Sababu nyingi zinaweza kuonyesha aina hii ya hitilafu, na ujumbe wa "trading is disabled". Kutatua hitilafu hii kutategemea terminali gani ya biashara unayotumia: MetaTrader 4 au MetaTrader 5.
- Katika MT4: kitufe cha Order Mpya kitaonekana kufanya kazi, lakini hitilafu ya "Trading is Disabled" itaonekana kwenye kichupo cha Jarida cha terminali ya biashara.
- Katika MT5: kitufe cha Orde Mpya kitaonekana kutofanya kazi.
Hitilafu ya aina hii mara nyingi husababishwa na matukio yafuatayo (kunaweza kuwa na matukio yasiyotokea mara nyingi):
Ufanyaji biashara umezimwa kwenye akaunti hiyo mahususi
Katika hali hii, kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kurekebisha tatizo hili:
- Hakikisha kuwa umekamilisha hatua ya kuweka kiasi cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza kwenye akaunti hiyo ya kutrade. Bila kiasi kinachotimiza masharti cha pesa zinazoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza, MT4 itaonyesha ujumbe wa hitilafu ya "Trade is disabled" wakati wowote unapojaribu kufungua order mpya. Kwa MT5, kitufe cha Order Mpya kitaonekana kutofanya kazi.
- Kamilisha uthibitishaji wa akaunti yako ya Exness; akaunti ambazo hazijathibitishwa zimewekewa vikwazo ambavyo ni pamoja na kuzuiwa kufanya biashara siku 30 baada ya pesa kuwekwa kwa mara ya kwanza. Katika hali hii terminali ya biashara itaonyesha ujumbe wa hitilafu. Fuata kiungo ili kupata maelezo kuhusu jinsi ya kuthibitisha wasifu wako wa Exness kikamilifu.
Ufanyaji biashara umezimwa kwenye zana mahususi
Instruments za biashara zinaweza kuzuiwa kwa muda tu au kabisa. Ukijaribu kutrade instruments hizi zikiwa zimezuiwa, utaona ujumbe wa hitilafu kwenye Dirisha la order:
- MT4 huonyesha hitilafu: “Trade: No”
- MT5 huonyesha hitilafu: “Trade: Disabled”
Ili kuthibitisha kuwa instrument mahususi imezuiwa, fuata kiungo hiki ili kuangalia upatikanaji wa instrument. Unaweza pia jaribu kutrade kwa kutumia instrument tofauti ili kuthibitisha kuwa hii ndiyo sababu ya hitilafu.
Usaidizi zaidi
Ikiwa bado unaona hitilafu ambayo inakuzuia kufanya biashara, na hakuna maelezo hao juu yanayoielezea, tafadhali wasiliana na Usaidizi kwa usaidizi zaidi.