Mifumo ya Malipo ya Kielektroniki (EPS) inapatikana kimataifa na hutumika kutuma na kupokea funds kwa urahisi kwa kuwa mchakato huu huokoa muda na ni rahisi sana kuutumia. Unaweza kuweka na kutoa pesa kwenye akaunti zako za kutrade kwa kutumia aina mbalimbali za EPS. Unachohitaji ni akaunti iliyosajiliwa kwa kutumia mfumo wa malipo wa kielektroniki ambao ungependa kutumia.
Ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu malipo kwa ujumla, soma makala yetu kwa kila kitu unachohitaji kujua.
- Neteller
- Skrill
- Perfect Money
- Sticpay
- Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Kumbuka: Ikiwa mojawapo ya njia hizi za malipo haipatikani, kwa sababu ya kutopatikana katika eneo hilo au kwa madhumuni ya matengenezo, tafadhali chagua njia nyingine ya malipo inayopatikana katika Eneo lako la Binafsi (EB).
Neteller
Neteller ni njia ya malipo ya kielektroniki maarufu kwa transactions za papo hapo na salama kote duniani. Unaweza kutumia njia hii ya malipo kuongeza pesa kwenye Akaunti yako ya Exness bila ada yoyote.
Haya ndiyo unahitaji kujua kuhusu Neteller:
Kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa | USD 10 |
Kiasi cha juu zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa | USD 50,000 kwa kila transaction |
Kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kutolewa | USD 4 |
Kiasi cha juu zaidi cha pesa kinachoweza kutolewa | USD 10,000 kwa kila transaction |
Ada za uchakataji wa uwekaji na Utoaji fedha | Bila malipo |
Muda wa uchakataji wa hatua za uwekaji fedha |
Wastani: Papo hapo* Muda wa juu zaidi: hadi dakika 30 |
Muda wa uchakataji wa hatua za utoaji fedha |
Wastani: Papo hapo* Muda wa juu zaidi: hadi siku 1 |
Kumbuka: Vikomo vilivyobainishwa hapo juu ni kwa kila transaction isipokuwa panapobainishwa vinginevyo.
*Neno "papo hapo" linamaanisha kuwa transaction itafanywa ndani ya sekunde chache bila uchakataji wa wataalamu wa idara yetu ya kifedha. Hii haihakikishi kuwa transaction itakamilika papo hapo, lakini kwamba mchakato umeanza mara moja.
Kuweka pesa kupitia Neteller
- Nenda kwenye sehemu ya Uwekaji fedha ya Eneo lako la Binafsi (EB), na ubofye Neteller.
- Kwenye dirisha ibukizi, chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kuongeza pesa, chagua sarafu ya uwekaji fedha, bainisha kiasi ambacho ungependa kuweka, na ubofye Inayofuata.
- Muhtasari wa transaction hiyo utaonyeshwa. Kagua data yote na ubofye Thibitisha malipo.
- Utaelekezwa kwenye tovuti ya Neteller ambapo utahitaji kuweka maelezo ya akaunti yako ya Neteller na ufuate vidokezo ili Kukamilisha Order.
- Kiasi kitatozwa kiotomatiki kutoka kwa akaunti yako ya Neteller.
- Funds zitaongezwa kwenye akaunti yako ya kutrade papo hapo.
Kutoa pesa kupitia Neteller
- Bofya Neteller kwenye sehemu ya Utoaji fedha ya Eneo lako la Binafsi (EB).
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kutoa funds, chagua sarafu yako ya utoaji fedha, weka anwani ya barua pepe ya akaunti yako ya Neteller, na ubainishe kiasi ambacho ungependa kutoa katika sarafu ya akaunti yako ya kutrade. Bofya Inayofuata.
Kumbuka: Anwani ya barua pepe inayotumiwa inapaswa kuwa sawa na ile iliyotumiwa wakati wa kuweka pesa kupitia Neteller.
