MultiTerminal ni jukwaa la biashara lililotengenezwa na MetaQuotes Software kwa ajili ya udhibiti wa akaunti nyingi za kutrade kwa wakati mmoja, hata kwa aina za akaunti zinazotofautiana.
Akaunti za kutrade za MetaTrader 4 pekee ndizo zinazoweza kutumika katika MultiTerminal, na inaweza kusakinishwa tu kwenye Windows OS.
Tofauti kubwa zaidi kati ya MetaTrader 4 na MultiTerminal ni kuwa MultiTerminal hukuruhusu kutrade kwa kutumia hadi akaunti 128 real au akaunti 10 za demo kwa wakati mmoja (kwenye seva ile ile ya biashara) ilhali hii haiwezi kufanywa katika MetaTrader 4. Tazama ulinganisho zaidi hapa chini:
MT4 | MultiTerminal | |
Chati |
✓ |
✕ |
Biashara ya kiotomatiki |
✓ | ✕ |
Toleo la kifaa cha mkononi/Tovuti |
✓ | ✕ |
MultiTerminal haipendekezwi kwa kutrade ukiwa na akaunti chache za kutrade, lakini hutoa urahisi usio na kifani kwa wasimamizi wa akaunti.
- Usakinishaji
- Kuingia kwenye akaunti
- Udhibiti wa akaunti
- Ugawaji wa lot
- Orders zilizofunguliwa
- Udhibiti wa order
Jinsi ya kutumia MultiTerminal
Mwongozo huu wa video unaonyesha jinsi ya kusakinisha MultiTerminal na kuingia.
Usakinishaji
Ili kusakinisha MultiTerminal, faili ya programu sharti ipakuliwe kwanza. Bofya kiungo cha moja kwa moja kilicho hapa chini ili kuipakua, au tembelea tovuti ya Exness ili kupata faili hiyo chini ya Majukwaa > MetaTrader 4.
Anzisha programu hiyo, kwa kufuata maagizo kwenye skrini ili kusakinisha MultiTerminal.
Kuingia kwenye akaunti
Unaweza kuingia kwenye MultiTerminal kwa kutumia akaunti nyingi za kutrade za MT4 katika seva ile ile ya biashara Aina yoyote ya akaunti ya MT4 inaweza kutumika. Fuata hatua zilizo hapa chini kila wakati unapotaka kuongeza akaunti ya kutrade.
- Sakinisha MultiTerminal.
- Bofya Ghairi unapoombwa kufungua akaunti mpya.
- Fungua Zana > Options na uchague seva iliyotengewa akaunti yako ya kutrade kwenye menyu kunjuzi ya Seva. Bofya Sawa ukishamaliza.
Fuata kiungo ili kupata maelezo ya jinsi ya kupata seva ya akaunti ya kutrade.
- Fungua Faili > Akaunti Mpya na uweke maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako ya kutrade.
- Rudia hatua ya 4 ili kuongeza akaunti zaidi za kutrade zinazolingana na seva ya sasa ya biashara iliyowekwa.
- Rudia hatua ya 3 ili kubadilisha seva ya sasa ya biashara (akaunti za kutrade za seva zingine zitafichwa hadi zirudishwe kwenye seva yao iliyowekwa).
Ukiwa umeingia kwa kutumia akaunti nyingi za kutrade, uko tayari kupata maelezo zaidi kuhusu udhibiti wa akaunti.
Udhibiti wa akaunti
Kumbuka taarifa zifuatazo kuhusu udhibiti wa akaunti:
- Seva ya biashara ya akaunti ya kutrade ni muhimu sana, kwa kuwa ni akaunti za kutrade kutoka kwa seva sawa ya biashara pekee zinazoweza kudhibitiwa kwa wakati mmoja. Pata maelezo zaidi kuhusu seva za biashara.
- Unapobadilisha seva ya biashara iliyowekwa kwenye MultiTerminal, kuingia kwenye akaunti zote za kutrade za seva zingine za biashara kutafichwa hadi seva zao ziwekwa tena.
- Akaunti za kutrade za MT4 pekee ndizo zinazoweza kutumika, lakini aina yoyote ya akaunti inayoweza kutumika kwa MT4 inaweza kutumiwa kuingia kwa wakati mmoja; kwa mfano akaunti ya Standard ya MT4 na akaunti ya Pro ya MT4 zinaweza kudhibitiwa kwenye MultiTerminal kwa wakati sawa.
