Kusubiri pesa ulizotoa kunaweza kufadhaisha ikiwa huna uhakika na sababu ya kucheleweshwa. Hapa kuna sababu chache ambazo zinaweza kuchangia wakati wa kusubiri.
Muda wa Uchakataji
Huenda kukawa na nyakati mahususi za uchakataji kwa mifumo fulani ya malipo. Angalia inachukua muda gani kwa funds kuonekana kulingana na mfumo wa malipo uliochagua kwenye EB lako. Kwa mfano, refunds za kadi ya mkopo zinaweza kuchukua hadi siku 10 za kazi kukamilika.
Nyakati hizi zinaweza kupatikana katika Kituo cha Usaidizi cha Mifumo ya Malipo; tafuta tu nchi unakoishi na utafute mfumo wa malipo ili kuona maelezo yake.
Angalia hali ya transaction yako kutoka kwa kichupo cha Transaction History kwenye Eneo lako la Binafsi. Utaweza kuona transactions kulingana na hali na aina (Kuweka pesa, Kutoa pesa, au Kuhamisha pesa).
Unaweza kuchuja akaunti zako kwa kutumia kichupo cha Akaunti zote. Ikiwa huwezi kuona kichujio hiki, akaunti zako hazina transactions.
Sera ya transaction
Wakati wa kutoa pesa, kumbuka kuwa hatua ya kutoa pesa sharti iwe kutoka kwa mfumo wa malipo uliotumia kuziweka kwenye Eneo lako la Binafsi. Isitoshe, utoaji wa pesa hufanywa kwa mifumo hiyo ya malipo kwa uwiano sawa na pesa zilivyowekwa na uko chini ya masharti ya kipaumbele ya mfumo wa malipo.
Hatua ya kutoa pesa inaweza kukataliwa, na hata kuchelewa ikiwa masharti haya hayajafuatwa.
Maelezo ya Transaction
Inawezekana kuwa baadhi ya maelezo hayakuwekwa kwa usahihi wakati wa kutoa pesa; ikiwa kuna njia ya kuthibitisha hili, zingatia kuwa kuna uwezekano wa utoaji wa pesa kukataliwa au kucheleweshwa ikiwa maelezo si kamili.
Ikiwa utoaji wako wa pesa umezidi muda wa juu zaidi wa uchakataji, unaweza kuwasiliana na Wasaidizi wa Exness kupitia EB lako au utume barua pepe kwa Wasaidizi ukitumia anwani yako ya barua pepe iliyosajiliwa, ukiwa na taarifa zifuatazo:
- Taarifa ya benki au Akaunti, kulingana na mfumo wako wa malipo uliotumia (kutoka tarehe ya kutoa pesa kufikia sasa)
- Nambari ya akaunti yako ya kutrade
- Nambari yako ya ankara
- Tarehe ya kutoa pesa
Fuata kiungo kwa maelezo mengine yoyote ambayo ungependa kujua kuhusu utoaji wa pesa.
Comments
0 comments
Article is closed for comments.