Furahia fursa ya kujifunza kwa kutumia nyenzo zetu za kina, zilizoundwa ili kuibua udadisi na kukuza maarifa

Utafutaji wa Kawaida:

LeverageSaa za biasharaSwapUwekaji fedhaUtoaji fedhaSpreadAina za akauntiKadi ya benki

Maswali ya kawaida

 • Je, ninaweza kufanya transactions nje ya saa za kazi?

  Ndiyo, unaweza kufanya transactions nje ya saa za kawaida za kazi, hata hivyo, kunaweza kuwa na ucheleweshaji kutoka kwa mtoa huduma wakati wa kuchakata transactions hizi.

 • Je, na nikitoa pesa hadi kwa nambari ya akaunti isiyo sahihi?

  Hili likitokea, ni vyema kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi ili uweze kusaidiwa. Kuna uwezekano wa matukio mawili ambayo yatafuata ukishatoa maelezo yote kuhusu muamala huu:

  • Ikiwa akaunti ya benki ya uliyoweka kimakosa haipo, benki itaturudishia pesa hizi na kisha tutarejesha pesa hizo kwenye akaunti yako; basi unaweza kuondoa fedha hizi kwa mara nyingine.
  • Ikiwa akaunti ya benki ya uliyoweka kimakosa ipo, basi fedha zitawekwa na benki kwenye akaunti hii ya benki na fedha zitapotea; ni muhimu kuthibitisha kila kitu kwa makini ili kuepuka hili kutokea.

 • Je, ninaweza kutoa pesa kwa kutumia njia tofauti ya malipo na ile iliyotumiwa kuziweka?

  Utoaji pesa kwa kawaida huhitaji njia, akaunti ya malipo na sarafu sawa na iliyotumiwa kuziweka. Ikiwa njia nyingi za malipo zinatumiwa kuweka pesa, hatua za utoaji pesa zinapaswa kulenga kuwa sawia katika njia hizi.

  Njia mbadala zinaweza kupatikana kwa traders waliotimiza masharti. Katika hali za kipekee, tunaweza kuondoa kanuni ya kawaida ya uwiano wa utoaji pesa kulingana na uthibitishaji wa akaunti uliofaulu na kuidhinishwa na wataalamu wetu wa malipo.

 • Je, inachukua muda gani kuchakata hatua ya uwekaji au utoaji pesa?

  Muda wa uchakataji huonyeshwa chini ya kila njia ya malipo katika Eneo lako la Binafsi (EB). Muda huu unaweza kutofautiana kulingana na njia ya malipo, kama inavyoonekana kwenye EB. Muda wa uchakataji huonyesha wastani hadi muda wa juu zaidi unaochukuliwa, ilhali muda wa wastani ni muda unaotarajiwa. Kumbuka kwamba hatua za uwekaji fedha zinaweza kuchukua hadi muda wa juu zaidi ulioonyeshwa.

  Njia nyingi za malipo zinazotolewa huonyesha uchakataji wa papo hapo, kumaanisha kuwa transaction hiyo hufanywa ndani ya sekunde chache bila uchakataji wa wataalamu wetu wa idara ya kifedha (sio kwamba transaction hiyo hukamilisha mchakato papo hapo).

  Ikiwa muda wa juu zaidi wa uchakataji umezidishwa, tafadhali wasiliana na Usaidizi ukiwa na Kitambulisho chako cha transaction na uthibitishaji wa kitambulisho kwa usaidizi zaidi.

 • Je, kuna ada zozote zinatozwa na Exness kwa kuweka na kutoa pesa?

  Hapana, hatutozi ada kwa hatua ya kuweka au kutoa pesa. Hata hivyo, baadhi ya mifumo ya malipo ya kielektroniki (EPS) na benki zina ada zao za transaction. Ni vyema zaidi kuthibitisha ada zinazoweza kutozwa kwa njia uliyochagua ya malipo kila wakati kwenye Eneo la Binafsi (EB).

 • Je, vikomo vya kiasi cha pesa kinachoweza kuwekwa ni vipi?

  Vikomo vya transaction huonyeshwa chini ya kila njia ya malipo katika sehemu ya Uwekaji pesa ya Eneo lako la Binafsi (EB). Vikwazo vya ziada vya muda vinaweza kutumika ikiwa una maombi yanayosubiri ya uthibitishaji.

Gundua kategoria zote