Je, kwa nini hili lilitokea?
-
Kufunga orders zilizofunguliwa wakati masoko yamefungwa
Ukijaribu kufunga order iliyofunguliwa wakati wa wikendi au wakati wa mapumziko ya kila siku ya instrument ya biashara, hutaweza kuifunga hadi soko lifunguliwe tena.
-
Hitilafu za onyesho na/au matatizo ya muunganisho
Hitilafu ya muonekano au matatizo ya muunganisho yanaweza kufanya order iliyofunguliwa ionekane kama haitafungwa.
-
Mapendeleo ya biashara ya mbofyo mmoja
Ikiwa umezoea kutrade kwa kutumia mapendeleo haya, unaweza kutarajia order kufungwa papo hapo.
-
Hedged orders
Hedged orders zinaweza kuzuia order kufungwa kutokana na masharti ya juu ya margin. Upande mmoja wa hedged order unapofungwa, order iliyobaki inaweza kuchukuliwa kama order mpya iliyofunguliwa. Masharti ya margin ya order iliyobaki yanapokokotolewa upya, yanaweza kuzuia kufungwa kutokana na free margin inayopatikana kutototosha
Jinsi ya kutatua tatizo hili?
-
Kufunga orders zilizofunguliwa wakati masoko yamefungwa
- Ili kutatua tatizo hili, subiri hadi soko lifunguliwe tena kwa instrument yako ya biashara na kisha ujaribu kufunga order hiyo.
-
Hitilafu za onyesho na/au matatizo ya muunganisho
- Ili kutatua tatizo hili, funga terminali yako ya biashara kabisa, kisha uifungue tena ili kuona kama order hiyo bado imefunguliwa.
-
Mapendeleo ya biashara ya mbofyo mmoja
- Ili kutatua tatizo hili, angalia mapendeleo ya terminali yako ya biashara kwa biashara ya mbofyo mmoja; ikiwa mpangilio huu umezimwa, huenda ukahitaji kuthibitisha hatua ya kufunga order.
-
Hedged orders
- Ili kutatua tatizo hili, thibitisha kuwa free margin yako inayopatikana inatosha kufunga order hiyo kisha ujaribu tena.
Tatizo hilo likiendelea, fungua tikiti katika kituo cha usaidizi kwa usaidizi.