- Muhtasari wa transaction hiyo utaonyeshwa. Weka msimbo wa uthibitishaji uliotumwa kwako kupitia barua pepe au SMS kulingana na aina ya usalama ya Eneo lako la Binafsi (EB). Bofya Thibitisha utoaji fedha
- Utapokea pesa zilizotolewa baada ya muda mfupi.
Skrill
Skrill ni njia maarufu sana ya malipo ya kielektroniki inayopatikana katika takriban nchi 200 kote duniani. Skrill inaweza kukusaidia kuhamisha pesa kati ya anuwai ya tovuti papo hapo na inaweza kutumika kuongeza pesa kwenye akaunti zako za kutrade za Exness bila ada.
Kumbuka: Mfumo huu wa malipo unaweza kuwa nje ya mtandao kwa ajili ya matengenezo kwa wakati wowote. Ikiwa njia hii ya malipo haipatikani, tafadhali chagua njia nyingine ya malipo inayopatikana kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
Kumbuka: Kwa sasa Skrill haipatikani kwa akaunti zilizosajiliwa katika baadhi ya maeneo. Tafadhali wasiliana na Usaidizi kwa taarifa zaidi kuhusu hili.
Haya ndiyo unahitaji kujua kuhusu Skrill:
Kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa | USD 10 |
Kiasi cha juu zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa | USD 100 000 kwa kila transaction |
Kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kutolewa | USD 10 |
Kiasi cha juu zaidi cha pesa kinachoweza kutolewa | USD 12 000 kwa kila transaction |
Ada za uchakataji wa uwekaji fedha | Bila malipo |
Ada za uchakataji wa hatua za utoaji fedha |
Chini ya USD 20: USD 1 Zaidi ya au sawa na USD 20: Bila malipo |
Muda wa uchakataji wa hatua za uwekaji fedha |
Wastani: Papo hapo* Muda wa juu zaidi: hadi dakika 30 |
Muda wa uchakataji wa hatua za utoaji fedha |
Wastani: Papo hapo* Muda wa juu zaidi: hadi siku 1 |
*Neno "papo hapo" linamaanisha kuwa transaction itafanywa ndani ya sekunde chache bila uchakataji wa wataalamu wa idara yetu ya kifedha. Hii haihakikishi kuwa transaction itakamilika papo hapo, lakini kwamba mchakato umeanza mara moja.
Kuweka pesa kupitia Skrill
- Chagua Skrill kwenye sehemu ya Utoaji fedha ya Eneo lako la Binafsi (EB).
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kuongeza pesa, pamoja na kiasi ambacho ungependa kuweka, na uchague sarafu, kisha ubofye Endelea.
- Muhtasari wa transaction huwasilishwa; bofya Thibitisha ili kuendelea.
- Utaelekezwa kwenye ukurasa wa tovuti wa Skrill ambapo:
a. Utaingia kwa kutumia maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako ya Skrill ili uweke eneo lako la mwanachama.
b. Utafungua akaunti mpya ya Skrill ili kufikia eneo lako la mwanachama. - Chagua njia yako ya malipo ndani ya tovuti ya Skrill na ufuate maagizo kwenye skrini.
- Hatua yako ya uwekaji fedha sasa imekamilika na funds zinapaswa kuonekana kwenye akaunti uliyochagua ya kutrade hivi karibuni.
Kutoa pesa kupitia Skrill
- Chagua Skrill kwenye sehemu ya Uwekaji fedha ya Eneo lako la Binafsi (EB).
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kutoa pesa, chagua sarafu yako utoaji fedha na kiasi ambacho ungependa kutoa, na uweke anwani ya barua pepe iliyosajiliwa ya akaunti yako ya Skrill. Bofya Endelea.
- Muhtasari wa transaction hiyo utaonyeshwa. Weka msimbo wa uthibitishaji uliotumwa kwa barua pepe au SMS yako kulingana na aina ya usalama ya Eneo lako la Binafsi (EB). Bofya Thibitisha.
- Hatua yako ya utoaji fedha sasa imekamilika.
