Ikiwa ungependa kuanza kutrade ukitumia terminali uliyochagua ya biashara lakini kitufe chako cha Order Mpya hakifanyi kazi, huenda imesababishwa na mojawapo ya hali zifuatazo:
- Hujaingia kwenye akaunti
- Umeingia kwenye akaunti kwa maelezo yasiyo sahihi
- Kiasi cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza kinasubiri kuanza kutrade
Hujaingia kwenye akaunti
Ikiwa haujaingia kwenye akaunti yako ya kutrade ya MetaTrader 4, kitufe cha Order mpya kitaonekana kutofanya kazi na hutaweza kutrade.
Ili uingie kwenye akaunti ya biashara:
- Nenda kwenye File > Login to Trade Account
- Weka nambari ya akaunti yako ya kutrade, nenosiri la akaunti yako ya kutrade na seva.
- Unaweza kupata nambari ya akaunti yako ya kutrade na seva katika Eneo la Binafsi chini ya Taarifa za akaunti.
- Bofya Login.
Ukiingia, utaweza kubofya kitufe cha Order Mpya na kutrade. Pia, unaweza kubofya mara mbili kwenye alama yoyote kwenye dirisha la taarifa za soko ili kutrade.
Umeingia kwenye akaunti ya biashara kimakosa
Hii ni hali ngumu, lakini tuko hapa kusaidia. Ukiingia kwenye akaunti yako ya kutrade ya MT4 ukitumia nenosiri lako la mwekezaji au nenosiri lako la ufikiaji wa kusoma pekee, utaweza kuona data ya biashara ya wakati halisi lakini hutakuwa na ufikiaji wa kufanya biashara wewe mwenyewe.
Unaweza kuthibitisha hili kwa haraka kwa kuangalia kwenye kichupo cha Jarida cha terminali yako ya biashara katika sehemu inayoonyesha ujumbe wa “biashara imezimwa - hali ya mwekezaji”.
Ikiwa ndivyo hali ilivyo, ingia tena kwa kutumia maagizo yaliyotolewa hapo awali. Fuata kiungo hiki ikiwa ungependa kubadilisha nenosiri la akaunti yako ya kutrade na ulitumie kuingia kwenye akaunti yako ya kutrade.
Kiasi cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa kwa mara ya kwanza kinasubiri kuanza kutrade
Kitufe cha Order Mpya kitaonekana kutofanya kazi na hakiwezi kutumika katika terminali ya biashara ya MetaTrader 5 ikiwa kiasi cha chini zaidi cha pesa zinazoweza kuwekwa kwenye akaunti hiyo ya kutrade ya MT5 hakijachakatwa. Pesa ulizoweka zinapochakatwa, kitufe cha Order Mpya kinafaa kufanya kazi na unaweza kuanza kutumia akaunti hiyo ya kutrade.