Aina ya usalama ya programu ya uthibitishaji hutumia programu ya uthibitishaji wa wahusika wengine kutengeneza misimbo ya uthibitishaji wakati wowote uthibitishaji wa akaunti unapohitajika.
Google Authenticator ndiyo programu ya uthibitishaji inayopendekezwa kwa aina hii ya usalama, lakini programu nyingi za uthibitishaji za wahusika wengine zinaweza kutumika.
Kuweka mipangilio ya aina ya usalama ya programu ya uthibitishaji
Unaweza kufuata mchakato kama inavyoonyeshwa kwenye Eneo lako la Binafsi (EB) unapochagua aina hii ya usalama, au ufuate hatua za mfumo wako ulio hapa chini.
iOS
+Tutakuonyesha jinsi ya kupakua programu na kuiweka kama aina ya usalama hapa chini:
- Gusa aikoni ya App Store, ili kufungua App Store.
- Tafuta Google Authenticator kwenye upau wa kutafutia. Fungua programu ya Google Authenticator (iliyochapishwa na Google LLC) kutoka kwa matokeo ya utafutaji.
- Chagua programu na uguse Get ili usakinishe. Huenda ukahitaji kuthibitisha programu hiyokwa kutumia Kitambulisho chako cha Apple, Kitambulisho cha Uso au Kitambulisho cha Kugusa.
- Ingia kwenye EB lako, panua Mipangilio, chagua Mipangilio ya usalama kisha Badilisha chini ya Uthibitishaji wa hatua 2.
- Chagua Programu ya uthibitishaji na uthibitishe kwa kubofya Inayofuata.
- Changanua msimbo wa QR kwenye Google Authenticator au uweke jina la akaunti na msimbo wa usalama wewe mwenyewe kwenye programu uliyochagua ya uthibitishaji. Anwani ya barua pepe iliyosajiliwa kwa programu ya uthibitishaji sharti ilingane na anwani iliyosajiliwa ya barua pepe ya Exness, au msimbo wa uthibitishaji huenda ukakosa kutolewa.
- Weka msimbo unaoonyeshwa katika programu yako ya uthibitishaji unapoombwa kwenye EB.
- Ikiwa umewekwa kwa usahihi, utaombwa kuthibitisha akaunti yako kwa kutumia aina yako ya usalama ya sasa.
- Baada ya kuthibitishwa, aina yako ya usalama sasa itawekwa kuwa aina ya usalama ya programu ya uthibitishaji.
Android
+Tutakuonyesha jinsi ya kupakua programu hiyo na kuiweka kama aina ya usalama hapa chini:
- Pakua programu ya Google Authenticator kutoka Google Play (tumia VPN ikihitajika) au programu mbadala ya uthibitishaji kutoka kwa maduka ya programu kama vile:
- Fuata maagizo kwenye skrini ili kusakinisha Google Authenticator (au programu mbadala).
- Ingia kwenye EB lako, panua Mipangilio , chagua Mipangilio ya usalama kisha Badilisha chini ya Uthibitishaji wa hatua 2.
- Chagua Programu ya uthibitishaji na uthibitishe kwa kubofya Inayofuata.
- Changanua msimbo wa QR kwenye Google Authenticator au uweke jina la akaunti na msimbo wa usalama wewe mwenyewe kwenye programu uliyochagua ya uthibitishaji. Anwani ya barua pepe iliyosajiliwa kwa programu ya uthibitishaji sharti ilingane na anwani iliyosajiliwa ya barua pepe ya Exness, au msimbo wa uthibitishaji huenda ukakosa kutolewa.
- Weka msimbo unaoonyeshwa katika programu yako ya uthibitishaji unapoombwa kwenye EB.
- Ikiwa umewekwa kwa usahihi, utaombwa kuthibitisha akaunti yako kwa kutumia aina yako ya usalama ya sasa.
- Baada ya kuthibitishwa, aina yako ya usalama sasa itawekwa kuwa aina ya usalama ya programu ya uthibitishaji.
Jinsi ya kuchanganua msimbo wa QR kwa kutumia Google Authenticator
Msimbo wa QR huonyeshwa kwenye EB wakati wa kusanidi aina hii ya usalama na sharti uchanganuliwe na programu ya uthibitishaji.
Jinsi ya kutengeneza msimbo wa uthibitishaji (TOTP) kwa kutumia Google Authenticator
Msimbo wa uthibitishaji, au Msimbo wa Wakati Mmoja (TOTP), hutolewa kwa ajili ya usanidi wa aina hii ya usalama na madhumuni ya uthibitishaji wa akaunti wakati aina hii ya usalama inatumika.
Kubadilisha aina ya usalama ya uthibitishaji
Inapatikana tu ndani ya siku 30 za kwanza baada ya usajili wa akaunti.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
- Panua Mipangilio, chagua Mipangilio ya usalama kisha Badilisha chini ya Uthibitishaji wa hatua 2.
- Chagua Barua pepe na uthibitishe kwa kubofya Inayofuata.
- Thibitisha akaunti yako ukitumia aina yako ya usalama ya sasa.
- Baada ya kuthibitishwa, aina yako ya usalama sasa itakuwa aina ya usalama ya barua pepe.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
- Panua Mipangilio, chagua Mipangilio ya usalama kisha Badilisha chini ya Uthibitishaji wa hatua 2.
- Chagua Simu au Nambari mpya ya simu na uthibitishe kwa kubofya Inayofuata.
- Option ya nambari mpya ya simu pia itakuomba uweke nambari mpya ya simu ili kuendelea, lakini options zote mbili zitahitaji uthibitishe akaunti yako kwa aina kutumia yako ya sasa ya usalama.
- Baada ya kuthibitishwa, aina yako ya usalama huwekwa kuwa aina ya usalama ya SMS.
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi (EB).
- Panua Mipangilio, chagua Mipangilio ya usalama kisha Badilisha chini ya Uthibitishaji wa hatua 2.
- Chagua Arifa za Programu na uthibitishe kwa kubofya Inayofuata.
- Changanua misimbo ya QR ili usakinishe Exness Trade na uwashe arifa za programu (mwongozo wa kina unapatikana kwenye makala ya arifa ya programu).
- Thibitisha akaunti yako ukitumia aina yako ya usalama ya sasa.
- Baada ya kuthibitishwa, aina yako ya usalama sasa itakuwa aina ya usalama ya arifa za programu.
Kwa masuala ya aina ya usalama, tunapendekeza ufungue tikiti kwenye kituo cha usaidizi kwenye EB kwa usaidizi zaidi.