Ikiwa umekumbana na matatizo yoyote wakati wa usajili, uthibitishaji wa wasifu, au kuingia kwenye akaunti yako, tuna orodha ya mada za kawaida ambazo zinaweza kukusaidia kutatua tatizo hilo.
Mada za kawaida:
- Je, kwa nini siwezi kusajili akaunti ya Exness?
- Je, kwa nini siwezi kuweka nenosiri wakati wa usajili?
- Je, kwa nini siwezi kupakia hati za uthibitishaji?
- Je, kwa nini siwezi kuingia kwenye Eneo langu la Binafsi?
Je, kwa nini siwezi kusajili akaunti ya Exness?
Hatua ya kujisajili kwenye akaunti ya Exness inahitaji tu anwani sahihi ya barua pepe na nambari ya simu inayofanya kazi kutoka nchi ya makazi iliyochaguliwa. Ili kuanza, utahitaji tu kuweka anwani ya barua pepe na kuunda nenosiri ili kufungua Eneo lako la Binafsi (EB); hatua ya kuongeza nambari ya simu kwenye akaunti huja baadaye.
Huenda unakumbana na mojawapo ya hitilafu zifuatazo ikiwa unakabiliwa na tatizo katika kusajili akaunti:
Anwani ya barua pepe tayari imeunganishwa na akaunti
Kumbuka: Ikiwa unaona hitilafu hii, anwani hii ya barua pepe tayari imetumika kusajili akaunti katika Exness na haiwezi kutumika tena. Pia kuna uwezekano kwamba ulitumia maelezo ya kuingia kwenye Google na ukachagua anwani hii ya barua pepe kuingia hapo awali.
Ili kurekebisha tatizo hili, unaweza:
- Kujaribu kurejesha nenosiri la Eneo lako la Binafsi (EB) hapa.
- Tumia anwani tofauti ya barua pepe kujisajili.
Weka anwani halali ya barua pepe
Hakikisha kuwa umeweka anwani yako ya barua pepe kwa usahihi na ukamilifu bila nafasi au herufi zozote za ziada ambazo zinaweza kuwa zimewekwa bila kukusudia. Ikiwa unatumia Google kuingia, hakikisha kuwa anwani hiyo ya barua pepe bado inatumika.
Ikiwa unaona hitilafu hii, bofya kitufe cha Enter kwenye kibodi yako katika sehemu ya kuweka anwani ya barua pepe ili kupata kidokezo kuhusu ni nini haswa kinahitaji kubadilishwa/kurekebishwa.
Je, kwa nini siwezi kuweka nenosiri wakati wa usajili?
Ni rahisi kuweka au kuweka upya nenosiri. Masharti ya msingi unayofaa kukumbuka wakati wa kuweka nenosiri la Eneo lako la Binafsi (EB) ni:
- Sharti liwe na herufi 8-15
- Sharti liwe na herufi kubwa na ndogo (mfano wa herufi kubwa - A,Z; mfano wa herufi ndogo - a,z)
- Sharti liwe na mchanganyiko wa nambari na herufi za Kiingereza (mfano - 123Happy)
- Ikiwa unajumuisha herufi maalum, unaweza kuchagua kati ya herufi zifuatazo: # [ ] ( ) @ $ & *! ? | , . / \ ^ + - _
Tovuti ina kipengele muhimu cha kuweka rangi ili uweze kutambua ni masharti gani yametimizwa na ambayo hayajatimizwa.
Ukishaweka nenosiri, rangi ya masharti itabadilika na kuwa kijani au nyekundu ili kuonyesha kama yametimizwa/hayajatimizwa mtawalia. Aidha, utaweza tu kubofya kitufe cha Endelea mara tu rangi ya masharti yote itakapokuwa kijani.
Kumbuka: Katika baadhi ya matukio, unaweza pia kuombwa kuweka alama kwenye captcha ya "I am not a robot” kabla ya kuweza kubofya kitufe cha Endelea. Mfano wa nenosiri linalokubalika ni Exness_123, lakini hatupendekezi utumie manenosiri rahisi kama haya.
