Ili kusajili akaunti ya Exness, unachohitaji ni anwani halali ya barua pepe na nambari ya simu inayofanya kazi kutoka nchi unakoishi iliyochaguliwa. Kuanza, utahitajika tu kuingiza barua pepe na nenosiri ili kuunda Eneo Binafsi lako; kuongeza nambari ya simu kwenye akaunti itafanyika baadaye.
Huenda unakabiliwa na mojawapo ya hitilafu zifuatazo ikiwa unakumbana na changamoto kusajili akaunti:
Barua pepe tayari imeunganishwa kwenye akaunti
Ikiwa unaona hitilafu hii, barua pepe hii tayari imetumika kujiandikisha na Exness na haiwezi kutumika tena.
Ili kurekebisha hii, unaweza:
- Jaribu kurejesha nenosiri lako la Eneo Binafsi kutoka hapa.
- Tumia anwani tofauti ya barua pepe kujiandikisha.
Weka barua pepe halali
Hakikisha umeingiza barua pepe yako kwa usahihi na ukamilifu bila nafasi zozote za ziada au vibambo ambavyo vinaweza kuwa vimeingizwa bila kukusudia.
Ikiwa unaona hitilafu hii, weka kipanya chako juu ya kosa ili kupata kidokezo juu ya nini hasa kinahitaji kubadilishwa/kurekebishwa.
Tunatumai makala haya yamekufaa. Tatizo hili likiendelea, usisite kuwasiliana na Timu yetu ya Usaidizi wa Exness kwa usaidizi zaidi.