Usaidizi kwa malipo ya Skrill
Ikiwa akaunti yako ya Skrill imezuiwa, tafadhali wasiliana na Usaidizi au ututumie barua pepe kwa support@exness.com ukiwa na uthibitisho kuwa akaunti imefungwa kwa muda usiojulikana. Idara yetu ya kifedha itakupa suluhu.
Perfect Money
Perfect Money ni njia ya malipo ya kielektroniki maarufu sana kote duniani. Unaweza kutumia njia hii ya malipo kuongeza pesa kwenye akaunti yako ya Exness.
Kumbuka: Perfect Money haipatikani kwa wateja waliosajiliwa na Huluki yetu ya Kenya, na kwa wateja nchini China na Vietnam.
- Kuweka pesa kwa kutumia Perfect Money
- Kutoa pesa kwa kutumia Perfect Money
- Je, ninawezaje kutoa pesa ikiwa akaunti yangu ya Perfect Money imezuiwa?
Haya ndiyo unahitaji kujua kuhusu Perfect Money:
Kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa | USD 10 |
Kiasi cha juu zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa | USD 100 000 kwa kila transaction |
Kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kutolewa | USD 2 |
Kiasi cha juu zaidi cha pesa kinachoweza kutolewa | USD 100 000 kwa kila transaction |
Ada za uchakataji wa uwekaji na Utoaji fedha | 0.5% |
Muda wa uchakataji wa hatua za uwekaji fedha |
Wastani: Papo hapo* Muda wa juu zaidi: hadi dakika 30 |
Muda wa uchakataji wa hatua za utoaji fedha |
Wastani: Papo hapo* Muda wa juu zaidi: hadi siku 1 |
Kumbuka: Vikomo vilivyobainishwa hapo juu ni kwa kila transaction isipokuwa panapobainishwa vinginevyo.
*Neno "papo hapo" linamaanisha kuwa transaction itafanywa ndani ya sekunde chache bila uchakataji wa wataalamu wa idara yetu ya kifedha. Hii haihakikishi kuwa transaction itakamilika papo hapo, lakini kwamba mchakato umeanza mara moja.
Kuweka pesa kwa kutumia Perfect Money
- Nenda kwenye sehemu ya Uwekaji fedha ya Eneo lako la Binafsi (EB), na ubofye Perfect Money.
- Kwenye dirisha ibukizi, chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kuongeza pesa, bainisha kiasi ambacho ungependa kuweka, na ubofye Inayofuata.
- Muhtasari wa transaction hiyo utaonyeshwa. Kagua data yote na ubofye Thibitisha malipo.
- Utaelekezwa kwenye tovuti ya Perfect Money.
- Chagua njia ya malipo ya Akaunti ya Perfect Money, na ubofye Fanya Malipo ili kukamilisha uhamishaji.
- Ukurasa utaonyesha kuwa transaction yako inaendelea.
- Ukishakamilisha transaction, funds zitawekwa kwenye akaunti yako ya Exness papo hapo.
Kutoa pesa wa kutumia Perfect Money
- Bonyeza Perfect Money kwenye sehemu ya Utoaji fedha ya Eneo lako la Binafsi (EB).
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kutoa funds, chagua sarafu yako ya utoaji fedha, weka nambari yako ya akaunti ya Perfect Money, na ubainishe kiasi ambacho ungependa kutoa kwenye sarafu ya akaunti yako ya kutrade. Bofya Inayofuata.
- Muhtasari wa transaction hiyo utaonyeshwa. Weka msimbo wa uthibitishaji uliotumwa kwako kupitia barua pepe au SMS kulingana na aina ya usalama ya Eneo lako la Binafsi (EB). Bofya Thibitisha utoaji fedha
- Ukurasa utaonyesha kuwa transaction yako inaendelea.
- Pesa zitawekwa kwenye akaunti yako ya Perfect Money baada ya muda mfupi.
Je, ninawezaje kutoa pesa ikiwa akaunti yangu ya Perfect Money imezuiwa?
