MetaTrader 4 (MT4) inapatikana kwa kompyuta ya mezani ya Windows, Android, na vifaa vya mkononi vya iOS. Makala haya yanaonyesha jinsi ya kutumia MT4 kwenye kifaa chako unachopendelea.
Kabla ya kusakinisha MT4, sharti ujue mahali unaweza kupata maelezo yako ya kuingia na seva ya akaunti yako ya kutrade kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
Kumbuka: Kwa akaunti za Pro, market execution itapatikana katika sarafu hizi za akaunti pekee USD, JPY, THB, CNY, IDR, VND.
Ikiwa ungependa kuchunguza majukwaa mengine ya biashara yanayopatikana, fahamu majukwaa ya biashara unayoweza kutumia kama vile Exness Trade, terminali ya biashara kwenye kifaa cha mkononi au Terminali ya Exness, terminali inayotumika kwa kivinjari kwa akaunti za kutrade za MT5 pekee.
- Kompyuta ya Mezani
- Android
- iOS
Jinsi ya kutumia MetaTrader 4 (Windows)
- Sakinisha MT4
- Ingia katika akaunti
- Kubadilisha akaunti
- Ongeza na uondoe instruments
- Kufungua orders
- Kufunga orders
- Pending orders
- Kubadilisha au kufuta orders
- Kufungua Jarida
- Kufungua Habari
Sakinisha MT4:
- Pakua programu ya MT4 kwenye tovuti ya Exness.
- Gusa Kubali kwenye ujumbe wa kukaribishwa kisha ubofye X ili Kufungua ujumbe wa akaunti ya demo.
- Ukurasa wa ingia kwenye akaunti iliyopo utaonyeshwa.
- Katika upau wa Tafuta Broker, weka “Exness Technologies Ltd” kisha uchague seva ya biashara inayofaa akaunti yako ya kutrade.
- Kwa wateja waliosajiliwa na Huluki yetu ya Kenya, tafadhali weka “Exness (KE) Limited”.
- Weka nambari yako ya akaunti ya kutrade na nenosiri la akaunti ya kutrade, kisha ubofye Ingia.
Akaunti ya kutrade huongezwa kwenye kichupo cha Akaunti.
Sakinisha MT4 kwenye Mac OS:
- Pakua MT4 kwenye tovuti ya Exness.
- Bofya mara mbili kwenye faili iliyopakuliwa ili kuanzisha usakinishaji wa MT4.
- Fuata vidokezo vilivyotolewa ili kusakinisha MT4 kwenye kifaa chako cha mezani.
- Weka “Exness Technologies Ltd” na uchague seva ya biashara inayofaa kwa akaunti yako ya kutrade. Bofya Inayofuata.
- Kwa wateja waliosajiliwa na huluki yetu ya Kenya, tafadhali weka “Exness (KE)Limited”
- Kisha, chagua Akaunti iliyopo ya kutrade na uweke nambari ya akaunti yako ya kutrade na nenosiri la akaunti ya kutrade, kisha ubofye Maliza.
- Akaunti ya kutrade huongezwa kwenye kichupo cha Akaunti.
Ingia katika akaunti
- Bofya Faili na uchague Ingia kwenye Akaunti ya Kutrade.
- Weka maelezo ya kuingia, Nenosiri na Seva ya akaunti yako ya kutrade, kisha ubofye Ingia.
- Taarifa hizi ziko kwenye Eneo lako la Binafsi (EB) la Exness. Maelezo yako ya kuingia kwenye MT4 na Seva yako huonyeshwa kwenye upande wa chini wa kadi za akaunti ya kutrade katika kichupo cha Akaunti zangu . Nenosiri lako ni nenosiri ambalo uliweka awali ulipofungua akaunti hii ya kutrade.
- Ukifanikiwa, utasikia sauti ya kengele ya uthibitisho kumaanisha kuwa sasa umeingia kwenye MT4 kwa kutumia akaunti yako ya kutrade.
Kubadilisha akaunti
- Ukiwa umeingia kwenye akaunti yako ya kutrade, bofya Faili > Ingia kwenye Akaunti ya Kutrade.
