Mfumo wa MetaTrader 5 (MT5) unapatikana kwa kompyuta yako ya mezani ya Windows, vifaa vya mkononi vya Android na iOS. Makala haya yanaeleza jinsi ya kutumia MT5 kwenye kifaa unachopendelea.
Kabla ya kusakinisha MT5 kwenye kifaa unachopendelea, pata maelezo kuhusu mahali pa kupata maelezo ya seva na kuingia kwenye akaunti yako ya kutrade katika Eneo lako la Binafsi (EB).
Ikiwa ungependa kuchunguza terminali zingine za biashara zinazopatikana, fahamu majukwaa ya biashara unayoweza kutumia kama vile Programu ya Exness Trade, terminali ya biashara kwenye kifaa cha mkononi au Terminali ya Exness, terminali inayotumia kivinjari mahususi kwa akaunti za kutrade za MT5. Fuata kiungo ili upate maelezo kuhusujinsi ya kusanidi MetaTrader 5.
- Windows
- Android
- iOS
Jinsi ya kutumia MetaTrader 5 (Windows)
- Sakinisha MT5
- Ingia katika akaunti
- Kubadilisha akaunti
- Ongeza na uondoe instruments
- Kufungua orders
- Kufunga orders
- Pending orders
- Badilisha au ufute pending orders
Sakinisha MT5
- Pakua faili ya usakinishaji wa MT5.
- Fungua faili hiyo kwenye kivinjari chako au ubofye mara mbili faili hiyo ya usakinishaji kutokea mahali ambapo ilipakuliwa.
- Unaweza kurekebisha mahali unaposakinisha MT5 kwa kubofya Mipangilio kwa mapendeleo yako, au ubofye Inayofuata ili kukubaliana na Mkataba wa Leseni ya Mtumiaji na uendelee.
- Usakinishaji utakapokamilika, bofya Maliza na itafungua MT5 kiotomatiki.
- Kwa mchakato wako wa kuingia katika akaunti kwa mara ya kwanza: funga dirisha lenye kichwa “Fungua akaunti” kwa kubofya Ghairi.
Ingia katika akaunti
- Bofya Faili na uchague Ingia kwenye Akaunti ya Kutrade.
- Weka maelezo ya kuingia, Nenosiri na Seva ya akaunti yako ya kutrade, kisha ubofye Ingia.
- Taarifa hizi ziko kwenye Eneo lako la Binafsi (EB) la Exness. Maelezo yako ya kuingia kwenye MT5 na Seva yako huonyeshwa kwenye upande wa chini wa kadi za akaunti ya kutrade katika kichupo cha Akaunti zangu . Nenosiri lako ni nenosiri ambalo uliweka awali ulipofungua akaunti hii ya kutrade.
- Ikiwa huwezi kupata seva hiyo, nenda kwenye Faili > Fungua Akaunti. Tafuta Exness, kisha uchague Exness Technologies Ltd. kwenye orodha. Chagua seva yako kwenye orodha na ubofye Maliza.
- Ikifanikiwa, utasikia sauti ya kengele ya uthibitishaji. Sasa umeingia katika akaunti kwenye MT5 ukitumia akaunti yako ya kutrade.
Kumbuka: Kwa akaunti za chaguomsingi za MT5 zilizofunguliwa wakati wa usajili wa Exness, nenosiri la Eneo lako la Binafsi linaweza kutumika kuingia kwenye akaunti hiyo ya kutrade. Inapendekezwa kuwa ubadilishe nenosiri lako chaguo-msingi la biashara haraka uwezavyo.
Kubadilisha akaunti
- Ukiwa umeingia kwenye akaunti yako ya kutrade, bofya Faili > Ingia kwenye Akaunti ya Kutrade.
- Ingia kwa kutumia nambari ya akaunti yako nyingine ya kutrade, nenosiri na seva inayolingana; kisha ubofye Sawa. Unaweza kuharakisha ubadilishaji wa akaunti wakati ujao kwa kuweka tiki kwenye Hifadhi nenosiri.
