Katika Exness, tunalenga kutoa hatua za haraka za kutoa pesa na mifumo mingi ya malipo ambayo unaweza kuchagua. Faida yetu ni kwamba unaweza kutoa funds wakati wowote kwa siku yoyote, ikiwa ni pamoja na wikendi na sikukuu.
Haya ndiyo unayohitaji kujua kuhusu uondoaji pesa katika Exness:
- Taarifa za Eneo Binafsi
- Kuondoa fedha
- Kipindi cha neema na uondoaji
- Ada za uondoaji
- Muda wa usindikaji wa uondoaji
- Mifumo ya Malipo
- Kipaumbele cha mfumo wa malipo
Taarifa za Eneo Binafsi
Eneo lililotolewa wakati wa kusajili akaunti yako ya Exness huonyesha njia za malipo zinazopatikana za kutoa pesa katika Eneo lako la Binafsi. Kwa hivyo, unaweza kujua ni njia gani za malipo zinapatikana katika eneo lako kwa kuingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
EB lako litaonyesha njia za malipo zinazopatikana pamoja na muda wa uchakataji na ada. Wakati njia ya kutoa pesa imezuiwa, EB pia litaonyesha sababu ya kuzuiwa; katika hali hii utahitaji kuwasiliana na Usaidizi kwa usaidizi zaidi.
Njia za malipo zinazopendekezwa
Ikiwa njia ya malipo inaonyeshwa kuwa inapendekezwa, basi ina kiwango cha juu cha kufanikiwa kwa hatua ya kutoa pesa katika eneo lako lililosajiliwa.
Njia za malipo za kimaeneo
Hali nadra zinaweza kutokea ambapo njia ya malipo ya eneo uliko (inayopatikana katika eneo maalum) inayotumika kuweka pesa huenda isionekane kwenye vichupo vya Kuweka pesa na Kutoa pesa vya EB. Hali hii itakapotokea, kutoa pesa kwa akaunti ya benki tofauti na ile iliyotumiwa kuziweka inawezekana lakini ikiwa benki hiyo inaweza kutumika kwa njia ya malipo ya kieneo pekee na jina la mwenye akaunti ya benki linalingana na jina la mwenye akaunti ya Exness.
Tafadhali wasiliana na Usaidizi kwa usaidizi zaidi ikiwa tukio hili lisilo la kawaida litakuzuia kutoa pesa.
Kuondoa fedha
Hatua za kutoa pesa zinaweza kufanywa siku yoyote, wakati wowote hivyo kukupa ufikiaji wa funds zako kwa wakati wowote. Unaweza kutoa funds kutoka kwa akaunti yako kwenye sehemu ya Kutoa pesa ya Eneo lako la Binafsi. Unaweza kuangalia hali ya uhamishaji chini ya Historia ya Transaction wakati wowote.
Walakini, fahamu sheria hizi za jumla za uondoaji pesa:
- Kiasi cha juu zaidi cha pesa unazoweza kutoa wakati wowote ni sawa na free margin ya akaunti yako ya kutrade inavyoonyeshwa katika Eneo lako la Binafsi.
- Hatua za kutoa pesa kwa kawaida huhitaji njia ya malipo, akaunti ya malipo na sarafu sawa na ile iliyotumika kuweka pesa ili kuhakikisha transactions rahisi zaidi. Ikiwa njia nyingi za malipo zitatumika kuweka pesa, tunalenga kusambaza pesa zinazotolewa kwa uwiano katika njia hizo za malipo.
- Options za ziada zinaweza kupatikana kwa traders waliotimiza masharti kando na njia za malipo zilizotumika kuweka pesa, kwa kuwa tunaelewa kwamba uwezo wa kutumia njia nyingi ni muhimu. Kwa hivyo katika hali fulani za kipekee, tunaweza kuondoa kanuni ya kawaida ya uondoaji sawia. Hata hivyo, hii hutegemea kukamilika kwa uthibitishaji wa akaunti na mwongozo wa wataalamu wetu wa malipo ambao huzingatia kwa makini kila ombi.
- Tunakuhimiza uchunguze options zako za kutoa pesa zinazopatikana katika Eneo lako la Binafsi. Jukwaa letu lina kiolesura rahisi kutumia ili kufanya hatua ya kutoa pesa iwe rahisi.
- Tafadhali kumbuka kuwa ikiwa unajaribu kutumia option rahisi ya malipo na ikataliwe, inaweza kumaanisha kuwa akaunti yako bado haijatimiza masharti ya njia mbadala hiyo mahususi. Options zetu za malipo zinazobadilika hutolewa kulingana na vipengele mbalimbali, ikiwa ni pamoja na historia ya akaunti yako na masuala ya udhibiti wa hatari.
- Kabla ya faida yoyote kuweza kutolewa kwenye akaunti ya kutrade, kiasi kamili kilichowekwa katika akaunti hiyo ya kutrade kupitia kadi ya benki au bitcoin sharti kitolewe kabisa. Operesheni hii inajulikana kama ombi la refund.
