Exness Premier ni programu ya uaminifu ambayo huzawadi wanachama wetu wa Exness wanaoendeleza biashara na walio waaminifu zaidi wa Premier kwa kuwapa mafao anuwai ya kipekee ambayo hukua kadri wanavyotimiza masharti kwa madaraja makubwa na ya kifahari zaidi ya uanachama.
- Mafao
- PressReader
- Madaraja
- Vigezo vya kutimiza masharti
- Masharti ya Kila Robo Mwaka
- Nchi zinazotimiza masharti
- Hali yako ya Premier
Mafao
Je, Exness Premier inanifaidi vipi?
Exness Premier hutambua na kuwatuza wanachama wanaoendeleza biashara na walio waaminifu na zawadi za kipekee na usaidizi uliopewa kipaumbele kutoka kwa timu yetu ya wasimamizi wataalamu wa akaunti.
Tungependa ufanikiwe kutrade katika Exness, na ufurahie usaidizi wa kiwango cha juu kwa urahisi. Tunathamini maoni yako na kuchukua hatua ili kuhakikisha kuwa umeridhika.
Kama mwanachama wa Exness Premier, tunakupa kipaumbele zaidi. Kwa taarifa zaidi, unaweza kutembelea ukurasa wetu wa mwanzo wa Exness Premier ili kugundua zaidi kuhusu manufaa ya kipekee utakayopata kama mwanachama wa Exness Premier.
Ni vizuri kujua: Mafao na zawadi za Exness Premier zinaweza kutofautiana kulingana na eneo na haziwezi kurejeshwa au kubadilishwa kuwa pesa taslimu. Iwe yametolewa na Exness au washirika wengine, mafao haya hayawezi kununuliwa, kuuzwa, kubadilishwa au kuhamishwa.
PressReader
Usajili wa kipekee kwa PressReader
Exness Premier pia inajivunia usajili usiolipishwa na wa kipekee wa muda mfupi wa PressReader kwa wanachama wote wa Premier Signature na Elite. Ni kampuni ya usambazaji wa magazeti ya kidijitali ambayo ina zaidi ya magazeti na makala 7000 kwa zaidi ya lugha 60.
Wanachama wa Exness Premier ambao wametimiza masharti ya kupata mafao haya watapokea kiungo cha kudai usajili wao usiolipishwa kupitia anwani zao za barua pepe zilizosajiliwa za akaunti ya Exness.
Kujisajili kwenye PressReader:
- Angalia barua pepe iliyosajiliwa ya akaunti yako ya Exness ili kupata barua pepe kuhusu usajili wa kipekee wa PressReader.
- Bofya kiungo kilichotolewa kwenye barua pepe ambacho kitakupeleka kwenye ukurasa wa kutua wa PressReader.
- Fuata maagizo kwenye skrini ili kufungua akaunti ya PressReader na/au kudai kipindi chako cha usajili usiolipishwa.
Ili kuongeza usajili wako kwa PressReader, hivi hapa ni vidokezo vichache:
-
Sikiliza makala
- Kuendelea na usomaji kunaweza kuwa changamoto ikiwa unasafiri kila wakati, lakini PressReader hutoa options za kubadilisha maandishi-hadi-sauti ili uweze kusikiliza makala yoyote kwenye jukwaa. Hii hapa ni jinsi ya kuwezesha kipengele cha kubadilisha maandishi-hadi-sauti kwa PressReader.
-
Soma katika lugha unayopendelea
- PressReader hutoa idadi kubwa ya makala yake katika hadi lugha 60. Kwa hatua chache, unaweza kutafsiri maudhui kwa lugha yoyote inayopatikana katika PressReader.
-
Habari jinsi ambayo ungependa
- Weka mapendeleo kwenye mpasho wako wa PressReader jinsi upendavyo, ukiwa na mwonekano thabiti wa mipangilio ambao unaweza kuchuja makala na mada kwa mapendeleo yako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubinafsisha PressReader ili ikufae zaidi.
Usaidizi wa PressReader
Ukijaribu kupakua maudhui yoyote na uombwe kununua, basi akaunti yako inaweza kuwa haijaunganishwa na usajili usiolipishwa ipasavyo. Tafadhali wasiliana na care@pressreader.com kwa usaidizi kutoka kwa timu ya Huduma kwa Mteja na Mshirika ya PressReader.
Kumbuka: Kwa miongozo zaidi ya watumiaji wa PressReader, tembelea Kituo cha Usaidizi cha PressReader kwa maelezo zaidi.
Madaraja
Madaraja ya Exness Premier
Premier Preferred
Huu ni mwanzo wa safari yako ya Exness Premier, na utapata mafao na zawadi mbalimbali za kipekee ambazo ni pamoja na huduma kwa mteja iliyopewa kipaumbele, rasilimali za kielimu, uchanganuzi wa kitaalamu wa biashara, na ofa maalum.