Ubadilishaji wa haraka
Unaweza kubadili kati ya akaunti zinazotumika za kutrade kwa kwenda kwenye Faili > Ingia kwenye Akaunti ya Kutrade - tumia menyu kunjuzi kwenye sehemu ya Kuingia ili kuchagua akaunti zozote za kutrade ulizoingia nazo awali.
Ongeza na uondoe instruments
Ili uongeze:
- Bofya kulia kwenye dirisha la Taarifa za Soko.
- Chagua Alama.
- Chagua kutoka kwenye orodha ya vikundi vya alama vilivyoonyeshwa.
- Bofya mara mbili kwenye instrument ili kuziongeza kwenye Taarifa za Soko na ubofye Sawa.
Ili uondoe:
- Bofya kulia kwenye soko katika Taarifa za Soko.
- Bofya Ficha.
Kufungua orders
Kuna njia 4 za kufungua order mpya:
- Bofya Order Mpya kwenye upau wa vidhibiti.
- Bofya F9 kwenye kibodi yako.
- Kwenye dirisha la Taarifa za soko, bofya kulia kwenye instrument ya biashara ambayo ungependa kutrade na ubofye Order Mpya.
- Bofya mara mbili instrument ya biashara katika dirisha la Market Watch.
Mbinu hizi hufungua dirisha la Order Mpya.
- Kwenye dirisha ya Order Mpya, chagua alama na kiwango unachopendelea, pamoja na viwango vya Stop Loss na Take Profit kwa hiari.
Kumbuka: Kwa akaunti za Pro, unaweza kuchagua aina ya execution wakati akaunti inafunguliwa. Unaweza kuchagua kati ya Market execution au Instant execution. Market execution sasa inapatikana kwa sarafu 6 za akaunti; USD, JPY, THB, CNY, IDR, VND.
- Bofya Uza kwa Soko au Nunua kwa Soko ili kuweka order.
Kufunga orders
Kuna njia nyingi za kufunga order:
- Bofya mara mbili kwenye order ambayo ungependa kufunga kwenye kichupo cha Trade (kwenye sehemu ya Terminali), kisha ubofye Kitufe cha manjano cha Funga Kwa Soko.
- Bofya kulia kwenye order yako kwenye kichupo cha Trade, chagua Funga Order, na uthibitishe. Ukiwa na Biashara ya Mbofyo Mmoja inayotumika, order hiyo hufungwa kitufe cha Funga Order kinapochaguliwa.
- Bofya X kwenye upande wa kulia wa order kwenye kichupo cha Trade; hii hufunga order hiyo mara moja ikiwa Biashara ya Mbofyo Mmoja inatumika.
Tumia njia yoyote kati ya hizi kufunga orders.
Kufunga orders kwa sehemu fulani
- Bofya order mara mbili kwenye kichupo cha Trade ili kufungua dirisha la Order.
- Weka ukubwa wa kiwango ambacho ungependa kufunga kwenye sehemu ya kiwango.
- Bofya Funga.
Funga Yote kwa
Ili kufunga kikamilifu au kwa sehemu fulani hedged order:
- Bofya mara mbili kwenye hedged order kwenye kichupo chaTrade ili kufungua dirisha la Order.
- Chini ya Aina, chagua Funga Kwa, na kisha uchague order katika sehemu ambayo inaonekana.
- Bofya kitufe cha manjano cha Funga.
- Hedged orders sasa zimefungwa.
Kufunga nyingi
Kipengele hiki hukuruhusu kufunga orders nyingi kwa wakati mmoja.
- Bofya kwenye kichupo cha Trade na ubofye kulia kwenye mojawapo ya positions zilizofunguliwa kisha uchague Operesheni Nyingi. Utaona orodha ya options za kufunga orders nyingi:
- Funga Positions Zote: Hufunga positions zote zilizofunguliwa kwa instruments zote.
- Funga Positions Zinazopata Faida: Hufunga positions zote zinazopata faida.
- Funga Positions Zinazopata Hasara: Hufunga positions zote zinazopata hasara.
- Funga Positions za Uuzaji/Ununuzi: Hufunga positions zote zenye aina sawa ya order pekee.
