Unaweza kupata hitilafu ya “Not enough money” wakati wa kufungua trade. Hitilafu hii hutokea wakati trader anajaribu kufungua trade lakini hana funds za kutosha kulipia gharama zake. Wacha tuangalie hii kwa undani zaidi:
Kuelewa margin na gharama ya spread
Ili kuelewa jinsi tunavyoweza kuepuka hitilafu hii, ni muhimu kuelewa margin na gharama ya spread ya trade:
- Margin: Hizi ni pesa zilizowekwa za dhamana zinazoshikiliwa kwa ajili ya kuweka trade wazi. Unaweza kuzikokotoa hili kwa urahisi kwa kutumia Kikokotoo chetu cha Biashara.
- Gharama ya Spread: Hii ni faida ya broker ambayo hutozwa unapofungua trade. Inaweza kuhesabiwa takriban kama:
Gharama ya Spread = Spread ya wastani katika pips × Pip Value
Pip value inaweza kupatikana kwenye kikokotoo cha uwekezaji nayo spread ya wastani inaweza kupatikana kwa urahisi kwenye tovuti yetu kwa instruments zote zinazotolewa.
Sasa kwa kuwa unajua jinsi ya kufanya ukokotoaji huu, unapaswa kuwa na uwezo wa kukadiria kiwango cha trades ambazo unaweza kuweka ukiwa na kiasi fulani cha funds.
Vidokezo vya kutatua hitilafu
Kuna hali ambapo spread, au gharama zinazohusiana na order, hubadilika mara kwa mara kulingana na wakati. Mtu anaweza chagua kungoja tu hadi mwenendo mzuri wa bei ujitokeze ili kujaribu order hiyo tena.
Hatua kuu za utatuzi wa hitilafu ni pamoja na:
- Kupunguza kiwango cha biashara ili kupunguza gharama za biashara.
- Kuongeza leverage ili kupunguza margin.
- Kuweka pesa ili kuongeza free margin yako.
Traders wengine wanaweza kupata vidokezo vingine vinavyofaa:
- Kuangalia kalenda ya kiuchumi kwa habari muhimu kunaweza kusaidia katika kutambua ni zana gani za biashara zitakuwa na mahitaji ya juu ya margin. Pia utapokea barua pepe yenye orodha ya instruments zilizoathiriwa kila siku kwa terminali za biashara za MT4/5.
- Kuweka mipangilio ya pending order kwa bei ambayo ungependa kunaweza pia kuwa muhimu, kwa kuwa order inaweza kufunguliwa baadaye kwa spread ya chini na kusababisha gharama ya chini ya spread.
Kumbuka: Mara tu pending order inapoghairiwa, iwe ni kwa sababu ya free margin isiyotosha au leverage ya chini, utapokea arifa ya programu kwa order iliyoghairiwa kwenye programu ya Exness Trade au arifa ibukizi itaonekana kwenye Terminali ya Exness.
Kwa mfano: Huwezi kutekeleza pending order #232323 ya UNUNUZI kwa lot(lots) 0.2 za XAU/USD.
Ikiwa bado utapata hitilafu hii, usisite kuwasiliana na Timu yetu ya usaidizi.