Kabla ya trader kutoa faida aliyopata, sharti atoe kwanza pesa zote zilizowekwa kwenye akaunti ya kutrade - hii inajulikana kama ombi la refund.
Refunds zinazofanywa sharti zifuate kipaumbele cha mfumo wa malipo ili kuboresha mara za transaction:
- Urejeshaji wa kadi ya benki
- Urejeshaji wa Bitcoin
- Utoaji wa faida, kwa kuzingatia uwiano wa kuweka na kutoa pesa.
Maombi ya refund kwa sehemu ni wakati maombi ya refund hufanywa kwa kiasi kidogo badala ya jumla ya kiasi cha funds kilichowekwa.
Kumbuka: Ikiwa maombi ya refund kwa sehemu hayapatikani katika eneo lako, itabidi utume ombi la refund kamili kulingana na kanuni za kipaumbele za mfumo wa malipo kabla ya kutoa faida.
Hapa kuna mfano:
Ikiwa umeweka funds kwenye akaunti ya kutrade zenye jumla ya USD 100, unaweza kutuma maombi mengi ya refunds ambayo yakijumlishwa yatafikia kiasi hicho; USD 50, USD 13, USD 27, na USD 10.
Mfano mwingine:
Iwapo uliweka funds zenye jumla ya USD 300 ukitumia kadi ya benki na ukapata hasara ya USD 100, basi utakuwa na USD 200 pekee kwenye akaunti yako ya kutrade.
Bado unaweza kutuma ombi la refunds kwa sehemu za kiasi cha USD 200 kwenye kadi yako ya benki, kulingana na kiasi cha pesa ulichoweka awali.
Ukiweka pesa zingine za kiasi cha USD 100 kupitia Skrill, na upate faida ya USD 50. Kulingana na kanuni za kipaumbele za mfumo wa malipo, bado utahitaji kufanya refund ya USD 100 kwenye kadi yako ya benki, kabla ya kutoa faida ya USD 50 kwenye Skrill.
Jinsi ya kutuma ombi la refund kwa sehemu
Kutuma ombi la refund kwa sehemu ni sawa na kutuma ombi la kufanya refund kwa ujumla. Tofauti pekee ni kuweka kiasi kidogo cha refund.
- Chagua Bank Card kutoka kwa sehemu ya Withdrawal ya EB yako.
- Bofya Show my refunds kutoka ukurasa unaofuata.
- Chagua kadi ya benki ili ukamilishe urejeshaji wa pesa.
- Katika ukurasa unaofuata, jaza fomu, ikijumuisha:
-
- Kuchagua kadi ya benki kama mbinu ya malipo.
- Chagua akaunti ya biashara ya kurejesha pesa kutoka.
- Weka kiasi kitakachorejeshwa.
Bofya Endelea.
- Muhtasari wa muamala utawasilishwa; bofya Thibitisha ili kuendelea.
- Weka nambari ya kuthibitisha iliyotumwa kwako kwa barua pepe au SMS (kulingana na aina ya usalama) ya Eneo Binafsi lako, kisha ubofye Thibitisha.
- Ujumbe utathibitisha kuwa ombi la kurejesha pesa limekamilika.
Kumbuka kuwa kiasi cha chini zaidi cha utoaji wa pesa bado kinatumika kwa ombi la refund, na kiasi kamili cha funds zilizowekwa sharti kirejeshwe kabla ya utoaji wa faida.
Baada ya ombi la refund kwa sehemu, unaweza kuona transactions nyingi za refund katika historia yako ya transaction. Hii hutokea ombi la refund linapozidi kiasi chochote cha pesa kilichowekwa ikiwa pesa hizo ziliwekwa kwa transactions kadhaa. Jumla ya kiasi cha refund kinachohitajika kabla ya utoaji wa faida kitasalia bila kubadilika hali hii itakapotokea.
Ukituma ombi la refund ndani ya saa 24 baada ya kuweka pesa, mchakato wa refund utachukua siku 3-5 za kazi.
Kwa maelezo zaidi, tunahimiza kila mtu asome zaidi kuhusu jinsi utoaji wa pesa unavyofanya kazi.