Utahitaji kuwasilisha uthibitishaji wa utambulisho wako na wa makazi/anwani kwa akaunti ya Exness iliyothibitishwa kikamilifu. Katika Exness, Uthibitisho wa Utambulisho hurejelewa kama POI na Uthibitisho wa Makazi/Anwani kama POR.
Uthibitishaji wa hati utachukua hadi saa 24 na ikiwa hakuna taarifa baada ya saa 24, tafadhali wasiliana na Wasaidizi wa Exness.
Unapopakia hati zako utaombwa uchague nchi yako na aina ya hati. Kulingana na chaguo lako, unaweza kuonyeshwa mifano ya hati zinazokubalika.
Mahitaji ya hati
Hati za uthibitishaji zinahitaji kutimiza masharti fulani au zinaweza kukataliwa na kuchelewesha mchakato wa uthibitishaji. Tunapendekeza ufuate kiungo ikiwa ungependa kuona mifano ya kwa nini hati za uthibitishaji zinaweza kukataliwa.
Muhimu kuzingatia:
- Utahitaji kutoa hati mbili (2) tofauti kwa uwasilishaji wa POI na POR. Utaombwa kuzipakia kwa mfululizo wakati wa mchakato wa uthibitishaji.
- Wateja katika baadhi ya nchi wanaweza kutumia hati moja kuthibitisha POI na POR.
Kwa Uthibitisho wa Utambulisho (POI)
Hati ya POI iliyotolewa sharti iwe na maelezo yafuatayo:
- Picha ya mteja iliyo na jina kamili la mteja linalolingana na jina la mwenye akaunti.
- Tarehe ya kuzaliwa ya mteja (Umri wa mteja unapaswa kuwa 18 au zaidi).
- Hati hiyo inapaswa kuwa halali (angalau mwezi mmoja wa uhalali) na haijaisha muda wake.
- Ikiwa hati ni ya pande mbili, tafadhali pakia pande zote za hati.
- Pembe zote nne za hati zinapaswa kuonekana.
- Muundo wa hati iliyopakiwa unapaswa kuwa wa ubora wa kiwango cha juu.
- Hati hiyo inapaswa kutolewa na serikali.
Mifano ya hati za POI |
|
Miundo ya upakiaji inayokubaliwa | Picha, Hati iliyochanganuliwa, Nakala (Pembe zote zionekane) |
Viendelezi vya faili vinavyokubaliwa |
jpg, jpeg, mp4, mov, webm, m4v, png, jpg, bmp, pdf (Hadi MB 64) |
Muhimu kuzingatia:Hati ya POI inapaswa kuwa ilitolewa rasmi na mamlaka halali na sharti ithibitishe jina, umri, na picha ya mteja. Sio lazima hati iwe ilitolewa mahali mteja alizaliwa au kwa nchi yake ya uraia.
Kwa mfano, mteja wa kutoka India anayeishi Kolombia anaweza kutumia hati ya POI iliyotolewa nchini India, Kolombia, au nchi nyingine yoyote ambapo tunakubali wateja wake. Ni ni muhimu kutambua kwamba hatukubali hati za POI zinazotolewa katika nchi hizi maalum: Samoa ya Amerika, Kisiwa cha Baker, Guam, Kisiwa cha Howland, Kisiwa cha Jarvis, Johnston Atoll, Kingman Reef, Visiwa vya Marshall, Visiwa vya Midway, Kisiwa cha Navassa, Visiwa vya Northern Mariana, Palmyra Atoll, Puerto Rico, Visiwa Vidogo vya nchi ya Marekani, Marekani, Visiwa vya Virgin vya Marekani, Vatican City, na Kisiwa cha Wake.
Kwa Uthibitisho wa Makazi (POR)
Hati ya POR iliyotolewa sharti iwe na maelezo yafuatayo:
- Jina kamili la mmiliki wa akaunti ya Exness na hati ya POI haswa.
- Jina kamili la mteja na anwani.
- Tarehe ya kutolewa.
- Hati hiyo inapaswa kuwa imetolewa ndani ya miezi 6 iliyopita.
- Kingo zote nne za hati zinapaswa kuonekana.
- Ikiwa hati ni ya pande mbili, tafadhali pakia pande zote za hati.
- Hati iliyopakiwa inapaswa kuwa ya ubora wa kiwango cha juu.
Muhimu kuzingatia:Hati ya POR inapaswa kuwa ilitolewa rasmi na mamlaka halali na sharti ithibitishe kuwa mteja anaishi katika nchi ambako amefungulia akaunti yake ya Exness. Hii hufanywa ili kuhakikisha kuwa mteja ana makazi ya kudumu katika nchi aliyochagua wakati wa usajili wa akaunti.
Mifano ya hati za POR |
|
Miundo ya upakiaji inayokubaliwa | Picha, Hati iliyochanganuliwa, Nakala (Pembe zote zionekane) |
Viendelezi vya faili vinavyokubaliwa |
jpg, jpeg, mp4, mov, webm, m4v, png, jpg, bmp, pdf (Hadi MB 64) |
Kumbuka:
- Mteja anaweza kutumia hati zozote zilizoorodheshwa kwenye sehemu ya POI kwa uthibitishaji wa POR ilmradi zisiwe zimetumika kwa uthibitishaji wa POI.
- Wateja katika baadhi ya nchi wanaweza kutumia hati moja kuthibitisha POI na POR.
Kuthibitisha utambulisho na anwani yako ni hatua muhimu ambayo hutusaidia kuweka akaunti yako na transactions zako za kifedha salama. Mchakato wa uthibitishaji ni moja tu ya hatua za usalama za Exness zinazotekelezwa ili kulinda traders wetu.
Comments
0 comments
Article is closed for comments.