Mifumo ya malipo ya kielektroniki (EPS) inapatikana kimataifa na hutumika kutuma na kupokea funds kwa urahisi kwa kuwa mchakato huu huokoa muda na ni rahisi sana kuutumia. Unaweza kuweka na kutoa pesa kwenye akaunti zako za kutrade kwa kutumia aina mbalimbali za EPS. Unachohitaji ili kuanza ni akaunti iliyosajiliwa iliyo na option ya malipo ambayo ungependa kutumia.
- Neteller
- Skrill
- Perfect Money
- Sticpay
- Maswali Yanayoulizwa Sana
Neteller
Neteller ni njia ya malipo ya kielektroniki maarufu kwa miamala ya papo hapo na salama duniani kote. Unaweza kutumia njia hii ya malipo kuongeza pesa kwenye Akaunti yako ya Exness bila ada yoyote.
Kumbuka: Hatua za uwekaji au utoaji pesa kwa kutumia njia ya malipo ya Neteller zinapatikana tu katika USD na EUR pekee.
Kuweka pesa kwa kutumia Neteller
Baada ya kuchagua Neteller kwenye sehemu ya Uwekaji pesa, fuata hatua hizi:
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kuongeza pesa, pamoja na kiasi ambacho ungependa kuweka na sarafu, kisha ubofye Endelea.
- Muhtasari wa transaction huonyeshwa; bofya Thibitisha ili kuendelea.
- Utaelekezwa upya kwenye tovuti ya Neteller. Weka maelezo ya akaunti yako ya Neteller na ufuate hatua ili kukamilisha hatua hiyo ya uwekaji pesa.
- Hatua yako ya uwekaji pesa sasa imekamilika na unapaswa kuona funds hizo kwenye akaunti ya kutrade uliyochagua hivi karibuni.
Kutoa pesa kwa kutumia Neteller
Baada ya kuchagua Netellerkwenye sehemu ya Utoaji pesa, fuata hatua hizi:
- Chagua sarafu ya utoaji pesa, kisha uweke nambari ya akaunti yako ya Neteller.
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kutoa pesa, na kiasi ambacho ungependa kutoa. Bofya Endelea.
- Muhtasari wa transaction hiyo utaonyeshwa. Bofya Thibitisha.
- Thibitisha transaction ukitumia aina yako ya usalama ya sasa (hatua zinaweza kutofautiana). Bofya Thibitisha.
- Hatua yako ya utoaji pesa sasa imekamilika.
Usaidizi wa Neteller
Ikiwa unahitaji usaidizi katika transaction yako, nenda kwenye Historia yako ya transaction, chagua transaction ambayo unahitaji usaidizi nayo, na ubofye Pata usaidizi ili kutuma ombi la usaidizi.
Skrill
Skrill ni njia maarufu sana ya malipo ya kielektroniki inayopatikana katika takriban nchi 200 kote duniani. Skrill inaweza kukusaidia kuhamisha pesa kwenye tovuti mbalimbali papo hapo na inaweza kutumika kuongeza pesa kwenye akaunti yako ya kutrade ya Exness bila kulipa ada yoyote.
Kuweka pesa kupitia Skrill
Chagua Skrill kwenye sehemu ya Uwekaji pesa na ufuate hatua hizi:
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kuongeza pesa, pamoja na kiasi cha kuweka pesa, na uchague sarafu, kisha ubofye Continue.
- Muhtasari wa transaction huonyeshwa; bofya Thibitisha ili kuendelea.
- Utaelekezwa upya kwenye ukurasa wa tovuti wa Skrill ambapo aidha:
-
- Utaingia ukitumia kitambulisho chako cha Skrill ili uingie eneo lako la mwanachama.
- Utafungua akaunti mpya ya Skrill ili kufikia eneo lako la mwanachama.
- Chagua njia yako ya malipo ndani ya tovuti ya Skrill na ufuate maagizo kwenye skrini.
- Hatua hiyo ya uwekaji pesa sasa imekamilika na uchakataji utaanza.
Kutoa pesa kupitia Skrill
Chagua Skrill kwenye sehemu ya Utoaji pesa na ufuate hatua hizi:
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kutoa pesa, chagua sarafu yako ya utoaji pesa na kiasi unachotoa na uweke anwani iliyosajiliwa ya barua pepe ya akaunti yako ya Skrill. Bofya Endelea.
- Muhtasari wa transaction utaonyeshwa, bofya Thibitisha.
- Thibitisha transaction ukitumia aina yako ya usalama ya sasa (hatua zinaweza kutofautiana). Bofya Thibitisha.
- Hatua yako ya utoaji pesa sasa imekamilika.
Usaidizi wa Skrill
Ikiwa unahitaji usaidizi katika transaction yako, nenda kwenye Historia yako ya transaction, chagua transaction ambayo unahitaji usaidizi nayo, na ubofye Pata usaidizi ili kutuma ombi la usaidizi.
Perfect Money
Perfect Money ni njia ya malipo ya kielektroniki maarufu sana kote duniani. Unaweza kutumia njia hii ya malipo kuongeza pesa kwenye akaunti zako za kutrade ikiwa una akaunti ya Exness iliyothibitishwa kikamilifu.
Kuweka pesa kwa kutumia Perfect Money
Baada ya kuchagua Perfect Money kwenye sehemu ya Uwekaji pesa, fuata hatua hizi:
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kuongeza pesa pamoja na kiasi ambacho ungependa kuweka na sarafu, kisha ubofye Endelea.