- Ingia kwa kutumia nambari ya akaunti yako nyingine ya kutrade, nenosiri na seva inayolingana; kisha ubofye Sawa. Unaweza kubadili haraka zaidi wakati ujao kwa kuweka tiki kwenye Save account information.
Ubadilishaji wa haraka
Unaweza kubadili kati ya akaunti zinazotumika za kutrade kwa kwenda kwenye Faili > Ingia kwenye Akaunti ya Kutrade - tumia menyu kunjuzi kwenye sehemu ya Kuingia ili kuchagua akaunti zozote za kutrade ulizoingia nazo awali.
Kumbuka: Huwezi kudhibiti akaunti nyingi za MT4 kwa wakati mmoja ukitumia MT4; ikiwa ungependa kufanya hivo, tunapendekeza MT4 MultiTerminal ambayo imeundwa kukidhi hitaji hili.
Ongeza na uondoe instruments
Ili uongeze:
- Bofya kulia kwenye dirisha la Taarifa za Soko.
- Chagua Alama.
- Chagua kutoka kwenye orodha ya vikundi vya alama vilivyoonyeshwa.
- Bofya kwenye instrument ili kuiongeza kwenye Taarifa za Soko na ubofye Funga.
Ili uondoe:
- Bofya kulia kwenye instrument katika Taarifa za Soko.
- Bofya Ficha.
Kufungua orders
Kuna njia 4 za kufungua order mpya:
- Bofya Order Mpya kwenye upau wa vidhibiti.
- Bofya F9 kwenye kibodi yako.
- Bofya kulia kwenye instrument ya biashara kwenye dirisha la Taarifa za Soko, kisha ubofye Order Mpya.
- Bofya mara mbili kwenye instrument ya biashara kwenye dirisha la Taarifa za Soko.
Mbinu hizi hufungua dirisha la Order Mpya.
- Kwenye dirisha la Order Mpya, chagua alama unayopendelea, ukubwa wa transaction, viwango vya Stop Loss (SL) na Take Profit (TP).
- Aina ya execution inapatikana chini ya Aina na hugunduliwa kiotomatiki na instrument iliyochaguliwa na aina ya akaunti ya kutrade.
- Bofya Sell by Market au Buy by Market ili kuweka order.
Kufunga orders
Kuna njia nyingi za kufunga order:
- Bofya mara mbili kwenye order ambayo ungependa kufunga kwenye kichupo cha Trade (kwenye sehemu ya Terminali), kisha ubofye Kitufe cha manjano cha Funga Kwa Soko.
- Bofya kulia kwenye order yako kwenye kichupo cha Trade, chagua Funga Order, na uthibitishe. Ukiwa na Biashara ya Mbofyo Mmoja inayotumika, order hiyo hufungwa kitufe cha Funga Order kinapochaguliwa.
- Bofya X kwenye upande wa kulia wa order kwenye kichupo cha Trade; hii hufunga order hiyo mara moja ikiwa Biashara ya Mbofyo Mmoja inatumika.
Tumia njia yoyote kati ya hizi kufunga orders.
Pending orders
Kuna aina 4 za pending order unazoweza kuchagua katika MT4 (Buy Limit, Sell Limit, Buy Stop na Sell Stop); Stop Loss na Take Profit zinaweza kuwekwa ili kufunga orders hizi kiotomatiki.
- Fungua dirisha la Order Mpya (F9).
- Chagua Alama, weka Kiwango cha order, na uchague Pending Order kwenye menyu kunjuzi ya Aina.
- Mipangilio ya Pending Order itaonekana. Chagua pending order unayopendelea kwenye menyu kunjuzi ya Aina, kisha uweke Bei na Tarehe ya mwisho wa matumizi unayopendelea.
- Kwa hiari, weka viwango vya Stop Loss (SL) na Take Profit (TP) hapo juu kama kawaida.
- Bofya Weka ili kuweka mipangilio ya pending order yako.
Kumbuka: Tarehe za mwisho wa matumizi ambazo zitakuwa wakati wa wikendi zitasababisha wakati wa order hiyo kuisha soko linapofungwa mwishoni wa wiki ya sasa (bila kujumuisha instruments za cryptocurrency).
Kubadilisha au kufuta orders
- Bofya kulia kwenye order kwenye kichupo cha Trade (kwenye sehemu ya Terminali).
