Programu ya Exness Trade terminali yako ya kifaa cha mkononi yenye vipengele vyote inayofanya kazi moja kwa moja na akaunti yako ya kutrade ya Exness. Pia hukupa vipengele vya usimamizi wa akaunti na uwezo kutrade popote ulipo.
Ikiwa unakumbana na matatizo katika Exness Trade, tuna mada mbalimbali za kawaida ambazo zinaweza kukusaidia. Ikiwa makala haya hayawezi kujibu maswali yako, tafadhali usisite kuwasiliana na Usaidizi kwa usaidizi.
Kabla ya kujaribu kuyatatua, tafadhali hakikisha kuwa umesasisha programu ya Exness Trade hadi toleo jipya zaidi; ni toleo la iOS 14.5 au toleo jipya zaidi pekee linalotumika.
Mada za kawaida:
- Kwa nini siwezi kuingia?
- Kwa nini siwezi kupata aikoni ya Trade chini ya akaunti yangu?
- Kwa nini sioni zana za kutrade?
- Kwa nini kituo changu cha biashara kimewekwa kuwa Exness?
- Kwa nini sijapokea msimbo wangu wa kuthibitisha?
- Je, kwa nini sipati programu ya Exness Trade katika Duka la Programu la Apple au Duka la Google Play?
Programu ya Exness Trade huenda isipatikane katika baadhi ya nchi kwenye Google Play na App Store. Ikiwa unahitaji usaidizi zaidi unaweza kuwasiliana na timu ya usaidizi ya Exness.
Kwa nini siwezi kuingia?
Tafadhali hakikisha kuwa maelezo yako ya kuingia kwenye akaunti yako ya Exness yamewekwa kwenye programu kwa usahihi. Utahitaji anwani yako ya barua pepe iliyosajiliwa ya akaunti ya Exness na nenosiri la akaunti (sio maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako ya kutrade ya Exness).
- Weka upya anwani ya Kuingia kwenye Akaunti
Fuata hatua hizi ili kuweka upya maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako na uweze kuingia:
- Fungua programu ya Exness Trade.
- Chagua Sign In.
- Gusa I forgot my password.
- Weka anwani yako ya barua pepe iliyosajiliwa na ukamilishe masharti ya usalama ya Captcha.
- Weka msimbo wa uthibitishaji uliotumwa kwa aina uliyochagua ya usalama.
- Bofya Thibitisha ili kubadilisha maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako ya Exness.
- Sasa unaweza kuingia kwa kutumia maelezo yako mapya.
Weka upya Nambari ya siri
Unapoingia kwa kutumia akaunti yako, unaweza kuombwa uweke msimbo wa siri (Nambari ya PIN yenye tarakimu 6). Msimbo huu wa siri umeunganishwa na Eneo la Binafsi au Akaunti moja.
Ukiingia kwa kutumia Eneo la Binafsi au Akaunti tofauti, hutaweza kuingia.
Ili kuweka upya nenosiri hili:
- Washa Exness Trade.
- Gusa Umesahau? kutoka kwa skrini ya kuingiza nambari ya siri.
- Gusa Sawa ili kuthibitisha kitendo.
- Chagua Sign in na uweke msimbo mpya wa siri ili kuendelea.
Kwa nini siwezi kupata aikoni ya Trade chini ya akaunti yangu?
Ikiwa umeweka jukwaa lako chaguomsingi la biashara kuwa Exness kwenye programu ya Exness Trade, hutaona aikoni ya Trade chini ya akaunti yako kwenye kichupo cha Accounts.
Ili kuweka trade:
- Nenda kwenye kichupo cha Trade kilicho sehemu ya chini ya skrini.
- Chagua instrument ambayo ungependa kutrade nayo.
- Gusa kitufe cha Sell au Buy.
- Sanidi kiwango cha biashara kwenye dirisha lililoonyeshwa.
- Angalia fedha halisi zinazoonyeshwa na uhakikishe kuwa kuna fedha za kutosha kufungua biashara.
- Bofya kwenye Confirm Buy au Confirm Sell ili kufungua trade.
a. Ili kuweka mipangilio ya pending order, rejelea Order Settings.
Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti mipangilio ya akaunti yako kwenye programu ya Exness Trade.
Kwa nini sioni zana za kutrade?
Sababu ya kawaida ya hitilafu hii inaweza kuwa muunganisho wa intaneti usio thabiti, ambao utaacha sehemu wazi ambapo instruments za biashara zinapaswa kuonyeshwa.
Tafuta na uunganishe kwenye mtandao thabiti, kama vile muunganisho wa moja kwa moja wa Wi-Fi na uonyeshe upya programu kwa kuondoka na kuingia tena.
- Tafuta zana mahususi
Ikiwa unatafuta instrument mahususi ya biashara lakini haijaonyeshwa, fuata hatua hizi ili kuipata na uiongeze kwenye Favouriteszako.