Premier Elite
Premier Elite hutoa mafao yote ya Premier Preferred, lakini zaidi ya hayo, unapokea usaidizi uliobinafsishwa na wa kipaumbele kutoka kwa msimamizi maalum wa akaunti.
Premier Signature
Premier Signature ndilo daraja la kifahari zaidi la Exness Premier, linalotoa fursa za mitandao za kiwango cha juu kabisa na ufikiaji wa moja kwa moja wa wasimamizi wetu wa utendaji, na masharti ya kipekee ya biashara. Bila shaka, uanachama wa Premier Signature unajumuisha vipengele vyote na mafao ya madaraja ya awali.
Vigezo vya kutimiza masharti
Jinsi ya kutimiza masharti kwa Programu ya Exness Premier?
Ili kutimiza masharti kwa programu hii, sharti angalau utimize masharti yafuatayo:
- Eneo lako la Binafsi(EB) sharti liwe lilifunguliwa zaidi ya siku 30 zilizopita.
- Jumla ya pesa zote ulizoweka kufikia sasa kwa akaunti yako inapaswa kuwa zaidi ya USD 15,000.
- Jumla ya kiwango cha biashara kufikia sasa inapaswa kuwa zaidi ya USD milioni 40.
Kila daraja la Exness Premier lina masharti ya kipekee kwa jumla ya pesa zilizowekwa kufikia sasa na kiwango cha biashara kwa kila robo mwaka, na vigezo vyote viwili sharti vifikiwe ili kutimiza masharti katika nchi zote ambako Exness inafanya kazi isipokuwa Uchina, Taiwan, Hong Kong, na Macao.
Daraja la Premier | Premier Preferred | Premier Elite | Premier Signature |
Jumla ya pesa zilizowekwa kufikia sasa | USD 20 000 | USD 50 000 | USD 100 000 |
Kiwango cha biashara kwa kila robo | USD milioni 50 | USD milioni 100 | USD milioni 200 |
- Ni pesa zilizowekwa kutoka nje pekee zinazotimiza masharti ya pesa zote zilizowekwa kufikia sasa na internal transfers hazitazingatiwa.
- Pesa zilizowekwa za Social Trading na kiwango cha biashara cha orders zilizofunguliwa na kufungwa kutoka kwa Wawekezaji zinajumuishwa katika ukokotoaji wa masharti.
- Ukokotoaji wa masharti hautajumuisha kiwango cha biashara kutoka kwa Wasimamizi wa Portfolio na Wawekezaji, pamoja na pesa zilizowekwa na Wawekezaji.
Masharti ya Kila Robo Mwaka
Masharti ya daraja la Exness Premier hukokotolewa kwa vigezo hivyo kila robo ya mwaka wa kalenda, na mchakato kamili umeelezewa kwa kina zaidi hapa chini:
- Robo ya 1: Kiwango cha biashara hufuatiliwa kati ya Januari 1 - Machi 31, pamoja na jumla ya pesa zote zilizowekwa kufikia sasa.
-
Robo ya 2: Akaunti yako inapotimiza masharti, itakabidhiwa daraja la Exness Premier kuanzia Aprili 1 - Juni 30.
Kiwango cha biashara bado hufuatiliwa kuanzia Aprili 1 - Juni 30, ikiwa ni pamoja na pesa zote zilizowekwa kufikia sasa. -
Robo ya 3: Akaunti yako inapotimiza masharti ya kupandishwa daraja, itakabidhiwa daraja linalofaa la Exness Premier kuanzia Julai 1 - Septemba 30, vinginevyo itasalia katika Daraja lile lile la Exness Premier.
Kiwango cha biashara bado hufuatiliwa kati ya Julai 1 - Septemba 30, ikiwa ni pamoja na pesa zote zilizowekwa kufikia sasa. - Robo ya 4: Mchakato huu hujirudia, na akaunti yako ni hukabidhiwa daraja linalofaa la Exness Premier kuanzia Oktoba 1 - Desemba 31. Kiwango cha biashara hufuatiliwa kati ya Oktoba 1 - Desemba 1, ikiwa ni pamoja na jumla ya pesa zote zilizowekwa kufikia sasa.
- Baada ya hapo mchakato huu hurudiwa kila robo mwaka kama ilivyoonyeshwa hapa juu.
Ukokotoaji wa kiwango cha biashara
Kiwango cha biashara hufuatiliwa kila robo mwaka na hukokotolewa kama jumla ya orders zote zilizofunguliwa na zilizofungwa katika robo ya sasa (katika pande zote mbili za order).
Points za kuzingatia:
- Ikiwa mteja amefungua na kufunga order katika robo ya sasa, basi tunahesabu kiwango cha kufungua na kufunga.
- Ikiwa mteja alifungua order katika robo iliyopita na akaifunga katika robo hii, basi tunahesabu kiwango cha kufunga pekee.