Utahitaji kuwasiliana na timu ya Usaidizi ukiwa na uthibitisho wa kutosha kwamba wewe ndiye mmiliki wa akaunti hiyo, na kuwa akaunti yako ya Perfect Money imezuiwa/kuondolewa. Utahitaji kuwasilisha maelezo yafuatayo, angalau:
- Nambari ya Akaunti yako ya Perfect Money
- Kitambulisho(vitambulisho) vya ankara
- Taarifa za akaunti ya Perfect Money
Ikiwa maelezo haya yatatimiza masharti ya uthibitishaji, ombi lisilo la kiotomatiki la utoaji fedha linaweza kutimizwa kwa kutumia mifumo ya malipo ya EPS inayopatikana; unaweza kuhitaji kuweka kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa ikiwa hujatumia mfumo wa malipo wa EPS uliochaguliwa.
Sticpay
Fanya transactions kwa urahisi kwenye akaunti zako za kutrade kwa kutumia Stickpay, huduma ya kimataifa ya pochi ya kidijitali ambayo hukuruhusu kuweka na kutoa pesa papo hapo. Ili kutumia Stickpay, utahitaji kuwa na akaunti ya Stickpay au ufungue akauti kwenye tovuti yao.
Kumbuka: Tafadhali kumbuka kuwa mfumo huu wa malipo unaweza kuwa nje ya mtandao kwa madhumuni ya matengenezo kwa wakati wowote. Ikiwa njia hii ya malipo haipatikani, tafadhali chagua njia nyingine ya malipo inayopatikana kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
Haya ndiyo unahitaji kujua kuhusu kutumia Stickpay:
Kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa | USD 10 |
Kiasi cha juu zaidi cha pesa kinachoweza kuwekwa | USD 10 000 |
Kiasi cha chini zaidi cha pesa kinachoweza kutolewa | USD 1 |
Kiasi cha juu zaidi cha pesa kinachoweza kutolewa | USD 10 000 |
Ada za uchakataji wa uwekaji na Utoaji fedha | Stickpay inaweza kutoza ada kwa ajili ya huduma zao. |
Muda wa uchakataji wa hatua za uwekaji fedha |
Wastani: Papo hapo* Muda wa juu zaidi: hadi dakika 30 |
Muda wa uchakataji wa hatua za utoaji fedha |
Wastani: Papo hapo* Muda wa juu zaidi: hadi siku 1 |
Kumbuka: Vikomo vilivyobainishwa hapo juu ni kwa kila transaction isipokuwa panapobainishwa vinginevyo.
*Neno "papo hapo" linamaanisha kuwa transaction itafanywa ndani ya sekunde chache bila uchakataji wa wataalamu wa idara yetu ya kifedha. Hii haihakikishi kuwa transaction itakamilika papo hapo, lakini kwamba mchakato umeanza mara moja.
Kuweka pesa kwa kutumia Sticpay
- Chagua Sticpay kwenye sehemu ya Utoaji fedha ya Eneo lako la Binafsi (EB).
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kuongeza pesa, pamoja na kiasi cha pesa ambacho ungependa kuweka, kisha ubofye Endelea.
- Muhtasari wa transaction huwasilishwa; bofya Thibitisha ili kuendelea.
- Utaombwa kuingia kwenye akaunti yako ya Sticpay katika ukurasa unaofuata.
- Weka anwani ya barua pepe ya pochi yako ya kibinafsi, nenosiri na tarehe ya kuzaliwa. Bofya Ingia.
- Stickpay huonyesha ujumbe wa uthibitisho na muhtasari wa pesa ulizoweka; bofya Lipa sasa ili kuthibitisha.
- Ukurasa utaonyesha kuwa transaction yako inaendelea.
- Hatua yako ya uwekaji fedha sasa imekamilika na funds zinapaswa kuonekana kwenye akaunti uliyochagua ya kutrade hivi karibuni.
