Ikiwa umewahi kuwasiliana na Usaidizi kuhusu masuala ya muunganisho wa intaneti, basi huenda umeombwa uwasilishe kumbukumbu zako za mtandao ili wataalamu wetu wazikague. Kumbukumbu za mtandao (Faili za .HAR) na kumbukumbu za dashibodi zinaweza kutusaidia kutatua hitilafu zinazoweza kutokea.
Makala haya yatatoa maelezo zaidi kuhusu faili za .HAR, na hatua zinazohitajika kwenye kivinjari chako ili kuzipakua.
- Kuhusu faili za .HAR
- Google Chrome
- Safari
- Mozilla Firefox
- Microsoft Edge
Kuhusu faili za .HAR
HAR (Muundo wa Kumbukumbu ya HTTP) ni umbizo la faili linalohifadhi data iliyotumwa kati ya kivinjari (mteja) na seva. Wakati mawasiliano kati ya mteja (mtumaji) na seva (mpokeaji) yanafanyika, faili za .HAR huhifadhi majibu ya HTTP na vichwa vya maombi.
Je, kwa nini ninahitaji faili za .HAR?
Faili za HAR huhifadhi taarifa za maombi yote ya tovuti yaliyotolewa na kichupo cha kivinjari ili kusaidia kutambua matatizo ya utendaji wa tovuti. Usaidizi unaweza kutumia faili za HAR kuondoa na kutambua matatizo ambayo yanaweza kuathiri uthibitishaji na matatizo ya utoaji wa ukurasa.
Pata maelezo ya jinsi ya kupakua kumbukumbu za mtandao kwa kivinjari chako kwa kuchagua mojawapo ya vichupo vilivyo hapo juu.
Google Chrome
- Fungua Tovuti ya Exness au Eneo la Binafsi (ikiwa linaweza kufikiwa).
- Bonyeza F12 kwa Windows au fn + F12 kwa iOS, au ufungue menyu ya kivinjari (menyu ya nukta 3) na uchague Zana zaidi kisha Zana za Wasanidi.
- Chagua kichupo cha Mtandao.
- Rudia hatua zilizosababisha tatizo hilo kichupo hiki kikiwa kimefunguliwa ili kuhifadhi data kwenye kichupo cha mtandao.
- Bofya kulia popote kwenye sehemu ya Jina ya kichupo cha mtandao na uchague Hifadhi zote kama HAR pamoja na maudhui.
- Hifadhi faili hiyo kwenye kifaa chako mahali ambapo ni rahisi kuipata.
- Wasilisha faili ya .HAR kwa Usaidizi kama unavyoombwa (kupitia barua pepe au kwa live chat).
Muhimu: ikiwa kivinjari chako kitafungua kichupo kipya bila kufungua zana za msanidi, sharti ufungue zana za msanidi (F12) kwenye kichupo kipya.
Safari
- Fungua Tovuti ya Exness au Eneo la Binafsi (ikiwa linaweza kufikiwa).
- Panua menyu kuu ya Safari na uchague Mipangilio.
- Fungua kichupo cha Mipangilio ya kina na uweke alama kwenye kisanduku ambacho kinaonyesha Onyesha vipengele vya wasanidi wa tovuti. Huhitaji kurudia hatua hii katika siku zijazo baada ya kuweka alama kwenye kisanduku hiki.
- Panua menyu ya Sanidi ambayo sasa inaonekana kwenye upau wa juu.
- Chagua Onyesha Dashibodi ya JavaScript kisha ufungue kichupo cha Mtandao.
- Rudia hatua zilizosababisha tatizo hilo kichupo hiki kikiwa kimefunguliwa ili kuhifadhi data kwenye kichupo cha mtandao.
- Bofya aikoni ya Hamisha kwenye sehemu ya juu ya kichupo hicho na uchague Hamisha HAR.
- Hifadhi faili hiyo kwenye kifaa chako mahali ambapo ni rahisi kuipata.
- Wasilisha faili ya .HAR kwa Usaidizi kama unavyoombwa (kupitia barua pepe au kwenye live chat).
Mozilla Firefox
- Fungua Tovuti ya Exness au Eneo la Binafsi (ikiwa linaweza kufikiwa).
- Bofya Ctrl + Shift + E au ufungue menyu ya kivinjari, chagua Zana Zaidi na Zana za Wasanidi wa Tovuti.
- Chagua kichupo cha Mtandao.
- Rudia hatua zilizosababisha tatizo hilo kichupo hiki kikiwa kimefunguliwa ili kuhifadhi data kwenye kichupo cha mtandao.
- Bofya kulia popote kwenye safuwima ya Faili na ubofye Hifadhi zote kama HAR.
- Hifadhi faili hiyo kwenye kifaa chako mahali ambapo ni rahisi kuipata.
- Wasilisha faili ya .HAR kwa Usaidizi kama unavyoombwa (kupitia barua pepe au kwenye live chat).
Microsoft Edge
- Fungua Tovuti ya Exness au Eneo la Binafsi (ikiwa linaweza kufikiwa).
- Bofya Ctrl + Shift + I au F12; vinginevyo fungua menyu ya kivinjari, chagua Zana Zaidi na Zana za Wasanidi.
- Chagua kichupo cha Mtandao (aikoni ya wifi).
- Rudia hatua zilizosababisha tatizo hilo kichupo hiki kikiwa kimefunguliwa ili kuhifadhi data kwenye kichupo cha mtandao.
- Bofya option ya hamisha HAR (mshale wa chini kwenye aikoni ya mstari); hii inapatikana kwenye upande wa juu wa kichupo.
- Hifadhi faili hiyo kwenye kifaa chako mahali ambapo ni rahisi kuipata.
- Wasilisha faili ya .HAR kwa Usaidizi kama unavyoombwa (kupitia barua pepe au kwenye live chat).