- Muhtasari wa transaction huonyeshwa. Bofya Thibitisha ili uendelee.
- Utaelekezwa upya kwenye tovuti ya Perfect Money; chagua option ya akaunti ya Perfect Money kisha ubofye Fanya Malipo.
- Huenda utahitaji kukamilisha captcha na kuthibitisha hatua hiyo ya uwekaji pesa.
- Baada ya kuthibitishwa, hatua hiyo ya uwekaji pesa imekamilika.
Kutoa pesa kwa kutumia Perfect Money
Baada ya kuchagua Perfect Moneykwenye sehemu ya Utoaji pesa, fuata hatua hizi:
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kutoa pesa na uweke kiasi ambacho ungependa kutoa katika sarafu iliyoonyeshwa, kisha ubofye Endelea.
- Muhtasari wa transaction huonyeshwa. Bofya Thibitisha
- Thibitisha transaction ukitumia aina yako ya usalama ya sasa (hatua zinaweza kutofautiana). Bofya Thibitisha.
- Hatua hiyo ya utoaji pesa imekamilika na uchakataji sasa utaanza.
Usaidizi wa Perfect Money
Ikiwa unahitaji usaidizi katika transaction yako, nenda kwenye Historia yako ya transaction, chagua transaction ambayo unahitaji usaidizi nayo, na ubofye Pata usaidizi ili kutuma ombi la usaidizi.
Sticpay
Fanya transactions kwa urahisi ukiwa na akaunti zako za kutrade kwa kutumia Stickpay, huduma ya kimataifa ya pochi ya kidijitali ambayo hukuruhusu kuweka na kutoa pesa papo hapo. Ili kutumia Stickpay, utahitaji kuwa na akaunti ya Stickpay au kuifungua kwenye tovuti yao.
Kuweka pesa kwa kutumia Sticpay
Baada ya kuchagua StickPay kwenye sehemu ya Uwekaji pesa, fuata hatua hizi:
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kuongeza pesa na uweke kiasi cha pesa ambacho ungependa kuweka. Bofya Endelea.
- Muhtasari wa transaction huonyeshwa. Bofya Thibitisha ili uendelee.
- Kisha, utaelekezwa kwenye tovuti ya Stickpay ili kuingia kwenye akaunti yako ya Sticpay.
- Weka anwani ya barua pepe na nenosiri la pochi yako ya kibinafsi. Bofya Ingia. Unaweza pia chagua kuingia kwa kutumia Msimbo wa QR.
- Stickpay huonyesha ujumbe wa uthibitisho na muhtasari wa hatua ya kuweka pesa; bofya Lipa sasa ili kuthibitisha.
- Ukurasa utaonyesha kuwa transaction yako inaendelea.
- Hatua hiyo ya uwekaji pesa sasa imekamilika na uchakataji utaanza.
Kutoa pesa kwa kutumia Sticpay
Chagua SticPay kwenye sehemu ya Utoaji pesa na ufuate hatua hizi:
- Chagua akaunti ya kutrade ambayo ungependa kutoa pesa na uweke kiasi ambacho ungependa kutoa katika sarafu iliyoonyeshwa, kisha ubofye Endelea.
- Muhtasari wa transaction hiyo utaonyeshwa. Bofya Thibitisha.
- Thibitisha transaction ukitumia aina yako ya usalama ya sasa (hatua zinaweza kutofautiana). Bofya Thibitisha.
- Weka anwani ya barua pepe iliyosajiliwa kwa akaunti yako ya Stickpay, kisha ubofye Thibitisha.
- Hatua hiyo ya utoaji pesa sasa imekamilika na uchakataji sasa utaanza.
Usaidizi wa Sticpay
Ikiwa unahitaji usaidizi katika transaction yako, nenda kwenye Historia yako ya transaction, chagua transaction ambayo unahitaji usaidizi nayo, na ubofye Pata usaidizi ili kutuma ombi la usaidizi.
Maswali Yanayoulizwa Sana
Je, ninaweza kuona wapi maelezo kuhusu njia zangu za malipo?
Muda wa uchakataji, ada na vikomo huonyeshwa chini ya njia ya malipo kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
Ikiwa unahitaji usaidizi katika transaction yako, nenda kwenye Historia yako ya transaction, chagua transaction ambayo unahitaji usaidizi nayo, na ubofye Pata usaidizi ili kutuma ombi la usaidizi
Je, Exness hutoza ada za transaction?
Exness haitozi ada ya uchakataji kwa hatua za uwekaji fedha, lakini baadhi watoa huduma za malipo wanaweza kutoza. Thibitisha ada zinazowezekana kwa njia ya malipo uliyochagua kila wakati kwenye Eneo la Binafsi, au kwenye tovuti ya mtoa huduma huyo wa malipo.
Je, na ikiwa EPS yangu niliyochagua imezuiwa kutoa pesa?
Tafadhali wasiliana na Usaidizi ikiwa akaunti ya mfumo wako wa malipo itazuiwa kwa sababu yoyote. Transactions zako zinaweza kosa kuchakatwa ikiwa akaunti hizi zimezuiwa.
Kuwa na taarifa hizi tayari huhakikisha upesi:
- Taarifa za akaunti
- Uthibitisho kuwa akaunti ya malipo imezuiwa.
Ukiwa na taarifa hizi, wataalamu wetu wa malipo wanaweza kukusaidia kutoa pesa wewe mwenyewe ikiwa uthibitishaji wa akaunti umethibitishwa.