Kutoa pesa kwa kutumia Sticpay
- Chagua Sticpay kwenye sehemu ya Uwekaji fedha ya Eneo lako la Binafsi (EB).
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kutoa pesa na uweke kiasi ambacho ungependa kutoa katika sarafu iliyoonyeshwa, kisha ubofye Endelea.
- Muhtasari wa transaction hiyo utaonyeshwa.
- Weka msimbo wa uthibitishaji uliotumwa kwa simu au barua pepe yako, kulingana na aina ya usalama, uliyochagua na kisha uthibitishe hatua.
- Weka kiungo cha anwani ya barua pepe iliyosajiliwa kwa akaunti yako ya Stickpay na kisha ubofye Thibitisha.
- Ukurasa utaonyesha kuwa transaction yako inaendelea.
- Hatua yako ya utoaji fedha imekamilika na funds zinapaswa kuonekana kwenye akaunti yako ya benki hivi karibuni.
Usaidizi kwa malipo ya Stickpay
Ikiwa transactions zako hazitaonekana kwenye akaunti yako ya kutrade ndani ya muda wa uchakataji, tafadhali wasiliana na Usaidizi ukiwa na maelezo ya pesa ulizoweka au kutoa tayari; kutoa ushahidi ya malipo au taarifa za benki zenye jina lako, kiasi na maelezo yoyote ya ziada kutaongeza uwezo wetu wa kukusaidia.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu EPS
Je, muda wa uchakataji wa EPS ni upi?
Uwekaji na utoaji fedha unaofanywa kupitia EPS ni wa papo hapo kumaanisha kuwa baada ya kukamilika, transaction hiyo itafanyika ndani ya sekunde chache bila kuchakatwa na wataalamu wetu wa idara ya kifedha. Hata hivyo, hii haihakikishi kuwa transaction itakamilika papo hapo, lakini kwamba mchakato utaanza mara moja. Transaction hiyo itakamilika kulingana na muda wa juu zaidi wa uchakataji.
Ikiwa transaction yako haitaonekana kulingana na muda wa uchakataji ulioonyeshwa, tafadhali wasiliana na Usaidizi.
Je, Exness hutoza ada za transaction?
Hatutozi ada za uwekaji au utoaji fedha unapoweka pesa kwa kutumia EPS nyingi zilizoonyeshwa hapo juu. Isipokuwa tu wakati unatoa funds kwa kutumia Skrill na Perfect Money.
Hakuna ada ya kutoa zaidi ya USD 20 kwa kutumia Skrill, lakini ukitoa chini yake ada ya USD 1 itatozwa. Kwa Perfect Money, kuna ada ya utoaji fedha ya 0.5%.
Ada zinaweza kutozwa na EPS fulani; inapendekezwa kuwa utembelee ukurasa wa mwanzo wa jukwaa la malipo kwa taarifa zozote kuhusu ada za transaction za EPS hiyo.
Je, na ikiwa EPS yangu niliyochagua imezuiwa kwa utoaji fedha?
Ikiwa akaunti yako iliyosajiliwa na mfumo wa malipo imezuiwa kwa sababu yoyote, huenda usiweze kuitumia kutoa pesa (kulingana na kanuni za Exness). Eneo Lako la Binafsi (EB) litaonyesha kwa nini limezuiwa hali hii inapotokea. Utahitaji kuwasiliana na Usaidizi ili kukusaidia kutoa pesa kwa kuwa sharti pesa zitolewe kwa njia ile ile iliyotumika kuziweka.
Unapowasiliana na Usaidizi, tafadhali wasilisha maelezo yafuatayo ili kuharakisha mchakato:
- Taarifa za akaunti
- Uthibitisho wa akaunti ambayo EPS imezuiwa (inaweza kuwa barua pepe).
- Uthibitishaji wa usalama, kama vile PIN yako ya Usaidizi.
Ukiwa na taarifa hizi, Usaidizi unaweza kukusaidia kutoa pesa wakati njia yako ya EPS haipatikani.
Comments
0 comments
Article is closed for comments.