- Ikiwa mteja atafungua order katika robo ya sasa na kuifunga katika robo inayofuata, basi tunahesabu kiwango cha kufungua pekee.
Kumbuka: Haiwezekani kuwa na uanachama mwingi wa Premier. Daraja la juu kabisa la Premier hutumika kwa akaunti zote ikiwa umetimiza masharti kwa madaraja mengi ya Premier katika Maeneo tofauti ya Binafsi. Ikiwa hungependa kushiriki katika programu ya Exness Premier, tafadhali tuma barua pepe kwa premier@exness.com ili kughairi uanachama wako, na usome sheria na masharti yetu kwa maelezo zaidi.
Nchi zinazotimiza masharti
Exness Premier inapatikana katika nchi nyingi ambako Exness inafanya kazi. Ikiwa eneo lako limeorodheshwa hapa chini, unaweza kujiunga na programu ya Exness Premier:
Asia: Afghanistan, Bahrain, Bangladesh, Brunei Darussalam, Kambodia, India, Indonesia, Jordan, Korea Kusini, Kuwait, Laos, Lebanon, Maldives, Nepal, Oman, Pakistan, Ufilipino, Qatar, Saudi Arabia, Singapore, Sri Lanka, Uturuki, Falme za Kiarabu, Vietnam, Thailand.
Afrika: Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Kameruni, Cabo Verde, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Comoros, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Côte d'Ivoire, Djibouti, Guinea ya Ikweta, Misri, Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Kenya, Lesotho, Liberia, Libya, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Mayotte, Morocco, Msumbiji, Namibia, Niger, Nigeria, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Ushelisheli, Sierra Leone, Somalia, Afrika Kusini, Tanzania, Togo, Tunisia, Uganda, Sahara Magharibi, Zambia, na Zimbabwe.
Amerika Kaskazini/Kati: Anguilla, Belize, El Salvador, Panama, Jamaica, Bahamas, Barbados, Costa Rica, Dominica, Jamhuri ya Dominica, Nicaragua, Guatemala, Haiti, Honduras, Antigua na Barbuda, Bermuda, Visiwa vya Cayman, Grenada, Mexico, Montserrat, St. Kitts na Nevis, St. Lucia, St. Martin, St. Vincent na Grenadines, Visiwa vya na Turks na Caicos, Visiwa vya Virgin, Saba.
Amerika Kusini: Aruba, Brazil, Argentina, Bolivia, Chile, Colombia, Ecuador, Guyana ya Ufaransa, Guyana, Paraguay, Peru, Trinidad na Tobago, Venezuela, Suriname, Bonaire, Sint Eustatius.
Angalia hali yako ya Premier
Je, ninawezaje kuangalia hali yangu ya Premier?
Unaweza kutazama hali yako ya Exness Premier katika Eneo lako la Binafsi (EB), Programu ya Exness Trade, na programu ya Social Trading. Hivi ndivyo utakavyofanya:
Kwenye EB lako:
- Ingia kwenye EB lako.
- Bofya aikoni ya Wasifu kwenye kona ya juu kulia.
- Bofya Exness Premier.
- Unaweza pia kubofya Mipangilio, na uende kwenye kichupo cha Exness Premier.
Kwenye programu ya Exness Trade:
- Ingia kwenye programu ya Exness Trade.
- Bofya kichupo cha Wasifu.
- Hali yako ya Exness Premier huonyeshwa chini ya Exness Premier.
Kwenye programu ya Social Trading:
- Ingia kwenye programu ya Social Trading.
- Bofya aikoni ya Wasifu.
- Kwenye kona ya juu kushoto, bofya jina lako.
- Hali yako ya Exness Premier huonyeshwa chini ya Uanachama Wako.
Kumbuka: Ikiwa huwezi kuona hali yako ya Exness Premier kwenye menyu ya Wasifu au hauna kichupo cha Exness Premier kwenye eneo la Mipangilio, bado hujatimiza masharti ya chini zaidi ya kuwa mwanachama wa Premier.
Kwa wateja waliotimiza masharti, hali ya Exness Premier itajumuisha taarifa muhimu, kama vile:
- Daraja la sasa
- Tarehe ya kuanza robo ijayo
- Kiungo cha mafao na zawadi za premier
- Vigezo vya kutimiza masharti kwa madaraja yanayoweza kufikiwa
- Kiungo cha Kituo cha Usaidizi kuhusu jinsi ya kufikia daraja linalofuata
- Zana ya ubadilishaji ili kukokotoa tena kiwango cha biashara katika lots za instruments zinazofanyiwa biashara sana
Kwa wateja walio karibu kutimiza masharti, kichupo cha Exness Premier huangazia hali ya Exness Premier inayoweza kufikiwa na taarifa muhimu, kama vile:
- Tarehe ya utathmini wa uanachama
- Vigezo vya kutimiza masharti vya madaraja yanayoweza kufikiwa
- Hatua ya uanachama
Comments
0 comments
Article is closed for comments.