Kuna sababu kadhaa za hitilafu hii.
- Hakuna bei za instruments zilizochaguliwa kwa sasa, au bei za mwisho haziwezi kuchukuliwa tena kama bei za soko. Kwa sababu hii, trader anapojaribu kutekeleza order kwa bei hizi, seva ya biashara hurejesha ujumbe wa 'Off quotes' na kukataa execution.
- Trader anafanya trade kwenye instrument ambayo imesitishwa.
- Wakati trader amepokea ujumbe wa kukataliwa hapo awali kama vile ‘Not enough free margin’.
Kumbuka: Kumbuka saa za biashara kwa kila kikundi cha instruments, pata maelezo zaidi kuhusu Saa za biashara za soko la Forex.
Hizi hapa ni baadhi ya hatua za kutatua hitilafu hiyo:
- Usifanye biashara wakati soko linabadilika-badilika na kukiwa na kiwango kidogo cha kuathirika kwa bei.
- Angalia kama instruments zinapatikana kwa biashara.
- Kagua ujumbe uliotangulia wa kukataliwa kutoka kwenye kumbukumbu au jarida.
Ikiwa bado utakumbana na hitilafu hii mara kwa mara, usisite kuwasiliana na Timu yetu ya usaidizi.