- Je, programu ya Exness Premier ni nini?
- Nchi zinazostahiki kushiriki katika Exness Premier
- Madaraja ya Exness Premier
- Je, nitaangaliaje hadhi yangu ya Exness Premier?
- Vigezo vya kutimiza masharti
- Je, Exness Premier inanifaidi vipi?
Je, programu ya Exness Premier ni nini?
Exness Premier ni programu ya uaminifu wa kuwatuza wanachama wetu wanaoendeleza biashara na waaminifu zaidi wa Exness Premier kwa kuwapa mafao mbalimbali ya kipekee ambayo huongezeka kadiri wanavyotimiza masharti ya madaraja ya juu na ya kifahari zaidi. Utatimiza masharti ya kufikia hadhi ya Exness Premier kulingana na jumla ya pesa ulizoweka kufikia sasa kwenye akaunti yako ya Exness na kiwango cha biashara cha kila robo mwaka.
Nchi zinazostahiki ushiriki wa Exness Premier
Exness Premier inapatikana katika nchi nyingi ambako Exness inafanya kazi. Ikiwa eneo lako limeorodheshwa hapa chini, unaweza kujiunga na programu ya Exness Premier:
Asia: Afghanistan, Bahrain, Bangladesh, Brunei Darussalam, Kambodia, India, Indonesia, Japan, Yordani, Korea Kusini, Kuwait, Laos, Lebanon, Maldivi, Nepal, Oman, Pakistan, Ufilipino, Katari, Saudia, Singapoo, Sri Lanka, Uturuki, Falme za Kiarabu, Vietnamu, Thailandi.
Afrika: Aljeria, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Kameruni, Cabo Verde, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Komoro, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Côte d'Ivoire, Djibouti, Guinea ya Ikweta, Misri, Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Kenya, Lesotho, Liberia, Libya, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Mayotte, Moroko, Msumbiji, Namibia, Niger, Nigeria, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Ushelisheli, Sierra Leone, Somalia, Afrika Kusini, Tanzania, Togo, Tunisia, Uganda, Sahara Magharibi, Zambia na Zimbabwe.
Amerika Kaskazini/Kati: Anguilla, Belize, El Salvador, Panama, Jamaika, Bahamas, Barbados, Kosta Rika, Dominika, Jamhuri ya Dominika, Nikaragua, Guatemala, Haiti, Honduras, Antigua na Barbuda, Bermuda, Visiwa vya Caymen, Grenada, Meksiko, Montserrat, St. Kitts na Nevis, St. Lucia, St. Martin, St. Vincent na Grenadines, Visiwa vya Turks na Caicos, Visiwa vya Virgin, Saba.
Amerika Kusini: Aruba, Brazili, Ajentina, Bolivia, Chile, Kolumbia, Ecuador, French Guiana, Guyana, Paraguay, Peru, Trinidad na Tobago, Venezuela, Suriname, Bonaire, Sint Eustatius.
Madaraja ya Exness Premier
Exness Premier ina madaraja 3 ya uanachama:
-
Premier Preferred
Umeanza sasa kutumia Exness Premier, na utapata mafao na malipo mbalimbali ya kipekee ikiwa ni pamoja na kipaumbele katika huduma kwa wateja, nyenzo za kielimu, uchanganuzi wa biashara wa kitaalamu na ofa maalum.
Ninawezaje kudumisha daraja?
Sharti ufikie Kiwango cha biashara cha kila robo mwaka cha USD milioni 200 ili ustahiki na kudumisha hadhi yako ya Premier Signature.
Ninawezaje kuboresha daraja?
Fikia thamani ya kuweka pesa ya maisha yote ya chini zaidi ya USD 50 000 pamoja na kiwango cha biashara cha kila robo mwaka cha angalau USD milioni 100 ili kuboresha hadhi yako ya Premier Preferred.
-
Premier Elite
Premier Elite ina mafao yote ya Premier Preferred, lakini pia utapokea usaidizi uliobinafsishwa na uliopewa kipaumbele kutoka kwa msimamizi maalum wa akaunti.
