Hatua zinazohitajika ili kurejesha nenosiri hutegemea aina ya nenosiri ambalo ungependa kurejesha:
Nenosiri la Eneo la Binafsi (EB)
Hili ndilo nenosiri linalotumiwa kuingia kwenye Eneo lako la Binafsi(EB).
- Tembelea exness.com na ubofye Ingia.
- Chagua Nimesahau nenosiri langu.
- Weka anwani ya barua pepe iliyotumiwa kujisajili katika Exness na ubofye Endelea.
- Kulingana na aina yako ya usalama, sharti uthibitishe hatua ya kurejesha nenosiri lako kabla ya kuendelea. Bofya Thibitisha.
- Unda nenosiri jipya, ukifuata masharti ya nenosiri halali.
- Nenosiri lako jipya sasa limewekwa. Unahitaji tu kulitumia wakati wa kuingia ili kumaliza.
Unaweza kuhitajika kukamilisha captcha ili kuendelea; kuweka captcha isiyo sahihi mara nyingi kunaweza kusababisha ukurasa wa kuweka upya nenosiri kusitishwa kwa saa 24.
Nenosiri la biashara
Nenosiri hili hutumika kuingia kwenye jukwaa la biashara kwa akaunti maalum ya kutrade.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB) na ubofye aikoni ya nukta 3 kando ya akaunti yoyote ya kutrade katika Akaunti Zangu.
- Chagua Badilisha nenosiri la biashara.
- Weka nenosiri la kipekee, ukifuata masharti ya nenosiri yaliyoonyeshwa kwenye skrini. Ukiweka nenosiri sawa na nenosiri lako la biashara, halitakubaliwa.
- Bofya Thibitisha ukishamaliza.
Nenosiri la ufikiaji wa kusoma pekee
Nenosiri hili huruhusu ufikiaji mdogo kwa akaunti ya biashara kwa wahusika wengine, na biashara zote zimezimwa.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB) na ubofye aikoni ya nukta 3 kando ya akaunti yoyote ya kutrade katika Akaunti Zangu.
- Chagua Wekaufikiaji wa kusoma pekee.
- Weka nenosiri la kipekee, ukifuata masharti ya nenosiri yaliyoonyeshwa kwenye skrini. Ukiweka nenosiri sawa na nenosiri lako la biashara, halitakubaliwa.
- Bofya Thibitisha ukishamaliza.
- Nenosiri lako la ufikiaji wa kusoma pekee sasa limebadilishwa.