Tumekusanya sababu za kawaida zinazosababisha hitilafu kutokea wakati wa kuweka na kutoa pesa ili uweze kupata suluhisho linalowezekana.
Ukiendelea kukumbana na hitilafu katika kuweka na kutoa funds, wasiliana na Usaidizi wa Exness ukiwa na maelezo yafuatayo tayari:
- Nambari yako ya akaunti.
- Jina la mfumo wa malipo unaojaribu kuhamishia pesa.
- Picha ya skrini au picha ya ujumbe wa hitilafu unaopokea (ikiwa upo).
Kumbuka: Sababu ya kutofaulu kwa hatua ya kuweka au kutoa pesa inaweza kuonekana kwenye Eneo lako la Binafsi.
Hitilafu za hatua za kuweka na kutoa pesa
Huu hapa ni ujumbe wa hitilafu unaotokea mara nyingi zaidi wakati wa kuweka na kutoa pesa, na jinsi unavyoweza kutatuliwa:
- Tarehe si sahihi
- Tafadhali kagua tarehe uliyoweka na ujaribu tena.
- Kadi haiwezi kutumika
- Tafadhali tumia kadi ya Visa, Mastercard, au JCB inayoweza kutumia sarafu hiyo ya transaction.
- Jina la mwenye kadi si sahihi
- Tafadhali kagua jina uliloweka na ujaribu tena.
- Akaunti Haipatikani
- Tafadhali kagua maelezo ya akaunti yako na ujaribu tena.
- Tatizo likiendelea, tafadhali wasiliana na Usaidizi wa Exness.
- Huna pesa za kutosha
- Tafadhali hakikisha kuwa kiasi cha pesa unazotoa kiko ndani ya kikomo cha free margin inayopatikana.
- Akaunti si ya Eneo lako la Binafsi**
- Tafadhali weka maelezo ya akaunti yaliyo chini ya jina lako.
- Umbizo la barua pepe si sahihi
- Tafadhali kagua anwani ya barua pepe na ujaribu tena.
- Kiasi cha chini zaidi cha BTC kinachoweza kutolewa
- Tafadhali hakikisha kuwa kiasi cha pesa unachotoa kiko ndani ya kikomo.
- Akaunti Perfect Money si sahihi
- Tafadhali kagua maelezo ya akaunti na ujaribu tena.
- Sarafu uliyoomba hailingani na sarafu ya akaunti
- Tafadhali rekebisha sarafu ya kutoa pesa ili ilingane na sarafu ya akaunti.
- Akaunti ya WebMoney si sahihi
- Tafadhali kagua maelezo uliyoweka ya akaunti na ujaribu tena.
**Inatumika kwa uhamishaji wa ndani pekee.
Comments
0 comments
Article is closed for comments.