Ninawezaje kudumisha daraja?
Sharti ufikie Kiwango cha biashara cha kila robo mwaka cha USD milioni 100 ili kudumisha hadhi ya Premier Elite.
Ninawezaje kuboresha daraja?
Hadhi ya Premier Signature hufikiwa kwa kuweka pesa ya maisha yote ya angalau USD 100 000 na kiwango cha biashara cha kila robo mwaka cha angalau USD milioni 200.
-
Premier Signature
Premier Signature ndilo daraja la kifahari zaidi la Exness Premier, lina fursa za mitandao za kimataifa zenye ufikiaji wa moja kwa moja kwa wasimamizi wetu wa utendaji, na masharti ya kipekee ya biashara. Bila shaka vipengele na mafao yote ya madaraja ya awali yamejumuishwa katika uanachama wa Premier Signature.
Ninawezaje kudumisha daraja?
Sharti ufikie Kiwango cha biashara cha kila robo mwaka cha USD milioni 200 ili kustahiki na kudumisha hadhi yako ya Premier Signature.
Mafao na malipo ya Exness Premier yanaweza kutofautiana kulingana na eneo, na hayawezi kurejeshwa au kubadilishwa kwa pesa taslimu. Iwe imetolewa na Exness au washirika wengine, mafao haya hayawezi kununuliwa, kuuzwa, kubadilishwa au kuhamishwa.
Je, nitaangaliaje hadhi yangu ya Exness Premier?
Unaweza kuangalia hadhi ya uanachama wako wa Premier kwenye menyu ya Profile katika programu ya Exness Trader na kwenye kichupo cha Exness Premier kinachopatikana katika sehemu ya Settings katika Eneo lako la Binafsi la Exness. Hadhi yako ya Exness Premier pia huonyeshwa katika programu ya Social Trading.
Ikiwa huwezi kuona hadhi yako ya Exness Premier katika menyu ya Profile au huna kichupo cha Exness Premier katika sehemu ya Settings , bado hujatimiza masharti ya chini zaidi ili kufikia kuwa mwanachama wa Premier.
Ili kuona hatua ulizopiga ili kufikia Exness Premier, sharti angalau utimize masharti haya:
- Eneo lako la Binafsi sharti liwe liliundwa zaidi ya siku 30 zilizopita.
- Jumla ya pesa ulizoweka katika maisha yote ya akaunti yako inapaswa kuwa zaidi ya USD 15,000.
- Jumla ya kiwango cha biashara cha maisha yote kinapaswa kuwa zaidi ya USD milioni 40.
Kwa wateja waliotimiza masharti, kichupo cha Exness Premier kinapatikana kwenye menyu ya Profile katika programu ya Exness Trader kwenye eneo la Settings la Eneo lako la Binafsi la Exness. Hadhi ya Exness Premier itajumuisha taarifa muhimu, kama vile:
- Daraja la sasa na kipindi cha uanachama
- Masharti ya kudumisha au kufikia hadhi inayofuata inayoweza kufikiwa
- Hatua za uanachama
Kwa wateja walio karibu kutimiza masharti, kichupo cha Exness Premier huonekana katika menyu ya Profile kwenye pogramu ya Exness Trader na kwenye eneo la Settings kwenye Eneo lako la Binafsi la Exness, na inaangazia hadhi ya Exness Premier inayoweza kufikiwa na taarifa muhimu, kama vile:
- Tarehe ya utathmini wa uanachama
- Vigezo vya kutimiza masharti ya madaraja yanayoweza kufikiwa
- Hatua ya uanachama
Vigezo vya kutimiza masharti
Kila daraja la Exness Premier lina masharti ya kipekee ya jumla ya kuweka pesa katika maisha yote na kiwango cha biashara kwa kila robo, na sharti vigezo vyote viwili vitimizwe ili kustahiki katika nchi zote ambako Exness inatumika isipokuwa Uchina, Taiwan, Hong Kong na Macao.