- Funga Positions za “Alama”: Hufunga positions zote za alama/instrument sawa pekee.
- Funga Positions za “Aina” “Alama”: Hufunga positions zote zenye aina sawa ya order kwa alama/instrument sawa pekee.
- Funga kwa “Alama”: Hufunga positions ambazo ziko hedged kwa alama/instrument sawa kwa kutumia kipengele cha Funga Kwa.
Kumbuka: Wakati order ya kufungwa nyingi inatekelezwa, seva itatekeleza orders moja baada ya nyingine, ambayo inaweza kuchukua milisekunde chache kati ya kila order.
Pending orders
Kuna aina 6 za pending order unazoweza kuchagua katika MT5 (Buy Limit, Sell Limit, Buy Stop, Sell Stop, Buy Stop Limit na Sell Stop Limit). Ili kufunga position unaweza kutumia Stop Loss na Take Profit.
- Bofya aikoni ya Order Mpya kwenye upau wa vidhibiti ulio juu au ubofye Zana > Order Mpya.
- Chagua Alama, weka Kiwango, na ubainishe Aina yako ya pending order.
- Weka Bei ambayo ungependa, viwango vya Take Profit, Stop Loss, na Muda wa Mwisho wa Matumizi. Kumbuka kuwa kuweka mipangilio ya Take Profit, Stop Loss, na Muda wa Mwisho wa Matumizi ni kwa hiari.
- Bofya Weka ili kuweka mipangilio ya pending order yako.
Kumbuka: Ukichagua tarehe ya mwisho wa matumizi ambayo itakuwa mwishoni mwa wiki, muda wa order yako utaisha kabla ya soko kufungwa mwishoni mwa wiki ya sasa.
Badilisha au ufute pending orders
- Bofya kulia kwenye pending order katika kichupo cha Trade na ubofye Rekebisha au Futa.
- Ili kurekebisha: rekebisha Bei, Stop Loss, Take Profit na Muda wa mwisho wa matumizi na ubofye Rekebisha.
- Ili ufute: bofya kwenye chaguo la Futa.
Kumbuka: Tafadhali fuata Viwango vya Kusitisha unapoweka mipangilio ya Pending orders (pamoja na SL na TP).
Jinsi ya kutumia MetaTrader 5 (Android)
- Pakua na uingie katika akaunti ya MT5
- Ongeza akaunti za kutrade
- Kubadilisha akaunti
- Ongeza, ondoa na upange upya instruments
- Kufungua orders
- Pending orders
- Funga au urekebishe orders
- Kufungua Jarida
- Kufungua Habari
Pakua na uingie katika akaunti ya MT5
- Pakua programu ya MT5 kwenye Tovuti ya Exness.
- Fungua MT5 na uchague Dhibiti Akaunti kwenye menyu kuu.
- Bofya aikoni ya + na uchague Ingia katika akaunti iliyopo.
- Weka “Exness Technologies Ltd” kisha uchague seva ya biashara inayofaa kwa akaunti yako ya kutrade.
- Weka nambari yako ya akaunti ya kutrade na nenosiri la akaunti ya kutrade, kisha ubofye Ingia.
- Akaunti ya kutrade huongezwa kwenye kichupo cha Akaunti.
Kumbuka: Kwa wateja waliosajiliwa na Exness (KE) Limited (huluki yetu ya Kenya), tafadhali weka Exness (KE) Limited kama jina la seva.
Ongeza akaunti za kutrade
- Bofya Mipangilio kwenye kona ya juu kushoto na uchague Dhibiti Akaunti.
- Bofya aikoni ya + na uchague Ingia katika akaunti iliyopo.
- Weka Exness kwenye utafutaji wa jina la kampuni au seva na uchague Exness-Server.
- Weka nambari ya akaunti yako ya kutrade, nenosiri la akaunti ya kutrade, na seva sahihi, kisha uguse Ingia.
- Akaunti ya kutrade huongezwa kwenye kichupo cha Akaunti.
Kubadilisha akaunti
- Chagua Dhibiti Akaunti kwenye menyu kuu.