- Viambishi tamati vya instrument vya aina za akaunti bado vinatumika, yaani EURUSDm na EURUSD huainishwa kama instruments tofauti kwa hivyo haziwezi kufanyiwa trade kwa wakati mmoja. Pata maelezo zaidi kuhusu viambishi tamati vya akaunti.
Ugawaji wa lot
Ugawaji wa lot unarejelea usambazaji wa kiwango cha order kwa akaunti nyingi za kutrade. MultiTerminal hutoa mipangilio mbalimbali ya ugawaji wa lots unayoweza kuchagua.
- Kiwango kilichobainishwa awali: njia hii huruhusu ugawaji wa wewe mwenyewe wa idadi ya lots kwa kila order.
- Kiwango cha jumla kwa kila order: njia hii hutumia kiwango kilichowekwa kwa kila order. Kwa mfano, ikiwa 0.5 imebainishwa kwa akaunti 3 za kutrade, order ya lots 0.5 hufunguliwa kwa kila akaunti ya kutrade.
- Sehemu sawa: njia hii hugawanya kiwango kilichowekwa kati ya akaunti nyingi za kutrade. Kwa mfano, kiwango kilichowekwa cha lot 1 kati ya akaunti 3 za kutrade kitafungua order ya lots 0.33 kwa kila akaunti ya kutrade.
- Kwa uwiano wa equity: njia hii hupima uwiano wa equity kwa kila akaunti ya kutrade; kadiri equity ya akaunti ya kutrade ilivyo juu, ndivyo kiwango cha lots kitakachokabidhiwa kwa akaunti hiyo ya kutrade kinavyokuwa juu. Tazama jedwali linaloonyesha njia hii ya ugawaji.
Kwa order ya lots 3, yenye equity ya jumla ya USD 3 381.98 katika akaunti 3 za kutrade.
Jumla | Akaunti A | Akaunti B |
Akaunti C |
|
Equity | USD 3 381.98 | USD 943.57 | USD 940.19 | USD 1,498.22 |
Uwiano |
100% |
27.9% | 27.8% | 44.3% |
Sehemu | sehemu 3 | lot 0.84 | lot 0.83 | lot 1.33 |
- Kwa uwiano wa free margin: njia hii huchangia free margin inayopatikana kwa kila akaunti ya kutrade wakati wa kugawa lots; kadiri free margin inayopatikana inakuwa juu, ndivyo kiwango cha lots kwa kila akaunti ya kutrade kinakuwa kikubwa. Tazama jedwali linaloonyesha njia hii ya ugawaji.
Kwa order ya lots 3, yenye jumla ya free margin ya USD 1 804 katika akaunti 3 za kutrade.
Jumla | Akaunti A | Akaunti B | Akaunti C | |
Free margin | USD 1 804.00 | USD 541.20 | USD 180.40 | USD 1,082.40 |
Uwiano | 100% | 30% | 10% | 60% |
Sehemu | lots 3 | lot 0.9 | lot 0.3 | lot 1.8 |
Tafadhali kumbuka kuwa ugawaji wa lot hufanya kazi tu ikiwa kuna funds za kutosha kwa margin na spread kwenye akaunti yako.
Orders zilizofunguliwa
Kufungua orders kwenye MultiTerminal kunawezekana kwa market orders na pending orders. Fuata hatua zilizo hapa chini kwa kila aina ya order, ukizingatia margin inayohitajika na/au spread, na pia mipangilio ya take profit na stop loss inayohitajika kwa pending orders.
Market orders
- Bofya mara mbili kwenye instrument ya biashara kwenye dirisha la Taarifa za Soko ili kufungua dirisha la order.
- Jaza sehemu zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na:
- Alama: instrument ya biashara
- Jumla ya kiwango: kiwango cha lots kwa order hiyo (haihitajiki kwa aina ya ugawaji wa kiwango kilichobainishwa awali )
- Ugawaji wa lot: chagua njia ya ugawaji wa lot
- Take Profit (TP): kiasi cha faida kilichowekwa ambacho hufunga order kiotomatiki
- Stop Loss (SL): kiasi cha hasara kilichowekwa ambacho hufunga order kiotomatiki
- Maoni: dokezo hili huongezwa kwa order, lakini halirekebishi masharti yoyote ya order
- Bofya Nunua kwa Soko au Uza kwa Soko, kisha Sawa ili kuthibitisha taarifa ulizoweka na ufungue order.
