Indices zinaweza kuathiriwa na marekebisho ya mgao kulingana na kama wewe ni mnunuzi au muuzaji wa index.
Je, Migawio kwenye Indices ni nini?
Index hujumlisha kampuni nyingi. Wakati moja kati ya kampuni hizi inalipa mgao, inapunguza thamani yake kwa kiasi cha mgao huo.
Kupungua huku kwa thamani hudhihirishwa na kushuka kwa bei ya hisa kwenye tarehe ya mgao wa awali. Katika hali ya index, kupungua kwa bei huenda sawia na ukubwa wa mgao na uzito wa kampuni zilizo ndani ya index hiyo. Kwa hivyo, wakati mwingine marekebisho ya mgao hayaonekani, ilhali kwa wakati mwingine, athari zake kwa bei ya index zinahitaji kufafanuliwa.
Katika Exness, kiasi cha mgao kitatozwa au kuwekwa kwenye salio la akaunti ya kutrade kila siku wakati wa kufunguliwa kwa kipindi cha biashara cha kila index.
Jinsi ya Kukokotoa Mgao kwenye Indices?
Ili kuonyesha hali za soko kwa usahihi, Exness hutumia marekebisho ya mgao kwa indices. Mgao hulipwa au kutozwa kwa "msingi wa kila instrument", kumaanisha kuwa marekebisho yaliyojumlishwa kwa positions zote kwenye index maalum ambazo bado zimefunguliwa hadi mwisho wa siku iliyotangulia tarehe ya mgao wa awali. Saa za biashara za indices zinaweza kupatikana hapa.
Trades za ununuzi zinaweza kupokea mgao, unaokokotolewa kama ifuatavyo:
Kiasi cha mgao kilichopokelewa (sarafu ya index iliyonukuliwa) = Lots × Contract size x Kiwango cha gawio
Trades za uuzaji zinaweza kutozwa mgao, unaokokotolewa kama ifuatavyo:
Kiasi cha mgao kinachotozwa (katika sarafu ya index iliyonukuliwa) = Lots × Contract size x Kiwango cha mgao
Tafadhali rejelea sehemu mpya ya Migawio chini ya kichupo cha Utendaji kwenye Eneo la Binafsi ili kufuatilia ni kiasi gani kilipatikana/kutozwa kama mgao kwa kila position.
Mabadiliko yoyote ya salio kutokana na migawio pia yanapatikana kwenye jukwaa la biashara la MT.
Tafadhali fuatilia kwa karibu taarifa mpya za Mgao unapofanya trade ya indices husika. Jedwali lifuatalo husasishwa kila wiki ili kuonyesha mgao ujao ambao utalipwa/kutozwa:
Chagua tarehe
Viwango vinaweza kutofautiana na vilivyoonyeshwa kwenye ukurasa huu. Kiasi kipya kilicholipwa au kutozwa kwa siku yoyote ile kinapatikana kupitia sehemu ya Migawio kwenye Eneo la Binafsi.
*Kumbuka: Ili kuona migawio ijayo itakayolipwa au kukatwa, tafadhali rejelea ukurasa huu kwa kuwa unatoa historia ndefu ya migawio na husasishwa kila wiki.