Je, kwa nini siwezi kupakia hati za uthibitishaji?
Hapa kuna vidokezo vichache vya kuhakikisha upakiaji rahisi wa hati zako za uthibitishaji:
- Hakikisha kuwa umejaza kikamilifu Wasifu wako wa Mteja Kiuchumi kabla ya kuendelea kuwasilisha hati zako za POI (Uthibitisho wa Utambulisho) na POR (Uthibitisho wa Makazi). Utahitaji kutayarisha hati mbili tofauti za uthibitishaji wa POI na POR.
Kwa mfano, ikiwa ulitumia Kadi yako ya Kitambulisho kwa POI, unaweza kutumia bili ya matumizi (umeme, gesi, maji) kwa uthibitishaji wa POR.
Kumbuka: Wateja katika baadhi ya nchi wanaweza kutumia hati moja kuthibitisha POI na POR.
- Ukubwa wa faili yako haupaswi kuzidi MB 50. Ikiwa kikomo hiki kimezidishwa, hati haitapakiwa kwa uthibitisho.
- Tayari umewasilisha: Ikiwa tayari umewasilisha hati ithibitishwe, huwezi kupakia upya hati nyingine hadi iliyowasilishwa ikaguliwe. Tafadhali subiri barua pepe kuhusu hali ya hati yako kabla ya kupakia hati nyingine. Unaweza pia kuangalia hili kwenye upau wa hali ya uthibitishaji juu ya skrini kuu katika Eneo la Binafsi.
- Hati za POI na POR zinaweza kuwasilishwa kwa ukaguzi pamoja. Ukipenda, unaweza kuruka upakiaji wa POR na uufanye baadaye, hata hivyo, tunapendekeza kwamba uwasilishe hati hizo pamoja ili kukamilisha mchakato wa uthibitishaji.
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuthibitisha wasifu wako kikamilifu.
Je, kwa nini siwezi kuingia kwenye Eneo langu la Binafsi?
Hapa kuna orodha ya ukaguzi ili kukusaidia kutatua tatizo la kutoweza kuingia kwenye EB lako.
- Ukaguzi wa jina la mtumiaji
Jina la mtumiaji la kuingia kwenye EB lako ni anwani yako ya barua pepe iliyosajiliwa. Usiweke nambari yoyote ya akaunti ya kutrade au jina lako kama jina la mtumiaji.
- Ukaguzi wa nenosiri
Unahitaji kutumia nenosiri la EB lililowekwa wakati wa usajili ili kuingia.
Wakati wa kuweka nenosiri, hakikisha kuwa hakuna nafasi za ziada na makosa ya uchapaji na uangalie ikiwa kitufe cha Caps Lock kimewashwa kwa kuwa manenosiri huathiriwa na ukubwa na udogo wa herufi.
Ikiwa umesahau nenosiri lako, unaweza kuliweka upya kwa kubofya kiungo hiki ili kuweka upya nenosiri la Eneo lako la Binafsi.
- Utatuzi wa matatizo ya kuingia
Unaweza kukumbana na matatizo wakati wa kuingia kwenye EB lako, hata maelezo sahihi ya kuingia yakiwa yamewekwa. Futa faili za akiba na vidakuzi vyako kwenye kivinjari chako na ujaribu tena, au ujaribu kuingia kutumia kivinjari tofauti.
- Ukaguzi wa akaunti
Ikiwa ulituma ombi la akaunti yako kufungwa katika Exness hapo awali, huwezi kutumia EB hilo tena. Zaidi ya hayo, huwezi kutumia anwani hiyo ya barua pepe kujisajili tena. Fungua EB jipya kwa kutumia anwani tofauti ya barua pepe ili ujisajili nasi tena.
Tunatumahi kuwa maelezo haya yatakufaa. Ikiwa kuna matatizo yoyote zaidi, usisite kuwasiliana na Usaidizi ukiwa na picha ya skrini ya ukurasa wenye hitilafu.