Daraja la Premier | Premier Preferred | Premier Elite | Premier Signature |
---|---|---|---|
Jumla ya pesa zilizoweka katika maisha yote | USD 20 000 | USD 50 000 | USD 100 000 |
Kiwango cha biashara kwa kila robo | USD milioni 50 | USD milioni 100 | USD milioni 200 |
- Pesa zilizowekwa kutoka nje pekee ndizo zinatimiza masharti ya kustahiki pesa zinazowekwa katika maisha yote na uhamishaji wa ndani hautazingatiwa.
- Kuweka pesa za Social Trading na kiwango cha biashara cha orders wazi na zilizofungwa kutoka kwa Wawekezaji hujumuishwa katika ukokotoaji wa kutimiza masharti.
- Ukokotoaji wa kutimiza masharti hautajumuisha kiwango cha biashara kutoka kwa Mameneja wa Portfolio na Wawekezaji, pamoja na pesa zilizowekwa na Wawekezaji.
Ustahiki wa kila robo
Masharti ya daraja la Exness Premier hukokotolewa kwa kila robo ya mwaka wa kalenda, kupitia mchakato kamili uliofafanuliwa kwa kina zaidi hapa chini:
Q1 — Tunakokotoa kiwango cha biashara kuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Machi na jumla ya pesa ulizoweka katika maisha yote kufikia tarehe 31 Machi ili kubaini ustahiki.
Q2 — Mteja hukabidhiwa daraja la Exness Premier kuanzia tarehe 1 Aprili hadi 30 Juni na anastahiki mafao na malipo ya Exness Premier. Tunakokotoa kiwango cha biashara kuanzia tarehe 1 Aprili hadi tarehe 30 Juni na jumla ya pesa za maisha yote kufikia tarehe 30 Juni ili kubaini ikiwa unastahiki tena.
Q3 — Mteja hukabidhiwa daraja la Exness Premier kuanzia tarehe 1 Julai hadi 30 Septemba na anastahiki mafao na malipo ya Exness Premier. Tunakokotoa kiwango cha biashara kuanzia tarehe 1 Julai hadi tarehe 30 Septemba na jumla ya pesa ulizoweka za maisha yote kufikia tarehe 30 Septemba ili kubaini ikiwa unastahiki tena.
Q4 — Mteja hukabidhiwa daraja la Exness Premier kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 31 Desemba na anastahiki mafao na malipo ya Exness Premier. Tunakokotoa kiwango cha biashara kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi tarehe 31 Desemba na jumla ya pesa ulizoweka za maisha yote kufikia tarehe 31 Desemba ili kubaini ikiwa unastahiki tena katika robo ijayo.
Tafadhali kumbuka: haiwezekani kwa mtu kuwa na uanachama zaidi ya mmoja wa Exness Premier. Daraja la juu zaidi la Premier hutumika iwapo utastahiki viwango vingi vya Premier katika Maeneo tofauti ya Binafsi. Ikiwa hungependa kushiriki katika programu ya Exness Premier, tafadhali tuma barua pepe kwa premier@exness.com ili kughairi uanachama wako, na usome sheria na masharti yetu kwa maelezo zaidi.
Je, Exness Premier inanifaidi vipi?
Exness Premier hutambua na kuwalipa wanachama wanaoendeleza biashara na waaminifu zawadi za kipekee na kipaumbele katika usaidizi kutoka kwa timu yetu ya wasimamizi wataalamu wa akaunti. Tungependa ufanikiwe kutrade na Exness, na ufurahie usaidizi wa hali ya juu kwa urahisi. Tunathamini maoni na kuchukua hatua ili kuhakikisha kuwa umeridhika. Kama mwanachama wa Exness Premier, tunakupa kipaumbele zaidi. Kwa maelezo zaidi, unaweza kutembeleaukurasa wetu wa mwanzo wa Exness Premier ili kupata maelezo zaidi kuhusu manufaa ya kipekee utakayopata kama mwanachama wa Exness Premier.