- Kwenye programu ya Exness Trade, nenda kwenye kichupo cha Trade.
- Gusa aikoni ya Kioo cha Ukuzaji kando ya sehemu ya Favorites.
- Weka jina au msimbo wa instrument.
- Gusa kwenye kadi ili kuleta maelezo kamili ya instrument.
- Kisha, bofya kwenye aikoni ya Nyota ili kuiongeza katika Favourites.
Vile vile, ili kuondoa zana kwenye orodha yako ya vipendwa, bofya tu tena kwenye aikoni ya nyota.
Ili kuweka mipangilio ya arifa za programu kwa instruments unazopendelea, pata maelezo zaidi kwenye jinsi ya kuhariri arifa.
Chati ya TradingView
Chati ya TradingView inakupa ufikiaji wa haraka wa utendaji hapa chini:
- Indicators zaidi ya 100
- Zana za Kuchora
- Mipangilio ya rangi
Kumbuka: Baadhi ya indicators (kama vile utendakazi unaohusiana na kiwango) hazipatikani.
TradingView itaonekana kwenye Stories. Unaweza kufikia TradingView kwa kubofya Profile kisha kwenye Settings. Bofya kwenye Trading terminal na uchague TradingView.
Kwa nini kituo changu cha biashara kimewekwa kuwa Exness?
Kwa chaguomsingi, terminali ya biashara itawekwa kuwa Exness unaposakinisha, kusakinisha upya au kusasisha programu yako ya Exness Trade. Ili kubadilisha hadi terminali zako za biashara unazopendelea kama vile Exness, Built-in MetaTrader 5 au MetaTrader 5, fuata hatua hizi:
- Kwenye skrini yako kuu, nenda kwenye kichupo cha Profile.
- Kwenye ukurasa wa Wasifu, bofya aikoni ya mipangilio iliyo kwenye kona ya juu kulia ya skrini.
- Chini ya mapendeleo, gusa kwenye Trading Terminal.
-
Kisha utaona terminali za biashara zinazopatikana unaweza kuchagua kutoka:
- Exness - Kuchagua hii kutamaanisha kuwa utatumia terminali ya Exness kwenye programu ya simu ya mkononi kufanya biashara.
- Built-in MetaTrader 5 - Ukichagua hii, utaweza kutumia MT5 iliyo ndani bila kuondoka kwenye Programu ya Exness Trade.
- MetaTrader 5 App - Kuchagua hii kutamaanisha kwamba utapelekwa kwenye programu ya MT5 kufanya biashara. Kwa hivyo, ukichagua hii, unahitaji kuhakikisha kuwa umesakinisha programu ya MT5 kwenye simu yako.
- Chagua terminali yako ya biashara unayopendelea.
Kumbuka: Options zote zilizotajwa hapo juu zinapatikana tu kwa kutrade kwenye akaunti za MT5. Ikiwa ungependa kutrade kwenye akaunti za MT4, utahitaji kusakinisha programu ya MT4. Kisha mfumo utakuelekeza kiotomatiki kwenye programu ya MT4 unapobofya Trade.
Kwa nini sijapokea msimbo wangu wa kuthibitisha?
Zingatia aina ya usalama uliyochagua kwa ajili ya Eneo lako la Binafsi. Ikiwa aina yako ya usalama imewekwa kuwa barua pepe, misimbo yako ya uthibitishaji itatumwa katika anwani yako ya barua pepe iliyosajiliwa bila kujali wakati programu ya Exness Trade itaonyesha ujumbe “Enter the code we sent to your phone ”.
Ili kuangalia hii:
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Chagua Settings kutoka kwenye menyu kuu, kisha uende kwenye kichupo cha Security Settings.
- Utaona Aina ya Usalama inayotumika kwa akaunti yako.
Ikiwa aina yako ya usalama iliwekwa kuwa Simu na bado hukupokea msimbo wa uthibitishaji kutoka kwa Exness Trade, tafadhali wasiliana na Usaidizi kwa usaidizi.
Je, kwa nini sipati programu ya Exness Trade katika Duka la Programu la Apple au Duka la Google Play?
Iwapo huwezi kupata programu ya Exness Trade kwenye Duka la Programu la Apple au Google Play, huenda, kwa bahati mbaya, hatukubali wateja kutoka nchi unakoishi.
Ikiwa tayari una programu hii, tunapendekeza usiiondoe kwa kuwa hautaweza kuirejesha.
Kwa taarifa zaidi kuhusu hili, bofya hapa kwa orodha ya nchi ambazo Exness haikubali wateja wake.
Ikiwa tatizo lako halijaorodheshwa hapa au halijatatuliwa vya kutosha, tafadhali pendekeza mada hiyo ili tuweze kuiongeza kwenye ukurasa huu, au uwasiliane na Usaidizi wa Exness kwa usaidizi zaidi.