Kudhibiti mipangilio ya akaunti yako ya Exness
Na mengi zaidi; utapata kila kitu unachohitaji kufanya biashara na Exness katika Eneo Binafsi lako.
Tazama video hapa chini kwa ziara ya kuongozwa ya Eneo Binafsi la Exness:
Jinsi ya kuingia kwenye Eneo Binafsi lako:
Ili kuingia katika Eneo Binafsi lako, tembelea Exness.com na ubofye Ingia.
Utahitaji kutoa vitambulisho vifuatavyo ili kuingia:
- Anwani yako ya barua pepe: anwani ya barua pepe uliyosajili nayo akaunti yako ya Exness.
- Nenosiri la Akaunti ya Exness: uliloweka ulipounda Eneo Binafsi lako (halilingani na nenosiri lolote la akaunti ya biashara).
Je, unatatizika kuingia? Tazama mwongozo wetu wa utatuzi.