WebTerminal ni jukwaa la biashara linalotumika kwenye kivinjari kilichotengenezwa na MetaQuotes Software linaloweza kutumia akaunti za kutrade za MetaTrader 4 na 5. Hakuna usakinishaji unaohitajika na vipengele vyote vya msingi vya kutrade vinavyotarajiwa kwa jukwaa la biashara vipo, na kuifanya kuwa option rahisi ya kuanza kutrade haraka.
Tazama hapa chini kwa ulinganisho wa WebTerminal na terminali za biashara zinazotumika kwenye kompyuta ya mezani:
WebTerminal | Kompyuta ya Mezani | |
---|---|---|
Hakuna usakinishaji unaohitajika | ✅ | ❌ |
Expert advisors na scripts | ❌ | ✅ |
Indicators | ✅ | ✅ |
Trailing stop | ❌ | ✅ |
Ishara | ❌ | ✅ |
Hakuna hitilafu za terminali | ✅ | ❌ |
WebTerminal inapendekezwa kwa traders ambao wanapendelea kufanya biashara kwa urahisi kwenye kivinjari chao cha tovuti.
Jinsi ya kutumia WebTerminal
Video hii itakuonyesha jinsi ya kuingia kwenye WebTerminal na kutrade.
Kuingia
Ili kufungua WebTerminal, bofya tu kitufe kilicho hapa chini kwenye kivinjari chako unachopendelea ili kupelekwa kwenye skrini ya kuingia.
Chagua kichupo cha MetaTrader 4 au MetaTrader 5, kisha ubofye Endelea. MetaTrader 5 inahitaji seva ya akaunti ya kutrade katika hatua hii (ambayo haiwezi kubadilishwa kwenye skrini ya kuingia).
Kwa MetaTrader 4:
- Jaza fomu na taarifa zifuatazo:
- Maelezo ya kuingia: nambari yako ya akaunti ya kutrade
- Nenosiri: nenosiri lako la akaunti ya kutrade
- Seva: seva ya akaunti hiyo ya kutrade
Bofya Sawa baada ya kuweka taarifa hizi.
- Sauti ya kengele itathibitisha kuwa sasa umeingia kwa kutumia akaunti yako ya kutrade ya MT4.
Kwa MetaTrader 5:
- Bofya Kubali ili kuthibitisha Onyo lililoonyeshwa.
- Jaza fomu na taarifa zifuatazo:
- Maelezo ya kuingia: nambari yako ya akaunti ya kutrade
- Nenosiri: nenosiri lako la akaunti ya kutrade
Bofya Unganisha kwenye akaunti baada ya kuweka taarifa hizo.
- Jukwaa la biashara litapakia kwenye kivinjari chako; umeingia kwa kutumia akaunti yako ya kutrade ya MT5.
Ni akaunti za kutrade za MT5 pekee kwenye seva maalum zinazoweza kutumiwa kuingia kwa aina hii ya WebTerminal. Fungua aina mpya ya WebTerminal na ufuate hatua hizo tena ili kuingia kwa kutumia akaunti ya kutrade ya MT5 kwa kutumia seva tofauti.
Kubadili akaunti kwa haraka
Kwa akaunti za kutrade za MT4, kipengele cha kubadili haraka hukuruhusu kubadili kati ya akaunti za kutrade ambazo zimetumiwa kuingia kwenye WebTerminal bila kuhitaji maelezo ya kuingia.
Bofya Faili > Badili utumie Akaunti na uchague kutoka kwa akaunti zozote za kutrade ambazo zimetumiwa kuingia hapo awali.
Kusanidi
Ingawa WebTerminal inatumika kwa kivinjari, bado ina mipangilio na mapendeleo kamili na muhimu unayoweza kutumia. Kwanza, hebu tuchanganue madirisha muhimu zaidi yaliyoonyeshwa:
- Taarifa za soko hukuonyesha instruments zinazopatikana za biashara, bei zao za wakati halisi, na spread.