- Bofya akaunti ya kutrade ambayo ungependa kufanya itumike kwenye kichupo cha Akaunti, weka maelezo ya kuingia kwenye akaunti ya kutrade ikiwa yatahitajika, kisha Ingia.
- Sasa utakuwa umeingia kwenye MT5 kwa kutumia akaunti hiyo ya kutrade.
Ongeza, ondoa na upange upya instruments
- Bofya kwenye Quotes.
- Bofya kwenye aikoni ya +, na kisha utafute instrument kutoka kwa vikundi vilivyoonyeshwa.
- Bofya kwenye instruments zozote ambazo ungependa kuongeza, na vitaongezwa kwenye orodha iliyoonyeshwa katika Quotes.
Ili kupanga upya:
- Bofya aikoni ya penseli ili kufungua kipengele cha kuhariri ambapo unaweza kuhamisha instruments ili kuzipanga upya.
Ili uondoe:
- Bofya aikoni ya pipa ili uwezeshe kipengele cha kufuta.
- Chagua instruments kwa kutumia aikoni ya tiki mbili, au uguse instruments binafsi ili kuzichagua.
- Bofya aikoni ya pipa tena ili uthibitishe uondoaji.
Kufungua orders
- Nenda kwa Quotes.
- Bofya alama ambayo ungependa kutrade kisha uguse Order Mpya.
- Weka vigezo vya order yako (yaani Stop Loss, Take Profit, n.k.).
- Bofya Ununuzi au Uuzaji ili ufungue Market order.
- Bofya Weka. Kisha utapokea arifa kuwa order imefunguliwa kwa mafanikio.
Pending orders
- Tafuta option ya Order Mpya.
- Bofya kwenye aina ya execution iliyoonyeshwa na uchague pending order.
- Weka mipangilio ya vigezo vifuatavyo:
- Kiwango cha Order
- Bei ya pending order (utahitaji kuweka mipangilio ya bei ya ziada ya Buy Stop Limit na Sell Stop Limit)
- Stop Loss (kwa hiari)
- Take Profit (kwa hiari)
Kumbuka: Kwenye dirisha la Order Mpya, menyu kunjuzi menyu kwenye aikoni iliyo kwenye kona ya juu kulia itaorodhesha instruments zote zilizoongezwa kwenye kichupo chako cha Quotes; chagua instrument ili kuweka pending order.
Funga au urekebishe orders
- Nenda kwa Trade.
- Bofya order ili kuona maelezo yake (Bei, S/L, T/P, Kitambulisho cha order, nk.).
- Bonyeza na ushikilie order hiyo.
Ili urekebishe:
- Bofya Rekebisha position.
- Badilisha vigezo vya order na Ubofye Rekebisha baada ya kumaliza.
Ili ufunge:
- Bofya Funga position.
- Bofya Funga kwa Hasara/Faida ili kuthibitisha hatua inayofaa.
- Utapokea arifa order itakapofungwa.
Kufungua Jarida
- Nenda kwenye Jarida katika menyu ya juu kushoto.
- Chagua tarehe na ubofye aikoni ya barua ili kuituma kupitia barua pepe. Hakikisha kuwa umebadilisha anwani ya mpokeaji hadi support@exness.com
Kufungua Habari
- Nenda kwenye Habari kwenye menyu iliyo upande wa juu kushoto.
- Tazama habari za hivi punde za kiuchumi kutoka FXStreet. Unaweza pia kubofya kila kipengee ili kufungua makala kamili kwa kina.
Jinsi ya kutumia MetaTrader 5 (iOS)
- Pakua na uingie katika akaunti ya MT5
- Ongeza akaunti za kutrade
- Kubadilisha akaunti
- Ongeza, ondoa na upange upya instruments
- Kufungua orders
- Pending orders
- Funga au urekebishe orders
- Kufungua Jarida
- Kufungua Habari
Pakua na uingie katika akaunti ya MT5
- Pakua programu ya MT5 kwenye Tovuti ya Exness.
- Fungua MT5 na uchague Dhibiti Akaunti kwenye menyu kuu.
- Bofya aikoni ya + na uchague Ingia katika akaunti iliyopo.