- Bofya Rekebisha au Futa Order.
- Ili kurekebisha: rekebisha sehemu zinazoweza kurekebishwa, ikiwa ni pamoja na Bei, Stop Loss, Take Profit na Muda wa Mwisho wa Matumizi. Bofya Rekebisha ukishamaliza.
- Ili kufuta: bofya option ya Futa.
Kumbuka: Tafadhali fuata Viwango vya Kusitisha unapoweka mipangilio ya Pending orders (ikiwa ni pamoja na SL na TP).
Kufungua Jarida
- Bofya Faili na ubofye kwenye Fungua Folda ya Data.
- Bofya kwenye folda ya Kumbukumbu.
Kwa data kuhusu vitendo vilivyofanywa na Expert Advisors, huwa inahifadhiwa kwenye faili tofauti ya kumbukumbu. Ili kuipata:
- Bofya Faili na ubofye kwenye Fungua Folda ya Data.
- Bofya kwenye MQL4 kisha Kumbukumbu.
Ikiwa unahitaji kutuma mstari mmoja au zaidi kutoka kwa kumbukumbu zako za terminali, unaweza kuzinakili moja kwa moja kutoka MT4. Kufanya hivyo:
- Nenda kwenye kichupo cha Experts au Jarida (kulingana na aina ya kumbukumbu unazohitaji: Experts kwa faili za kumbukumbu za Expert Advisors, au Jarida kwa faili za kumbukumbu za kawaida).
- Bofya kulia kwenye mstari unaotaka na ubofye Nakili. Unaweza kuchagua mistari kadhaa kwa kubofya Ctrl+Shift kwenye kibodi.
- Baada ya kunakiliwa, unaweza kutuma taarifa hizo kwa Timu yetu ya Usaidizi kupitia Live chat au barua pepe support@exness.com
Kufungua Habari
- Katika upau wa vidhibiti, bofya Zana > Options.
- Katika kichupo cha Server chagua Enable News.
Kumbuka: Ikiwa unatumia akaunti za Demo au akaunti za Standard Cent, utaweza tu kuona kichwa cha habari, na sio makala yote.
Jinsi ya kutumia MT4 (Android)
- Kupakua na kuingia kwenye MT4
- Kubadilisha akaunti inayotumika ya kutrade
- Ongeza au uondoe instruments za biashara
- Kufungua orders
- Pending orders
- Funga au urekebishe orders
- Fungua chati za instruments
- Kubadilisha aina za chati
- Kubadilisha timeframe
- Kuongeza indicators
- Kufungua Jarida
- Kufungua Habari
- Arifa
- Arifa Maalum
Kupakua na kuingia kwenye MT4
- Pakua programu ya MT4 kwenye tovuti ya Exness.
- Bofya Kubali kwenye ujumbe wa kukaribisha kisha uguse X ili Kufungua ujumbe wa akaunti ya demo.
- Ukurasa wa ingia kwenye akaunti iliyopo utaonyeshwa.
- Katika upau wa Tafuta Broker, weka “Exness Technologies Ltd” kisha uchague seva ya biashara inayofaa akaunti yako ya kutrade.
- Kwa wateja waliosajiliwa na huluki yetu ya Kenya, tafadhali weka “Exness (KE)Limited”.
- Weka nambari yako ya akaunti ya kutrade na nenosiri la akaunti ya kutrade, kisha ubofye Ingia.
- Akaunti ya kutrade huongezwa kwenye kichupo cha Akaunti.
Kubadilisha akaunti
- Fungua MT4 na uchague Dhibiti Akaunti kwenye menyu kuu.
- Bofya akaunti ya kutrade ambayo ungependa itumike katika kichupo cha Akaunti, weka maelezo ya kuingia kwenye akaunti ya kutrade ikiwa utaombwa na kisha Ingia.
- Akaunti hiyo ya kutrade sasa inafanya kazi katika MT4.
Ongeza au uondoe instruments za biashara
Bofya aikoni ya Quotes iliyo upande wa chini kushoto wa skrini ili kuonyesha orodha chaguo-msingi ya instruments.
Bofya aikoni ya + kwenye kona ya juu kulia.