- Ili kuboresha nyakati za transaction, hatua ya kutoa pesa sharti ifuate kipaumbele cha mfumo wa malipo: ombi la refund ya kadi ya benki kwanza, ikifuatiwa na ombi la refund ya bitcoin, kisha ombi lingine lolote. Tazama maelezo zaidi kuhusu mfumo huu mwishoni mwa makala haya.
Hapa chini kuna mfano wa jinsi kanuni zote zilizo hapo juu zinafanya kazi pamoja:
Umeweka jumla ya USD 1 000 kwenye akaunti yako: USD 700 kupitia kadi ya benki na USD 300 kupitia Neteller. Kwa kuzingatia kipaumbele cha mfumo wa malipo, utahitajika kufanya refund ya pesa zilizowekwa kupitia kadi yako ya benki kwanza.
Hebu tuchukulie kuwa umepata USD 500 na ungependa kutoa salio lako lote, pamoja na faida:
- Akaunti yako ya kutrade ina free margin ya USD 1 500, ambayo ndiyo jumla ya ya pesa ulizoweka awali na faida inayofuata.
- Utahitaji kwanza kutuma maombi ya refund ukifuata kipaumbele cha mfumo wa malipo, yaani, kuanza na kufanya refund ya USD 700 kwenye kadi yako ya benki.
- Maombi yote ya refund yatakapokamilika, unaweza kutoa funds kupitia njia nyingine za malipo (k.m. Neteller).
Madhumuni ya mfumo wa kipaumbele wa malipo ni kuhakikisha kuwa Exness inafuata sheria za kifedha zinazokataza utakatishaji wa fedha haramu na ulaghai unaoweza kutokea, na kuifanya kuwa kanuni muhimu bila kighairi.
Kipindi cha neema na uondoaji
Kipindi cha neema ni muda kabla ya akaunti ya Exness kuthibitishwa kikamilifu, na huzuia utendaji wa akaunti kwa njia fulani. Hakuna kikomo cha funds zinazoweza kutolewa au kuhamishwa wakati wa kipindi cha neema, lakini pesa haziwezi kutolewa kwa kutumia njia hizi za malipo:
Unaweza kuendelea kutoa pesa hata baada ya akaunti kuzuiwa ( kipindi cha neema kinapoisha), lakini internal transfers huzimwa baada ya kipindi cha neema kuisha.
Fuata kiungo ili kupata maelezo kuhusu kipindi cha neema.
Ada za uondoaji
Hakuna ada zinazotozwa wakati wa kutoa pesa, lakini baadhi ya mifumo ya malipo ina ada ya transaction. Ni vyema kufahamu ada zozote za mfumo wako wa malipo kabla ya kuamua kutumia kuweka pesa.
Tunapendekeza ufuate kiungo kwa maelezo zaidi kuhusu mifumo ya malipo inayotolewa.
Muda wa usindikaji wa uondoaji
Idadi kubwa ya hatua za kutoa pesa kwa Mifumo ya Malipo ya Kielektroniki (EPS) hufanywa papo hapo, kumaanisha kuwa transaction hukaguliwa ndani ya sekunde chache (hadi saa zisizozidi 24) bila kuchakata mwenyewe.
Unaweza kupata muda wa uchakataji wa hatua ya kutoa pesa kwa kila njia ya malipo kwenye sehemu ya Kutoa pesa ya Eneo lako la Binafsi.
Ikiwa muda uliobainishwa wa kutoa pesa umepita, tafadhali wasiliana na Timu ya Usaidizi ya Exness ili tuweze kukusaidia kutatua hitilafu hiyo.
Mifumo ya Malipo
Exness inaendelea kuongeza Mifumo mipya ya Malipo ya Kielektroniki (EPS) ili kukupa options zaidi za kufanya transaction. Fahamu kuwa baadhi ya options zimezuiwa na eneo, na tunapendekeza usome zaidi kuhusu EPS ili kupata maelezo kuhusu njia inayoweza kukufaa zaidi.
Kipaumbele cha mfumo wa malipo
Ili kuhakikisha transactions za haraka, tafadhali kumbuka kipaumbele cha mfumo wa malipo kilichowekwa ili kuzingatia sheria za kifedha. Kutoa pesa ukitumia njia zilizoorodheshwa za malipo sharti ifanywe kulingana na kipaumbele hiki:
- Urejeshaji wa kadi ya benki
- Urejeshaji wa Bitcoin
- Kutoa faida, kwa kuzingatia uwiano wa kuweka na kutoa pesa kama ilivyoelezwa hapo awali
Kipaumbele cha mfumo wa malipo kinategemea Eneo lako la Binafsi kwa ujumla badala ya akaunti moja ya kutrade.
Comments
0 comments
Article is closed for comments.