- Weka “Exness” kisha uchague seva ya biashara inayofaa kwa akaunti yako ya kutrade.
- Weka nambari yako ya akaunti ya kutrade na nenosiri la akaunti ya kutrade, kisha ubofye Ingia.
- Akaunti ya kutrade huongezwa kwenye kichupo cha Akaunti.
Kumbuka: Kwa wateja waliosajiliwa na Exness (KE) Limited (huluki yetu ya Kenya), tafadhali weka Exness (KE) Limited kama jina la seva.
Ongeza akaunti za kutrade
- Fungua MT5 na uchague Mipangilio.
- Bofya Akaunti Mpya na uweke Exness Technologies Ltd” katika bar ya kutafutia. Chagua seva ya biashara inayofaa kwa akaunti yako ya kutrade.
- Weka nambari ya akaunti yako ya kutrade na nenosiri la akaunti ya kutrade, kisha ubofye Ingia.
Kubadilisha akaunti
- Fungua MT5 na uende kwenye Mipangilio.
- Bofya kishale kilicho karibu na akaunti iliyoonyeshwa juu ya ukurasa. Utapata akaunti zote ulizotumia kuingia kwenye programu.
- Bofya kwenye akaunti yoyote ili uingie katika akaunti.
- Sasa utakuwa umeingia kwenye MT5 kwa kutumia akaunti hiyo ya kutrade.
Ongeza, ondoa na upange upya instruments
Ili uongeze:
- Nenda kwa Quotes.
- Bofya kwenye upau wa utafutaji ili kufungua orodha ya vikundi vyote vya instruments zinavyopatikana kwa biashara.
- Bofya aikoni ya + kando ya instrument ambayo ungependa kuongeza na zitaongezwa kwenye orodha yako ya Quotes.
Ili uondoe:
- Bofya aikoni ya penseli na uchague instruments ambazo ungependa kuondoa.
- Bofya aikoni ya pipa.
Ili kupanga upya:
- Bofya aikoni iliyo upande wa kulia wa instrument.
- Buruta instrument kulingana na chaguo lako.
Kufungua orders
- Nenda kwa Quotes.
- Bofya instrument ambayo ungependa kutrade, kisha uguse Trade.
- Weka vigezo vya order yako (yaani Kiwango, Stop Loss, Take profit, n.k.)
- Bofya Ununuzi au Uuzaji.
Pending orders
- Tafuta option ya Trade.
- Bofya kwenye aina ya execution iliyoonyeshwa na uchague pending order.
- Baada ya kuchagua pending order, weka mipangilio ya vigezo vifuatavyo:
- Kiwango cha Order
- Bei ya pending order (utahitaji kuweka mipangilio ya bei ya ziada ya Buy Stop Limit na Sell Stop Limit)
- Stop Loss (kwa hiari)
- Take Profit (kwa hiari)
- Muda wa mwisho wa matumizi
Kumbuka: Kwenye dirisha la Order Mpya, menyu kunjuzi kwenye aikoni iliyo kwenye kona ya juu kulia itaorodhesha instruments zote ambazo zimeongezwa kwenye kichupo chako cha Quotes. Unaweza kuchagua instrument ili kuweka pending order.
Funga au urekebishe orders
- Nenda kwa Trade.
- Bofya order ili kuona maelezo yake (Bei, Stop Loss, Take Profit, Kitambulisho cha order, n. k.).
Ili urekebishe:
- Bofya Rekebisha position na uweke mipangilio ya vigezo ambavyo ungependa (Stop Loss na Take Profit).
Ili ufunge:
- Ikiwa ungependa kufunga order, bofya Funga position.
- Thibitisha bei na ubofye Funga.
- Utapokea arifa kwamba order imefungwa.
Kufungua Jarida
- Nenda kwa Mipangilio.
- Chagua Jarida ili kuonyeshwa kumbukumbu ya shughuli za kipindi chako.
Kufungua Habari
- Nenda kwa Mipangilio.
- Chagua Habari ili kuonyeshwa uteuzi wa makala kutoka FXStreet. Unaweza pia kubofya kila kipengee ili kufungua makala kamili kwa kina.