Ikiwa hutapokea msimbo wa uthibitishaji kupitia SMS unapojaribu kuidhinisha kitendo cha akaunti yako, kuna mambo machache ambayo unaweza kujaribu ili kutatua tatizo hili.
- Thibitisha kuwa aina ya usalama uliyowekwa ni simu yako kwa kuingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB). Bofya Mipangilio > Mipangilio ya usalama na utazame maelezo yaliyoorodheshwa chini ya uthibitishaji wa hatua 2. Nambari yako ya simu ambayo SMS inapaswa kutumwa inapaswa kuonyeshwa. Ikiwa inaonyesha anawani ya barua pepe au nambari tofauti ya simu, bofya Badilisha na uchague au uongeze nambari yako ya simu.
- Hakikisha kuwa nambari ya simu uliyoweka iko katika umbizo sahihi la kimataifa. Msimbo wa nchi unaweza kuwa umelinganishwa kiotomatiki na nchi yako ya makazi iliyosajiliwa, hivyo kusababisha nambari yako halisi ya simu kutosajiliwa kwa usahihi. Ikiwa msimbo wa nchi sio sahihi, sasisha nambari hiyo ya simu kwa kufuata mchakato ule ule ulioonyeshwa kwenye Point ya 1, na kisha ujaribu kutuma SMS tena.
Kumbuka: Ikiwa unasafiri kwenda nchi ya kigeni, sharti uwashe mipangilio ya muunganisho nje ya eneo lako ili kupokea misimbo ya SMS.
- Subiri kidogo na ikiwa ujumbe hautatumwa ndani ya dakika 5, bofya Resend the Message kwenye skrini ya uthibitishaji. Unaweza kurudia hatua hii mara 3 - 4 ukitumia vivinjari tofauti, kwa vipindi visivyozidi dakika 1 kati ya kila wakati.
- Futa faili za akiba na vidakuzi vya kivinjari chako kisha ujaribu tena. Unaweza pia jaribu kutumia kivinjari tofauti.
- Kwenye kifaa chako cha mkononi, washa data yako na/au iweke kwenye Hali ya Ndegeni ili kuanzisha upya muunganisho, na ubofye Resend the Message.
- Zima kisha uwashe simu yako tena, na ubofye Resend the Message. Subiri saa moja ili mipangilio hiyo iwekwe upya.
- Weka kadi yako ya SIM kwenye simu tofauti na ubofye Resend the Message.
Ikiwa bado haujapokea SMS, bofya Tumia njia nyingine ili kupokea msimbo na uchague simu ya kiotomatiki kwa nambari yako ya simu ili kupokea msimbo.
Ikiwa hakuna mojawapo ya mapendekezo yaliyo hapo juu yatakayotatua tatizo hilo, usisite kuwasiliana na Timu yetu ya Usaidizi ambayo itakupa usaidizi zaidi.
Ikiwa nambari yako ya simu ya sasa iliyosajiliwa itaendelea kuonyesha tatizo hili, zingatia kutumia nambari nyingine ya simu ili kuona kama tatizo linaendelea. Fuata kiungo kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubadilisha nambari ya simu ya akaunti yako.
Kumbuka: Unaweza kutumia Arifa za programu ili kuthibitisha transactions badala ya uthibitishaji wa SMS. Arifa za programu hukuruhusu kutekeleza hatua zinazohitaji kiwango cha juu cha usalama kwa haraka. Hatua inapofanywa, kwa mfano ombi la utoaji pesa, Arifa ya programu hutumwa kwa kifaa chako cha mkononi. Bofya Ndiyo/Hapana ili kuthibitisha ombi hilo.
Ili kuwezesha Arifa za programu, unaweza kubadilisha aina yako ya usalama kwenye Eneo lako la Binafsi. Pata maelezo zaidi kuhusu kubadilisha aina yako ya usalama kuwa Arifa za programu.