- Chati huonyesha utendaji wa instrument inayotumika ya biashara kwa muda fulani.
- Kisanduku cha zana kina vichupo vitatu: Trade, ambapo unaweza kuona orders zako zilizofunguliwa kwa sasa, Historia, ambapo unaweza kuona orders zilizofungwa na operesheni za salio, na Jarida, ambapo unaweza kupata taarifa za terminali (huonyeshwa kama aikoni kwenye akaunti za kutrade za MT5).
Taarifa za Soko
Utaona seti ya instruments chaguomsingi za biashara, lakini zaidi zinaweza kuongezwa kwa kufuata hatua zifuatazo:
Kwa MetaTrader 4:
- Bofya kulia popote kwenye dirisha, na uchague Symbols.
- Bofya kikundi cha instrument ili kupanua uteuzi wake. Instruments zenye aikoni ya manjano tayari zimeonyeshwa, aikoni zenye rangi ya kijivu zimefichwa.
- Bofya mara mbili ili kuongeza au kuondoa instrument kwenye dirisha la Taarifa za soko. Vitufe vya Onyesha na Ficha hufanya kazi kwa njia sawa.
- Ukimaliza, bofya Close.
Kwa MetaTrader 5:
- Bofya upau wa Alama ya Utafutaji ili kuonyesha orodha ya vikundi vya instruments.
- Chagua kutoka kwa vikundi vya instrument vilivyoonyeshwa, au uweke msimbo wa instrument, yaani USDGBP, STOXX50, nk.
- Bofya aikoni ya + ili kuongeza instrument au ubofye aikoni yoyote ya ✓ ili kuondoa instrument.
- Bofya aikoni ya ✕ kwenye upau wa Alama ya Utafutaji ili kurudi kwenye dirisha la Taarifa za Soko.
Bofya kulia kwenye instrument yoyote ili kuonyesha mipangilio na vipimo vyake; hii hutumika kwa akaunti za kutrade za MT4 na MT5.
Dirisha la Chart
Fungua chati ya instrument kwa kuiburuta kutoka kwa dirisha la Taarifa za Soko (MT4), au kubofya kwenye instrument kwenye dirisha la Taarifa za Soko (MT5).
Kuna aina tatu za chati zinazopatikana ambazo unaweza kuchagua kutoka: chati ya Bar, Vinara na chati ya Mstari. Unaweza kubadili kwa urahisi kati ya chati hizi kwenye menyu.
Timeframes zinaweza kubadilishwa kwa chati yako kwa kuchagua moja kwenye vitufe katika sehemu ya kichwa, yaani, M1 (dakika 1), H4 (saa 4), W1 (wiki 1), nk.:
Ili kubadilisha mipangilio ya rangi ya chati, bofya-kulia kwenye chati, bofya Sifa, na kisha uchague mojawapo ya mipango ya rangi (MT4), au ufungue menyu kuu na uchague Violezo vya rangi, kisha uchague kutoka kwa options zilizoonyeshwa (MT5).
-
MT4:
- Nyeusi kwenye Nyeupe
- Manjano kwenye Nyeusi
- Kijani kwenye Nyeusi.
-
MT5:
- Kijani & Nyekundu
- Samawati & Nyekundu
- Nyeusi & Nyeupe
- Isiyo na Mkolezo Wowote
Ukiwa na WebTerminal iliyosanidiwa, unaweza kufungua orders.
Orders zilizofunguliwa
Market orders na pending orders zinaweza kufunguliwa kwenye WebTerminal.
Market order
- Bofya mara mbili kwenye instrument ya biashara kwenye dirisha la Taarifa za Soko.
- Bainisha Kiwango katika lots.
- Chagua Market Execution au Instant Execution (upatikanaji unategemea aina ya akaunti yako) kwenye menyu kunjuzi ya Aina.