- Ili kuongeza: Chagua kikundi cha alama.
- Bofya instrument(s) ambazo ungependa kuongeza.
- Bofya kitufe cha Nyuma hadi utakaporejea kwenye kichupo cha Quotes.
Ili uondoe:
- Bofya aikoni ya penseli (juu kulia), kisha aikoni ya pipa.
- Chagua alama ambayo(ambazo) zinafaa kufutwa kwa kuweka alama kwenye visanduku.
- Bofya aikoni ya pipa tena ili kuthibitisha uondoaji.
- Bofya kitufe cha Nyuma ukishamaliza.
Kufungua orders
- Nenda kwa Quotes.
- Bofya instrument ambayo ungependa kutrade nayo kisha Order Mpya.
- Weka vigezo vya order yako (Stop Loss, Take Profit, Mkengeuko, n. k.)
- Ili kutekeleza market order sasa, bofya Nunua kwa Soko au Uza kwa Soko.
- Bofya Weka. Kisha utapokea arifa kuwa order imefunguliwa kwa mafanikio.
Pending orders
- Tafuta option ya Order Mpya.
- Bofya kwenye aina ya execution iliyoonyeshwa na uchague pending order.
- Weka vigezo vifuatavyo:
- Kiwango cha Order
- Bei ya pending order (utahitaji kuweka mipangilio ya bei ya ziada kwa Buy Stop Limit na Sell Stop Limit)
- Stop Loss (kwa hiari)
- Take Profit (kwa hiari)
- Muda wa mwisho wa matumizi
Kumbuka: Tarehe za mwisho wa matumizi ambazo zitakuwa wakati wa wikendi zitasababisha wakati wa order hiyo kuisha soko linapofungwa mwishoni wa wiki ya sasa (bila kujumuisha instruments za cryptocurrency).
Kumbuka: Kwenye dirisha la Order Mpya, menyu kunjuzi kwenye aikoni iliyo kwenye kona ya juu kulia itaorodhesha instruments zote zilizoongezwa kwenye kichupo chako cha Quotes; chagua instrument ili kuweka pending order.
Funga au urekebishe orders
- Bofya kwenye aikoni ya Trade.
- Bofya order ili kuona maelezo yake (Bei, S/L, T/P, Kitambulisho cha order, nk.).
- Bofya na ushikilie order, kisha ubofye Funga au Rekebisha order.
- Bofya Funga Order ili kufunga order.
- Badilisha mipangilio yoyote iliyoonyeshwa, kisha Ubofye Rekebisha.
- Utapokea arifa ya kuthibitisha hatua hiyo.
Fungua chati za instruments
- Nenda kwa Quotes.
- Bofya instruments, kisha uchague Fungua chati.
Kubadilisha aina za chati
- Bofya Menyu, kisha ubofye Mipangilio.
- Bofya Aina ya mstari.
- Chagua kutoka kwa aina tatu za chati za wakati halisi: chati ya Bar, Kinara, na ya mstari.
Kubadilisha timeframe
- Bofya kwenye chati.
- Chagua timeframe kwenye dirisha ibukizi. Timeframes 9 zinaweza kutumika: M1, M5, M15, M30, H1, H4, D1, W1 na MN.
Kuongeza indicators
- Ukiwa kwenye grafu, bofya aikoni ya ƒ kwenye menyu ya juu.
- Bofya ƒ+ karibu na Chati Kuu.
- Chagua indicator kutoka kwa zile zilizoonyeshwa.
- Weka mapendeleo yako kwa indicator iliyochaguliwa.
- Bofya Nimemaliza.
Kufungua Jarida
- Nenda kwenye Jarida (menu ya juu kushoto).
- Chagua tarehe na ubofye aikoni ya barua ili kuituma kupitia barua pepe kwa anwani unayopendelea ya barua pepe.
Kufungua Habari
- Nenda kwa Habari (menyu ya juu kushoto).
- Bofya ingizo lolote ili kuona habari za kiuchumi kutoka FXStreet kwa undani.
Kumbuka: Ikiwa unatumia akaunti za Demo au akaunti za Standard Cent, utaweza tu kuona kichwa cha habari, na sio makala yote.
Arifa
- Chagua Ujumbe na ubofye kitufe cha MQID.