Orders huonekana kwenye kichupo cha Orders, ambapo utendaji wao hufuatiliwa.
Pending Orders
- Fungua kichupo cha Pending kwenye MultiTerminal.
- Jaza sehemu zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na:
- Alama: instrument ya biashara
- Jumla ya kiwango: kiwango cha lots kwa order hiyo (haihitajiki kwa aina ya ugawaji wa kiwango kilichobainishwa awali )
- Ugawaji wa lot: chagua njia ya ugawaji wa lot
- Bei ya kufunguliwa: bei ambayo pending order hii itafunguliwa
- Aina: aina ya pending order, yaani buy stop, buy limit, sell stop, sell limit
- Take Profit (TP): kiasi cha faida kilichowekwa ambacho hufunga order kiotomatiki
- Stop Loss (SL): kiasi cha hasara kilichowekwa ambacho hufunga order kiotomatiki
- Maoni: dokezo hili huongezwa kwa order, lakini halirekebishi masharti yoyote ya order
- Tarehe ya mwisho wa matumizi: pending order hii itaondolewa ikiwa masharti haya hayatatimizwa kufikia tarehe iliyowekwa
- Bofya Weka ili kufungua pending order kwa taarifa zilizowekwa.
Orders zilizofunguliwa kwa pending order zitaonekana kwenye kichupo cha Orders.
Kwa nini siwezi kubofya Weka kwa pending order yangu?
Angalia thamani zilizowekwa za SL au TP (ikiwa zipo) kwani zinaweza kuwa batili. Kwa Buy Stop na Limit orders sharti SL iwe chini, na TP iwe juu, ya bei ya ufunguzi. Kwa Sell Stop na Limit orders sharti TP iwe juu, na SL iwe chini, ya bei ya ufunguzi. Pia thibitisha kuwa SL/TP iliyowekwa ni halali kulingana na stop level ya instrument hiyo.
Udhibiti wa order
Udhibiti wa order unajumuisha kufunga na kurekebisha orders zinazotumika, na kufuta pending orders.
Kufunga orders
- Fungua kichupo cha Funga kwenye MultiTerminal.
- Chagua orders ambazo ungependa kufunga au funga zote kwa kutochagua yoyote, kisha ubofye Funga.
- Bofya Sawa ili kuthibitisha.
Orders zilizofungwa huonekana kwenye kichupo cha Historia.
Kwa orders za kurekebisha, kipengele cha Funga Kwa au Funga Nyingi Kwa ni muhimu. Rejelea mada za usaidizi zinazopatikana kwenye MultiTerminal ili kupata maelezo zaidi kuhusu vipengele hivi; bofya Usaidizi kwenye menyu ya juu.
Kurekebisha orders
Fungua kichupo cha Rekebisha ili udhibiti kwa urahisi orders zilizofunguliwa na pending orders.
Market orders:
Unaweza chagua kufanya mabadiliko kwa orders zote, au kuchagua orders kwa kuweka alama/kuondoa alama kwenye visanduku vilivyo kando ya orders hizo. Mipangilio ya stop loss (SL) na take profit (TP). inaweza kutumika baada ya kubofya Sawa.
Ujumbe wa hitilafu wa S/L Batili au T/P Batili utaonekana ikiwa viwango vya SL au TP vimekaribiana sana na bei ya sasa ya soko. Rekebisha SL na TP yako kisha ujaribu tena ili kurekebisha hitilafu hii.
Pending orders:
Bei ya kufunguliwa na tarehe ya mwisho wa matumizi kwa pending orders zinaweza kubadilishwa:
- Weka alama kwenye kisanduku cha Bei ya Kufunguliwa na uweke bei mpya ya pending orders zako
- Ili kubadilisha tarehe ya mwisho wa matumizi, weka alama kwenye kisanduku cha Tarehe ya mwisho wa matumizi na ubainishe tarehe mpya ya mwisho wa matumizi
- Bofya Rekebisha baada ya kubainisha mabadiliko ambayo ungependa kufanya, na kisha ubofye Sawa