Kuanzia hatua za uwekaji pesa zilizokataliwa hadi za utoaji pesa ambazo hazikufaulu, kutojua sababu kunaweza kukatisha tamaa. Katika makala haya, tutaeleza sababu za kawaida zinazosababisha malipo kutofaulu, pamoja na baadhi ya hatua mahususi unazoweza kuchukua ili kutatua hitilafu hizo.
Hatua muhimu zaidi ni kuangalia Historia ya transaction (kwenye eneo lako la binafsi) kwanza. Kila transaction ambayo haitafaulu itaonyesha msimbo au ujumbe wa hitilafu.
Hizi hapa ni hitilafu za kawaida ambazo unaweza kukumbana nazo:
Muda wa transaction umeisha kwa sababu ya kutochukua hatua, kutokamilisha transaction, au hitilafu ya muunganisho. Ikiwa timeframe imebainishwa, hakikisha kuwa umekamilisha transaction hiyo ndani ya time frame iliyowekwa. Tatizo hilo likiendelea, unaweza jaribu njia nyingine ya malipo.
Hali hii inaweza kutokea ukituma maombi mengi sana ndani ya muda mfupi au ikiwa mfumo wa mtoa huduma umejaa kupita kiasi. Unaweza rudia operesheni hii baadaye. Tatizo hilo likiendelea, unaweza jaribu njia nyingine ya malipo.
Hali hii inaweza kutokea ikiwa umefunga fomu ya uhamishaji bila kuikamilisha, umeacha fomu ikiwa imefunguliwa bila kuchukua hatua, au unakumbana na hitilafu za muunganisho. Hakikisha kuwa muunganisho wako ni dhabiti na urudie operesheni hiyo, huku ukikamilisha hatua zote muhimu. Tatizo hilo likiendelea, unaweza jaribu njia nyingine ya malipo.
Hali hii inaweza kutokea ikiwa kuna tatizo la muda kwa upande wa benki kutokana na matengenezo ya muda mfupi. Unaweza kujaribu tena baadaye, na ikiwa tatizo hilo halijatatuliwa ndani ya saa 24, unaweza kuwasiliana na benki yako. Wakati huo huo, unaweza pia kutumia njia nyingine ya malipo.
Hali hii inaweza kutokea ikiwa kuna tatizo la muda kwa upande wa mtoa huduma wa malipo kutokana na tatizo la kiufundi la muda mfupi. Unaweza kujaribu tena baadaye au utumie njia nyingine ya malipo.
Kumekuwa na tatizo katika kuchakata kadi yako. Hakikisha kuwa umeweka maelezo sahihi ya malipo na kuwa muda wa matumizi wa kadi haujaisha na ujaribu tena. Unaweza pia kutumia njia nyingine ya malipo.
Hali hii hutokea wakati salio la akaunti yako halitoshi kukamilisha transaction hiyo. Unaweza kuongeza salio lako au kurekebisha kiasi cha transaction.
Transaction yako haikuchakatwa na benki inayotoa kadi hiyo. Unaweza jaribu tena, lakini si kwa zaidi ya mara 3 hadi 5 mfululizo ili kuzuia kadi yako kuzuiwa.
Tatizo hilo likiendelea, unaweza kuwasiliana na benki yako ili upate maelezo kama kuna vikomo au vikwazo vilivyowekwa kwenye kadi yako. Vinginevyo, unaweza kutumia kadi au njia nyingine ya malipo.
Hali hii hutokea wakati uthibitishaji wa 3D Secure (OTP) haujafaulu. Unaweza kujaribu mojawapo ya suluhisho zifuatazo:
- Hakikisha kuwa umeweka msimbo sahihi.
- Ikiwa muda wa msimbo umeisha, tuma omba jipya na ujaribu tena.
- Hakikisha kuwa ukurasa wa Udhibiti wa Ufikiaji haujazuiwa na programu jalizi za kivinjari.
- Tumia kadi au njia nyingine ya malipo, kwa kuwa 3D Secure huenda isiweze kutumika na mtoa huduma wako wa malipo.
Hali hii inaweza kutokea ikiwa umejaribu zaidi ya mara tatu bila kufanikiwa ukitumia kadi sawa au umetumia zaidi ya kadi tatu tofauti ndani ya saa 24.
Tafadhali subiri saa 24 ili ujaribu tena ukitumia njia iyo hiyo ya malipo. Wakati huo huo, unaweza kutumia njia nyingine ya malipo.
Hali hii hutokea wakati BUID uliyoweka si sahihi au bado haijathibitishwa. Hakikisha kuwa umeweka BUID ya sasa na ujaribu tena.
Ikiwa bado haujathibitisha BUID yako katika Exness, tafadhali wasiliana na timu yetu ya usaidizi ukiwa na picha ya skrini au rekodi ya video ya akaunti yako ya Binance.
Tumeona hatua kadhaa za uwekaji pesa kupitia njia ya malipo iliyotumika, ikifuatiwa na utoaji pesa kupitia njia nyingine za malipo, bila shughuli zinazolingana za biashara. Kwa sababu hii, huwezi kutumia njia ya malipo iliyotumika tena, kwa hatua za uwekaji pesa. Kwa hatua za uwekaji pesa za siku zijazo, tafadhali tumia njia nyingine za malipo zinazopatikana.
Hii inaweza kutokea ikiwa umeomba kutoa pesa kupitia benki ya mtandaoni. Tafadhali wasilisha taarifa yako ya benki au uthibitisho wa transaction kwa ankara mahususi (pesa zilizowekwa zilizoonyeshwa) kwa kutumia kitufe cha Pata usaidizi. Hakikisha kuwa taarifa hiyo ya benki au uthibitisho wa transaction una jina lako.
Tafadhali tumia njia nyingine za malipo zinazopatikana katika Eneo lako la Binafsi (EB) kwa uwekaji pesa wa siku zijazo. Bado utaweza kutoa pesa bila vikomo na unaweza kuendelea kutumia njia nyingine za malipo kwa hatua za uwekaji pesa.