- Nakili au uhifadhi kitambulisho.
- Kisha, ingia kwenye MT4 kwenye kifaa chako cha mezani.
- Fungua menyu ya Tools, na uchague Options.
- Chagua kichupo cha Arifa na ubofye Wezesha Arifa za Programu.
- Weka MQID unapoombwa na ubofye Jaribu.
- Unapaswa kupokea arifa ya programu iliyotumwa kwa sehemu yako ya Ujumbe ya MT4 kwenye kifaa chako cha Android.
Arifa Maalum
- Ingia kwenye MT4 kwenye kifaa chako cha mezani.
- Fungua kichupo cha Arifa kwenye dirisha la Terminali.
- Bofya kulia popote na uchague Create.
- Chagua Wezesha na uchague Arifa kwenye menyu kunjuzi ya Hatua.
- Weka mapendeleo kwenye arifa unayopendelea, kisha ubofye Jaribu.
- Unapaswa kupokea arifa maalum ya programu iliyotumwa kwenye sehemu ya Ujumbe ya MT4 kwenye kifaa chako cha Android.
- Bofya Sawa ili kukamilisha kuweka mipangilio ya arifa maalum.
Jinsi ya kutumia MetaTrader 4 (iOS)
- Kupakua na kuingia kwenye MT4
- Kubadilisha akaunti inayotumika ya kutrade
- Ongeza au uondoe instruments
- Kufungua orders
- Pending orders
- Funga au urekebishe orders
- Fungua chati za instruments
- Kubadilisha aina za chati
- Kubadilisha timeframe
- Kuongeza indicators
- Kufungua Jarida
- Kufungua Habari
- Arifa
- Arifa Maalum
Kupakua na kuingia kwenye MT4
- Pakua programu ya MT4 kutoka kwa Tovuti ya Exness.
- Fungua MT4 na uchague Mipangilio.
- Bofya Akaunti Mpya na uchague Ingia kwa akaunti iliyopo.
- Weka “Exness Technologies Ltd” kisha uchague seva ya biashara inayofaa kwa akaunti yako ya kutrade.
- Weka nambari ya akaunti yako ya kutrade na nenosiri la akaunti ya kutrade, kisha ubofye Ingia.
Kubadilisha akaunti
- Fungua MT4 na uende kwa Mipangilio.
- Bofya kishale kilicho karibu na akaunti iliyoonyeshwa juu ya ukurasa. Utaona akaunti unayofanyia biashara kwa sasa chini ya Current Account. Chini ya hapo, chini ya Trade Accounts utapata akaunti zingine zilizoongezwa kwenye programu.
- Bofya kwenye akaunti yoyote ya kutrade ili uingie.
- Akaunti hiyo ya kutrade sasa inatumika.
Ongeza au uondoe instruments
Ili uongeze:
- Nenda kwa Quotes.
- Bofya aikoni ya + kwenye kona ya juu kulia.
- Chagua kikundi cha alama.
- Bofya + ya kijani ili kuongeza instrument(s), kisha ubofye Nimemaliza.
Ili uondoe:
- Bofya aikoni ya penseli (kona ya juu kushoto) kisha uchague ishara.
- Bofya aikoni ya kikapu chenye rangi nyekundu (kona ya juu kulia).
- Bofya aikoni ya Kuhariri ili kurudi kwenye kichupo cha Quotes.
Kufungua orders
- Nenda kwa Quotes.
- Bofya alama ambayo ungependa kutrade kisha ubofye Trade.
- Weka kiwango cha biashara.
- Weka Stop Loss, na Take Profit pia kwa hiari.
- Bofya Uza kwa Soko ili kuuza au Nunua kwa Soko ili kununua.
- Arifa kwamba order imefunguliwa kwa mafanikio itatumwa.
Pending orders
- Fungua option ya Trade.
- Bofya kwenye aina ya execution iliyoonyeshwa na uchague pending order.
- Weka vigezo vifuatavyo:
- Kiwango cha Order
- Bei ya pending order (bei za ziada zinahitajika kwa Buy Stop Limit na Sell Stop Limit)
- Stop Loss (kwa hiari)
- Take Profit (kwa hiari)
- Muda wa mwisho wa matumizi
Kumbuka: Tarehe za mwisho wa matumizi ambazo zitakuwa wakati wa wikendi zitasababisha wakati wa order hiyo kuisha soko linapofungwa mwishoni wa wiki ya sasa (bila kujumuisha instruments za cryptocurrency).