- Bainisha viwango vya stop loss (SL) na take profit (TP) vya order yako kwa hiari; unaweza kuhariri viwango hivo baada ya order kufunguliwa.
- Bofya Uuzaji au Ununuzi (maandishi kamili yanaweza kutofautiana kulingana na aina ya order execution).
Pending order
- Bofya mara mbili kwenye instrument ya biashara kwenye dirisha la Taarifa za Soko.
- Bainisha Kiwango katika lots.
- Kwa MT4: chagua Pending order kwenye uteuzi katika menyu kunjuzi ya Aina kisha uchague kwenye menyu kunjuzi ya Aina Mpya inayoonekana.
Kwa MT5: Bofya menyu kunjuzi ya aina ya order iliyo juu ya dirisha na uchague aina maalum ya pending order kwenye orodha.
- Kamilisha sehemu zinazohitajika za aina ya pending order yako.
- Weka viwango vya stop loss (SL) na take profit (TP) kwa hiari, pia weka Muda wa mwisho wa matumizi kwa pending order hiyo.
- Bofya Mahali (ikiwa ina rangi ya kijivu, vigezo vilivyowekwa vinaweza kuwa batili).
Pending order yako itaonekana kwenye kichupo cha Trade.
Udhibiti wa order
Udhibiti wa order unajumuisha kufunga na kurekebisha orders zinazotumika, na kufuta pending orders.
Kufunga orders
Bofya aikoni ya X kwenye kichupo cha Trade, au ubofye kulia kwenye order na uchague Funga order. Biashara ya mbofyo mmoja (maelezo zaidi hapa chini) inapofanya kazi, order hiyo itafungwa mara moja. Vinginevyo, sharti uthibitishe hatua ya kufunga order kwa kubofya kitufe cha manjano cha Funga .
Orders zilizofungwa huonekana kwenye kichupo cha Historia.
Kurekebisha orders
Unaweza kurekebisha pending orders zako na zilizofunguliwa kwenye kichupo cha Trade. Bofya kulia kwenye order kwenye kichupo cha Trade, na ubofye Rekebisha au Futa.
Kurekebisha order hukuruhusu kubadilisha stop loss (SL) au take profit (TP) kwa market orders zilizofunguliwa, au bei ya Fungua kwa, SL/TP na Muda wa mwisho wa matumizi kwa pending orders zako.
Biashara ya mbofyo mmoja
Biashara ya mbofyo mmoja ni kipengele muhimu ambacho hukuruhusu kufungua orders mpya kwa mbofyo mmoja.
Hivi ndivyo biashara ya mbofyo mmoja inavyoonekana kwa akaunti za kutrade za MT4:
Utaona kipengele cha biashara ya mbofyo mmoja, kama inavyoonyeshwa hapo juu, kwenye chati inayotumika. Badilisha instrument inayotumika ili kuonyesha kitufe chake cha biashara ya mbofyo mmoja.
MT4 pekee: Bainisha kiwango ambacho ungependa kutrade, kisha ubofye Ununuzi au Uuzaji ili kufungua trade kwa mbofyo mmoja.
Ili kuwasha biashara ya mbofyo mmoja
Onyo la biashara ya mbofyo mmoja sharti kwanza likubaliwe kabla ya kutumia kipengele hiki. Kwa MT4, bofya Options > Biashara ya Mbofya Mmoja ili kufungua onyo hilo. Kwa MT5, fungua menyu kuu na uchague Biashara ya Mbofya Mmoja ili kufungua onyo hilo.
Weka tiki kwenye Ninakubali Sheria na Masharti haya, basi bofya Kubali/Sawa ili kuwasha biashara ya mbofyo mmoja.
Dirisha la biashara ya mbofyo mmoja hubadilisha rangi kulingana na mwenendo wa bei. Bei inapoongezeka, rangi hukuwa ya samawati. Bei inapopungua, rangi hubadilika kuwa nyekundu.