Akaunti za kutrade za demo huiga masharti halisi ya biashara lakini hazihitaji pesa halisi ili kufungua orders na kuzifanya kuwa option bora la kufanya mazoezi ya biashara.
Hatutoi akaunti za kutrade za demo kwa aina ya akaunti ya Standard Cent.
Jinsi ya kufungua akaunti ya kutrade ya demo
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Fungua sehemu ya Akaunti Zangu na uchague Fungua Akaunti Mpya.
- Tumia menyu kunjuzi kuchagua jukwaa unalopendelea - MT4 au MT5.
- Chagua aina ya akaunti ya kutrade (Standard Cent haipatikani) kutoka kwa zinazowasilishwa, kisha Endelea.
- Chagua Demo kama aina ya akaunti ambayo ungependa kufungua, kisha ujaze maelezo yafuatayo:
- Leverage ya juu zaidi
- Salio la kuanza
- Sarafu
- Jina wakilishi la akaunti
- Nenosiri la biashara
- Bofya Fungua akaunti.
- Akaunti ya kutrade ya demo inapatikana katika kichupo cha Demo cha sehemu ya Akaunti Zangu.
Jinsi ya kuongeza pesa kwenye akaunti ya kutrade ya demo
- Ingia kwenye Eneo lako la Binafsi.
- Fungua sehemu ya Akaunti Zangu, kisha uchague kichupo cha Demo.
- Bofya Weka Salio kwenye akaunti ya kutrade ya demo ambayo ungependa kuongeza pesa.
- Katika Mwonekano wa gridi, menyu ya nukta 3 inapaswa kufunguliwa ili kupata option ya Kuweka Salio.
- Salio lililowekwa linaweza kuwa chini au juu ya salio la sasa.
- Salio hilo linaweza tu kuwekwa kwenye sarafu ya akaunti ya demo.
- Weka salio ambalo ungependa, kisha uchague Weka Salio ili kuthibitisha.
- Salio jipya la akaunti ya kutrade ya demo limewekwa.
Akaunti za kutrade za demo zinaweza kufunguliwa kwa kutumia programu ya Exness Trade.