Kumbuka: Kwenye dirisha la Order Mpya, menyu kunjuzi menyu kwenye aikoni iliyo kwenye kona ya juu kulia itaorodhesha instruments zote zilizoongezwa kwenye kichupo chako cha Quotes; chagua instrument ili kuweka pending order.
Funga au urekebishe orders
- Nenda kwa Trade.
- Bofya order ili kuona maelezo yake (S/L, T/P, Kitambulisho cha order, swap, nk.).
- Bofya na ushikilie order, kisha ubofye Funga au Rekebisha order.
- Ili kufunga: Bofya Funga ili kufunga order.
- Ili kurekebisha: Badilisha vigezo vya Stop Loss na/au Take Profit, kisha ubofye Rekebisha ili kuthibitisha.
- Arifa itatumwa ili kuthibitisha hatua hiyo.
Fungua chati za instruments
- Nenda kwa Quotes.
- Bofya instruments kisha ubofye Chati.
Kubadilisha aina za chati
- Bofya popote kwenye chati, kisha ubofye Mipangilio.
- Chagua aina ya chati. Unaweza kutumia aina tatu za chati za wakati halisi katika kituo cha simu: Chati ya Pau, Kinara na Chati ya laini.
- Bofya kitufe cha Nyuma.
Kubadilisha timeframe
- Bofya muda uliopo kwenye kona ya juu kushoto ya skrini.
- Chagua timeframe. Timeframes 9 zinaweza kutumika: M1, M5, M15, M30, H1, H4, D1, W1 na MN.
Kuongeza indicators
- Bofya alama ya ƒ kwenye chati yoyote.
- Chagua Dirisha Kuu au Dirisha la 1 la indicator na ubofye +.
- Chagua indicator. Unaweza kufikia indicators thelathini za kiufundi.
- Bainisha mipangilio ya indicator iliyochaguliwa.
- Bofya Nimemaliza.
Kufungua Jarida
- Nenda kwa Mipangilio na uchague Jarida.
- Chagua tarehe za kuonyeshwa kumbukumbu ya shughuli za kipindi chako. Unaweza kuituma kwa anwani yako ya barua pepe unayopendelea.
Kufungua Habari
- Nenda kwa Mipangilio.
- Chagua Habari ili kuonyeshwa uteuzi wa makala kutoka FXStreet. Bofya kila kipengee cha kibinafsi ili kufungua makala kamili.
Kumbuka: Ikiwa unatumia akaunti za Demo au akaunti za Standard Cent, utaweza tu kuona kichwa cha habari, na sio makala yote.
Arifa
- Nenda kwa Mipangilio.
- Chagua Gumzo na Ujumbe.
- Nakili au uhifadhi Kitambulisho cha MetaQuotes kilicho chini ya skrini.
- Kisha, ingia kwenye MT4 kwenye kifaa chako cha mezani.
- Fungua menyu ya Tools, na uchague Options.
- Chagua kichupo cha Arifa na ubofye Wezesha Arifa za Programu.
- Weka Kitambulisho cha MetaQuotes unapoombwa na ubofye Jaribu.
- Unapaswa kupokea arifa ya programu iliyotumwa kwa sehemu yako ya Ujumbe ya MT4 kwenye kifaa chako cha iOS.
Arifa Maalum
- Ingia kwenye MT4 kwenye kifaa chako cha mezani.
- Fungua kichupo cha Arifa kwenye dirisha la Terminali.
- Bofya kulia popote na uchague Create.
- Chagua Wezesha na uchague Arifa kwenye menyu kunjuzi ya Hatua.
- Weka mapendeleo kwenye arifa unayopendelea, kisha ubofye Jaribu.
- Unapaswa kupokea arifa maalum ya programu iliyotumwa kwenye sehemu ya Ujumbe ya MT4 kwenye kifaa chako cha iOS.
- Bofya Sawa ili kukamilisha kuweka mipangilio ya arifa maalum.